Hili ni toleo lililohifadhiwa la Sera yetu ya Faragha. Tazama toleo la sasa au matoleo yote ya awali.

Sera ya Faragha

Ilibadilishwa mwisho tarehe: 20 Desemba 2013 (angalia matoleo yaliyohifadhiwa)

Kuna njia nyingi tofauti za kutumia huduma zetu – kutafuta na kushiriki habari, kuwasiliana na watu wengine au kubuni maudhui mapya. Unaposhiriki habari nasi, kwa mfano kwa kufungua Akaunti ya Google, tunaweza kuboresha huduma hizo hata zaidi – kukuonyesha matokeo ya utafutaji na matangazo yanayofaa zaidi, kukusaidia ujumuike na watu wengine au kurahisisha kushiriki na wengine kwa haraka zaidi. Unapotumia huduma zetu, tunataka uelewe jinsi tunavyotumia maelezo na njia ambazo unaweza kutumia kulinda faragha yako.

Sera yetu ya Faragha inaeleza:

 • Maelezo gani tunayoyakusanya na sababu gani tunayakusanya.
 • Jinsi tunavyoyatumia maelezo hayo.
 • Chaguo tunazokupa, pamoja na jinsi ya kufikia na kusasisha maelezo.

Tumejaribu kuiweka rahisi iwezekanavyo, lakini kama hujazoea maneno kama vidakuzi, anwani za IP, lebo za pikseli na vivinjari, basi soma kuhusu maneno haya muhimu kwanza. Faragha yako ni muhimu kwa Google kwa hivyo uwe mgeni kwa Google au mtumiaji wa muda mrefu, tafadhali chukua muda wa kufahamu desturi zetu – na ikiwa una maswali yoyote angalia ukurasa huu.

Maelezo tunayokusanya

Tunayakusanya maelezo ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu wote – kutoka kubashiri mambo ya msingi kama ni lugha ipi unayozungumza, hadi mambo magumu zaidi kama ni matangazo yapi utakayoona kuwa yana manufaa zaidi au watu ambao unawajali zaidi mtandaoni.

Tunakusanya maelezo kwa njia mbili:

 • Maelezo unayotupa. Huduma zetu nyingi zinahitaji ujisajili kwenye Akaunti ya Google. Unapofanya hivyo, tutakuuliza maelezo ya kibinafsi, kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, nambari ya simu au kadi ya mkopo. Kama unataka kupata manufaa kamili ya vipengee vya kushiriki tunavyozitoa, tunaweza kukuomba ubuni Maelezo Yako Mafupi ya Google yatakayokuwa wazi kwa umma, ambayo yanaweza kujumuisha jina lako na picha yako.

 • Maelezo tunayopata kutokana na matumizi yako ya huduma zetu. Tunaweza kukusanya maelezo kuhusu huduma unazotumia na jinsi unavyozitumia, kama wakati unapotembelea tovuti ambayo inatumia huduma zetu za matangazo au unapoangalia na kuingiliana na matangazo yetu na maudhui yake. Maelezo hayo ni pamoja na:

  • Maelezo kuhusu kifaa

   Tunaweza kukusanya maelezo mahususi ya kifaa (kama vile aina ya kifaa chako, toleo la mfumo wa uendeshaji, vitambulisho vya kipekee vya kifaa, na maelezo ya mtandao wa simu ya mkononi yakiwa ni pamoja na namba ya simu). Google inaweza kuhusisha vitambulishi vya kifaa chako au nambari yako ya simu kyenye Akaunti yako ya Google.

