Google hulindaje faragha yangu na kuweka maelezo yangu yakiwa salama?

Tunajua usalama na faragha ni muhimu kwako - na ni muhimu kwetu, pia. Tunalipatia suala la kuwa na usalama dhabiti kipaumbele na kukupa imani ya kwamba maelezo yako ni salama na utayapata unapoyahitaji.

Tunaendelea kujitahidi ili kuhakikisha usalama thabiti, kulinda faragha yako, na kufanya Google ikufae zaidi. Tunatumia mamia ya mamilioni ya dola kila mwaka kudumisha usalama, na tumewaajiri wataalamu maarufu katika usalama wa data ili kulinda taarifa zako. Tumebuni pia zana zilizo rahisi kutumia za faragha na usalama kama vile Dashibodi ya Google, uthibitishaji wa hatua mbili na mipangilio ya matangazo yaliyowekewa mapendeleo yanayopatikana katika Kituo Changu cha Matangazo. Kwa hivyo, kuhusu suala la taarifa unazoshiriki na Google, uamuzi huwa ni wako.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu ulinzi na usalama mtandaoni, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kujilinda mwenyewe na familia yako mtandaoni, katika Kituo cha Usalama cha Google .

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyoweka maelezo yako ya kibinafsi yakiwa ya faragha na salama — na kukuweka kwenye usukani.

Kwa nini akaunti yangu inahusishwa na eneo fulani?

Akaunti yako huhusishwa na eneo fulani katika Sheria na Masharti ili tuweze kubaini mambo kadhaa:

  1. Mshirika wa Google anayetoa huduma, anayechakata maelezo yako na anayewajibikia kutii sheria za faragha zinazotumika. Kwa kawaida, Google hutoa huduma zake kwa wateja kupitia mojawapo ya kampuni mbili:
    1. Google Ireland Limited, iwapo unaishi kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (nchi za Umoja wa Ulaya pamoja na Aisilandi, Lishensteni na Norwe) au Uswizi
    2. Google LLC, inayopatikana Marekani, kwa nchi nyingine zote zilizosalia
  2. Toleo la sheria na masharti yanayosimamia uhusiano wetu, ambayo yanaweza kutofautiana kulingana na sheria za mahali uliko
  3. Utumiaji wa masharti ya eneo mahususi katika huduma za Google mahali unakoishi

Kubaini eneo linalohusishwa na akaunti yako

Unapofungua akaunti mpya, tunahusisha akaunti yako na eneo kulingana na mahali ulipofungulia Akaunti yako ya Google. Kwa akaunti ambazo zimedumu kwa angalau mwaka mmoja, tunatumia eneo ambako kwa kawaida wewe hutumia huduma za Google — kwa kawaida huwa ni mahali ambako umekaa kwa muda mrefu katika mwaka mmoja uliopita.

Hali ya kusafiri mara kwa mara kwa kawaida haiathiri eneo linalohusishwa na akaunti yako. Ukihamia katika eneo lingine, inaweza kuchukua takribani mwaka mmoja kabla ya eneo linalohusishwa na akaunti yako kusasishwa.

Iwapo eneo linalohusishwa na akaunti yako halilingani na eneo unakoishi, hali hii inaweza kutokana na tofauti kati ya eneo unakofanyia kazi na eneo unakoishi, kwa sababu umeweka Mtandao Pepe wa Faragha (VPN) ili kuficha anwani yako ya IP, au kwa sababu unaishi karibu na mpaka wa eneo. Ikiwa hukubali eneo linalohusishwa na akaunti yako, tuma ombi la kubadilisha eneo lako.

Ninawezaje kuondoa maelezo kunihusu kutoka matokeo ya utafutaji ya Google?

Matokeo ya utafutaji Google ni mfano wa maudhui yanayopatikana na umma kwenye wavuti. Mitambo ya kutafuta haiwezi kuondoa maudhui moja kwa moja kutoka kwa tovuti, kwa hivyo kuondoa matokeo ya utafutaji kutoka Google hakuwezi kuondoa maudhui kwenye tovuti. Ikiwa unataka kuondoa chochote kwenye wavuti, unafaa kuwasiliana na msimamizi wa wavuti wa tovuti ambayo maelezo yamechapishwa na umuulize abadilishe. Maudhui yanapoondolewa na Google imetambua mabadiliko, maelezo hayatapatikana katika matokeo ya utafutaji ya Google. Kama una ombi la dharura la kuondoa maudhui, unaweza pia kutembelea ukurasa wetu wa usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Je, hoja zangu za utafutaji hutumwa kwenye tovuti ninapobofya matokeo kwenye huduma ya Tafuta na Google?

Kwa kawaida, hapana. Unapobofya tokeo la utafutaji katika huduma ya Tafuta na Google, kivinjari chako hutuma maelezo fulani kwenye ukurasa wa wavuti unaolengwa. Hoja zako za utafutaji zinaweza kuonekana kwenye anwani ya Intaneti, au URL, ya ukurasa wa matokeo ya utafutaji, lakini huduma ya Tafuta na Google inanuia kuzuia vivinjari visitume URL hiyo kwenye ukurasa unaolengwa kama URL ya Anayeelekeza. Tunatoa data kuhusu hoja za utafutaji kupitia Google Trends na Dashibodi ya Utafutaji wa Google, lakini tunapofanya hivyo, tunajumlisha hoja pamoja ili tushiriki tu hoja zinazotolewa na watumiaji wengi.

Programu za Google
Menyu kuu