  • Maelezo ya kumbukumbu

   Unapotumia huduma zetu au kutazama maudhui yaliyotolewa na Google, tunaweza kukusanya na kuhifadhi maelezo fulani kiotomatiki katika kumbukumbu za seva. Maelezo hayo yanaweza kujumuisha:

   • maelezo ya jinsi ulivyotumia huduma yetu, kama vile hoja zako za utafutaji.
   • maelezo ya kumbukumbu ya simu kama vile nambari yako ya simu, nambari ya anayekupigia, nambari za kusambaza kwa simu, saa na tarehe simu ilipopigwa, muda uliotumika kuongea kwenye simu, maelezo ya kutuma SMS na aina ya simu zilizopigwa.
   • Anwani ya Itifaki Wavuti (IP).
   • Maelezo ya matukio kwenye kifaa kama kukwama kwa kifaa, utendakazi wa mfumo, mipangilio ya maunzi, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na saa ya ombi lako na URL marejeleo.
   • vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari chako au Akaunti yako ya Google kwa njia ya kipekee.
  • Maelezo ya eneo

   Unapotumia huduma ya Google iliyo na uwezo wa kufikia eneo, tunaweza kukusanya na kuchakata maelezo ya mahali hasa ulipo, kama mawimbi ya GPS yanayotumwa na simu ya mkononi. Tunaweza pia kutumia teknolojia mbalimbali kama vile data ya vifaa vya kunasa kwenye kifaa chako ambacho kwa mfano kinaweza kutoa maelezo kuhusu vituo vya ufikiaji wa Wi-Fi na na minara ya simu iliyo karibu.

  • Nambari za kipekee za programu

   Baadhi ya Huduma hujumuisha nambari ya kipekee ya programu. Nambari hii pamoja na maelezo kuhusu usakinishaji wako (kwa mfano, aina ya mfumo wa uendeshaji na nambari ya toleo la programu) huenda vikatumwa kwa Google unapoweka au kuondoa huduma hiyo au wakati huduma hiyo inapowasiliana mara kwa mara na seva zetu, kama vile kupata visasisho vya kiotomatiki.

  • Hifadhi ya ndani

   Tunaweza kukusanya na kuhifadhi maelezo (pamoja na maelezo ya kibinafsi) yaliyo kwenye kifaa chako kwa kutumia taratibu kama vile hifadhi ya kivinjari kwenye wavuti (pamoja na HTML 5) na akibisho ya data ya programu.

  • Vidakuzi na vitambulishi visivyojulikana

   Tunatumia teknolojia mbalimbali kukusanya na kuhifadhi maelezo unapotembelea huduma ya Google na hii inaweza kujumuisha kutuma kidakuzi kimoja au zaidi au vitambulishi visivyojulikana kwa kifaa chako. Pia tunatumia vidakuzi na vitambulishi visivyojulikana unapoingiliana na huduma tunazotoa kwa washirika wetu, kama vile huduma za matangazo au vipengee vya Google vinavyoweza kuonekana kwenye tovuti zingine.

Jinsi tunavyotumia maelezo tunayoyakusanya

Tunatumia maelezo tunayokusanya kwenye huduma zetu zote kutoa, kudumisha, kulinda na kuboresha huduma hizo, kubuni zingine mpya na kulinda Google na watumiaji wetu. Pia tunatumia maelezo haya kukupa maudhui ya kukufaa – kama vile matangazo na matokeo mwafaka zaidi ya utafutaji.

Tunaweza kutumia jina unalotoa kwenye Maelezo yako Mafupi ya Google kwenye huduma zote tunazotoa ambazo zinahitaji Akaunti ya Google. Zaidi ya hayo, tunaweza kubadilisha majina ya awali yanayohusishwa na Akaunti yako ya Google ili uwakilishwe kwa njia sawa kwenye huduma zetu zote. Ikiwa watumiaji wengine tayari wana barua pepe yako, au maelezo mengine ambayo yanakutambulisha, tunaweza kuwaonyesha Maelezo yako Mafupi ya Google yanaoonekana kwa umma, kama vile jina na picha yako.

Unapowasiliana na Google, tunaweza kuweka rekodi ya mawasiliano yako ili kukusaidia kutatua matatizo yoyote unayoweza kuwa ukipitia. Tunaweza kutumia anwani yako ya barua pepe kukujulisha kuhusu huduma zetu, kama vile kukujulisha kuhusu mabadiliko yanayokuja au uboreshaji.

Tunatumia maelezo yaliyokusanywa kutokana na vidakuzi na teknolojia zingine, kama lebo za pikseli, ili kuboresha uzoefu wako wa matumizi na ubora wa kijumla wa huduma zetu. Kwa mfano, kwa kuhifadhi mapendeleo yako ya lugha, tutaweza kufanya huduma zetu zionekane kwa lugha unayoipendelea. Tunapokuonyesha matangazo yanayokulenga, hatutahusisha kidakuzi au kitambulishi kisichojulikana na mambo nyeti kama vile asili, dini, mwelekeo wa kijinsia au afya.

Tunaweza kuunganisha maelezo ya kibinafsi ambayo umetupa kwenye huduma moja, yakiwemo maelezo ya kibinafsi, na maelezo kutokana na huduma zingine za Google – kwa mfano kukurahisishia kushiriki vitu na watu unaowajua. Hatutachanganya maelezo ya kidakuzi cha DoubleClick na maelezo yanayoweza kukutambulisha kibinafsi kama hatuna idhini yako kuwa umechagua hivyo.

Tutaomba ruhusa yako kabla ya kutumia maelezo kwa madhumuni mengine yoyote kando na yale yaliyowekwa katika Sera hii ya Faragha.

Google huchakata maelezo ya kibinafsi kwenye seva zetu katika nchi nyingi duniani. Tunaweza kuchakata maelezo yako ya kibinafsi kwenye seva iliyo nje ya nchi unamoishi.

Uwazi na chaguo

Watu wana shauku tofauti za faragha. Lengo letu ni kuwa na uwazi kuhusu ni maelezo yapi tunayoyakusanya, ili uwezo kufanya uamuzi wa maana kuhusu jinsi yanavyotumika. Kwa mfano, unaweza:

 • Kukagua na kudhibiti aina fulani ya maelezo yaliyowekwa kwenye Akaunti yako ya Google kwa kutumia Dashibodi ya Google.
 • Tazama na uhariri mapendeleo yako kuhusu matangazo yanayoonyeshwa kwako kwenye Google na katika wavuti, kama vile aina ambazo zinazoweza kukuvutia, kwa kutumia Mipangilio ya Matangazo. Hapa, unaweza pia kuamua kujitoa kwenye baadhi ya huduma za matangazo ya Google.
 • Tumia kihariri chetu ili kuona na kurekebisha jinsi Maelezo yako Mafupi ya Google hutokea kwa watu binafsi.
 • Dhibiti nani unayeshirikisha naye habari.
 • Faidika na maelezo kutoka kwenye huduma zetu nyingi.

Unaweza pia kupanga kipitiaji chako kizuie kuki zote, pamoja na kuki zinazohusiana na huduma zetu, au kuonyesha ni wakati gani kuki inapangwa na sisi. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba huduma zetu nyingi zinaweza zisifanye kazi vizuri kama kuki zako zimeondolewa uwezo. Kwa mfano, tunaweza tusikumbuke hiari yako ya lugha.

Maelezo unayoshirikisha

Nyingi ya huduma zetu zinakuruhusu ushiriki maelezo na watu wengine. Kumbuka kwamba unaposhirikisha maelezo kadamnasini, yanaweza kufahirisiwa na injini za utafutaji, ikiwemo Google. Huduma zetu hukupa hiari tofauti za kushiriki na kuondoa maudhui yako.

Kufikia na kusasisha maelezo yako binafsi

Wakati wo wote unapotumia huduma zetu, tunalenga kukupa ufikiaji wa maelezo yako ya kibinafsi Kama maelezo hayo sio sahihi, tunajitahidi kukupa njia za kusasisha haraka au kuyafuta – isipokuwa iwe tunatakikana tuyaweke maelezo hayo kwa ajili ya biashara za kihalali au madhumuni ya kisheria. Unaposasisha maelezo ya kibinafsi, tunaweza kukuomba uthibitishe utambulisho wako kabla hatujaweza kushughulikia ombi lako.

Tunaweza kukataa maombi ambayo yanajirudiarudia kupindukia, yanayohitaji juhudi zisizofaa za kiufundi (kwa mfano, kutengeneza mfumo mpya au kubadilisha kimsingi desturi yoyote iliyopo), yanayohatarisha faragha ya wengine, au yasiyofaa kabisa (kwa mfano, maombi yanayohusu maelezo ya mifumo ya hifadhi rudufu).

ambapo tunaweza kutoa maelezo ya utumiaji na usahihishaji , tutafanya hivyo bila malipo, isipokuwa pale itahitaji juhudi kubwa mno. kudumisha huduma zetu kwa njia ambayo inalinda habari kutokana na uharibifu wa maelezo ama kwa bahati mbaya au kwa kukusudia. Kwa sababu hii, baada ya kufuta maelezo kutoka kwenye huduma zetu, huenda tusifute mara moja nakala zilizosalia kutoka kwa seva zetu amilifu na huenda tusitoe maelezo kutoka kwa mifumo yetu yenye nakala saidizi.

Maelezo tunayoshirikisha

Hatushirikishi maelezo ya kibinafsi na kampuni, mashirika, na watu binafsi nje ya Google isipokuwa mojawapo ya hali zifuatazo itokee:

 • Kwa idhini yako

  Tutashirikisha maelezo ya kibinafsi na kampuni, mashirika, na watu wa nje ya Google tukiwa na idhini yako ya kufanya hivyo. Tunahitaji kibali cha uamuzi wa kuingia cha kushirikisha maelezo yoyote nyeti ya kibinafsi.

 • Na wasimamizi wa kikoa

  Kama Akaunti ya Google yako imedhibitiwa na msimamizi wa kikoa(kwa mfano, kwa watumiaji wa Google Apps) basi msimamizi wako wa kikoa chako na wauzaji ambao hutoa usaidizi wa kiufundi kwa watumiaji kwenye shirika lako watafikia maelezo ya akaunti yako ya Google (zikiwemo barua pepe na data zingine). Msimamizi wako wa kikoa anaweza pia:

  • kuona takwimu kuhusu akaunti yako, kama takwimu zinazohusu programu unazosakinisha.
  • kubadilisha nenosiri la akaunti yako.
  • kusitisha au kukomesha ufikiaji wa akaunti yako.
  • kufikia au kuweka maelezo yaliyohifadhiwa kama sehemu ya akaunti yako.
  • kupokea maelezo ya akaunti yako ili kuridhisha sheria inayotumika, kanuni, mchakato wa sheria, au ombi la kulazimishwa kutoka kwa serikali.
  • kuzuia uwezo wako wa kufuta au kuhariri maelezo au kupanga faragha.

  Tafadhali rejelea sera ya faragha ya msimamizi wako wa kikoa kwa maelezo zaidi.

 • Kwa mchakato wa nje

  Tunatoa maelezo ya kibinafsi kwa washirika wetu wadogo au biashara zingine tunazoamini au watu ili kuichakata kwa niaba yetu, kulingana na maagizo yetu na kwa kufuata Sera yetu ya Faragha na hatua zingine zozote zinazofaa za faragha na usalama.

 • Kwa sababu za kisheria

  Tutashirikisha maelezo ya kibinafsi na makampuni, mashirika au watu walioko nje ya Google ikiwa tuna imani kwamba ufikiaji, matumizi, uhifadhi au ufichuzi wa maelezo hayo ni muhimu ili:

  • kutimiza sheria yoyote husika, masharti, mchakato wa kisheria au ombi linaloweza kutekelezwa la kiserikali
  • kutekeleza Masharti husika ya Huduma, ikiwa ni pamoja na uchungzi wa ukiukaji unaowezekana kutokea.
  • kugundua, kuzuia, au kushughulikia ulaghai, masuala ya usalama au kiufundi.
  • kulinda dhidi ya madhara ya haki, mali au usalama wa Google, watumiaji wetu au umma kama inavyotakikana au kuruhusiwa na sheria.

Tunaweza tukashirikisha, habari kwa jumla isiyoweza kutambulisha mtu hadharani na wenzetu – kama vile wachapishaji, watangazaji wa biashara au tovuti zilizounganishwa. Kwa mfano, tunaweza kushirikisha habari kwa umma ili kuonyesha mitindo kuhusu utumiaji wa jumla wa huduma zetu.

Kama Google itahusishwa katika muungano na kampuni zingine, kuchukuliwa au kufilisishwa, tutaendelea kuhakikisha usiri wa habari yoyote ya kibinafsi na kuwapa watumiaji walioathiriwa ilani kabla maelezo ya kibinafsi hayajahamishwa au kuwekwa chini ya sera tofauti ya faragha.

Usalama wa maelezo

Tunafanya bidii kulinda Google na watumiaji wetu dhidi ya ufikiaji ambao haujaidhinishwa au mabadiliko yasiyoidhinishwa, uchakachuaji haramu au uharibifu wa maelezo tuliyoweka. Hasusani

 • Huduma zetu nyingi tunazisimbisha tukitumia SSL.
 • Unapotaka kuingia kwenye Akaunti yako ya Google, tunakuhitaji ujithibitishe mara mbili,na chombo Kipitiaji Salama cha Google Chrome
 • Tunatathmini mkusanyo wetu wa maelezo, uhifadhi na desturi za kuyashughulikia, zikiwemo askari wa usalama kulinda, dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa kwenye mitambo.
 • Tunazuia ufikiaji wa maelezo ya kibinafsi kwa waajiriwa wa Google, wakandarasi na mawakala ambao wanahitaji kujua maelezo hayo ili kuichakata kwa niaba yetu, na ambao wako chini ya majukumu makali ya mkataba ya faragha na wanaweza wakaadhibiwa au kufutwa kazi ikiwa watashindwa kuyatimiza majukumu haya.

Matumizi

Sera yetu ya Faragha hutumika kwa huduma zote zinazotolewa na Google Inc. na wenzake wadogo, ikiwa ni pamoja na huduma zinazotolewa kwenye tovuti zingine (kama vile huduma zetu za matangazo ya kibiashara), lakini haijumuishi huduma ambazo zina sera tofauti za faragha ambazo hazijumuishi Sera hii ya Faragha.

Sera yetu ya Faragha haitumiki kwenye huduma zinazotolewa na makampuni mengine au watu binafsi, ikiwa ni pamoja na bidhaa au tovuti ambazo zinaweza kuonyeshwa kwako kama matokeo ya utafutaji, tovuti ambazo zinaweza kujumuisha huduma za Google, au tovuti zingine zinazounganishwa kutokana na huduma zetu Sera yetu ya Faragha haishughulikii utumiaji wa maelezo ya makampuni na mashirika mengine ambayo yanatangaza huduma zetu, na ambao wanaweza kutumia kuki, vibandiko vya pikseli na teknolojia zingine ili kuhudumia na kutoa matangazo husika.

Utekelezaji

Tunatathmini mara kwa mara azma yetu ya kutii Sera yetu ya Faragha. Tunafuata pia mifumo kadhaa inayojidhibiti. Wakati tunapopokea malalamiko rasmi kimaandishi, tutawasiliana na mtu aliyetoa malalamiko hayo ili tufuatilie Tunafanya kazi na mamlaka dhibiti husika, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kulinda data za eneo, ili kutatua malalamiko yoyote kuhusiana na uhamishaji wa data za kibinafsi, ambayo hatuwezi kuyatatua na watumiaji wetu moja kwa moja.

Mabadiliko

Sera yetu ya Faragaha inaweza kubadilika mara kwa mara. Hatutapunguza haki zako chini ya Sera ya Faragha hii bila idhini yako dhahiri. Tutachapisha mabadiliko yoyote ya sera ya faragha kwenye ukurasa huu na, kama mabadiliko ni muhimu, tutatoa taarifa inayoonekana zaidi (inayojumuisha, kwa huduma fulani, taarifa ya barua pepe ya mabadiliko ya sera ya faragha). Pia tutaweka toleo za awali za Sera ya Faragha hii katika kumbukumbu kwa tathmini yako.

Desturi maalumu za bidhaa

Taarifa zifuatazo zinaelezea desturi maalumu za faragha kulingana na bidhaa fulani za Google na huduma unazoweza kutumia:

Programu za Google
Menyu kuu