Hili ni toleo lililohifadhiwa la Sera yetu ya Faragha. Tazama toleo la sasa au matoleo yote ya awali.

Sera ya Faragha

Ilibadilishwa mwisho tarehe: 28 Juni 2016 (angalia matoleo yaliyohifadhiwa)

Kuna njia nyingi tofauti za kutumia huduma zetu – kutafuta na kushiriki habari, kuwasiliana na watu wengine au kubuni maudhui mapya. Unaposhiriki habari nasi, kwa mfano kwa kufungua Akaunti ya Google, tunaweza kuboresha huduma hizo hata zaidi – kukuonyesha matokeo ya utafutaji na matangazo yanayofaa zaidi, kukusaidia ujumuike na watu wengine au kurahisisha kushiriki na wengine kwa haraka zaidi. Unapotumia huduma zetu, tunataka uelewe jinsi tunavyotumia maelezo na njia ambazo unaweza kutumia kulinda faragha yako.

Sera yetu ya Faragha inaeleza:

  • Maelezo gani tunayoyakusanya na sababu gani tunayakusanya.
  • Jinsi tunavyoyatumia maelezo hayo.
  • Chaguo tunazokupa, pamoja na jinsi ya kufikia na kusasisha maelezo.

Tumejaribu kuifanya rahisi iwezekanavyo, lakini kama hujazoea istilahi kama vile vidakuzi, anwani za IP), lebo za pikseli na vivinjari, basi soma kuhusu istilahi hizi muhimu kwanza. Faragha yako ni muhimu kwa Google kwa hivyo uwe ni mgeni kwetu au mtumiaji wetu wa muda mrefu, tafadhali chukua nafasi ujifahamishe kuhusu desturi zetu – na kama una maswali yoyote wasiliana nasi.

Maelezo tunayokusanya

Sisi hukusanya maelezo ili kutoa huduma bora kwa watumiaji wetu wote – kuanzia kuelewa mambo ya kawaida kama lugha unayoongea, hadi mambo changamani zaidi kama matangazo utakayoyapata kuwa muhimu sana, watu muhimu sana kwako mtandaoni, au video za YouTube unazoweza kupenda.

Sisi hukusanya maelezo kwa njia zifuatazo:

  • Maelezo unayotupa. Kwa mfano, huduma zetu nyingi zinahitaji ujisajili kwenye Akaunti ya Google. Unapofanya hivyo, tutakuuliza maelezo ya kibinafsi,kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, nambari ya simu au kadi ya mkopo ili kuhifadhi pamoja na akaunti yako. Kama unataka kupata manufaa kamili ya vipengee vya kushiriki tunavyotoa, tunaweza kukuomba ubuni Wasifu kwenye Google utakaokuwa wazi kwa umma, ambao unaweza kujumuisha jina lako na picha.

  • Maelezo tunayoyapata kutokana na matumizi yako ya huduma zetu. Tunakusanya maelezo kuhusu huduma ambazo unatumia na jinsi unavyozitumia, kama wakati unapotazama video kwenye YouTube, unapotembelea tovuti ambayo hutumia huduma zetu za utangazaji, au unapotazama na kushirikiana na matangazo na maudhui yetu. Maelezo hayo ni pamoja na:

    • Maelezo kuhusu kifaa

      Tunakusanya maelezo yanayohusu kifaa (kama vile modeli ya maunzi yako, toleo la mfumo wa uendeshaji, vitambulishi vya kipekee vya kifaa, na maelezo ya mtandao wa simu ikiwa ni pamoja na nambari ya simu). Google inaweza kuhusisha vitambulishi vya kifaa chako au nambari yako ya simu na Akaunti yako ya Google.

    • Maelezo ya kumbukumbu

      Wakati unapotumia huduma zetu au kutazama maudhui yaliyotolewa na Google, sisi hukusanya na kuhifadhi maelezo mengine kiotomatiki kwenye kumbukumbu za seva. Hii ni pamoja na:

      • maelezo ya jinsi ulivyotumia huduma yetu, kama vile hoja zako za utafutaji.
      • maelezo ya kumbukumbu ya simu kama vile nambari yako ya simu, nambari ya anayekupigia, nambari za kusambaza kwa simu, saa na tarehe simu ilipopigwa, muda uliotumika kuongea kwenye simu, maelezo ya kutuma SMS na aina ya simu zilizopigwa.
      • Anwani ya Itifaki Wavuti (IP).
      • Maelezo ya matukio kwenye kifaa kama kukwama kwa kifaa, utendakazi wa mfumo, mipangilio ya maunzi, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na saa ya ombi lako na URL marejeleo.
      • vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari chako au Akaunti yako ya Google kwa njia ya kipekee.
    • Maelezo ya eneo

      Wakati unapotumia huduma za Google, tunaweza kukusanya na kuchakata maelezo kuhusu eneo lako halisi. Tunatumia teknolojia mbalimbali kubainisha eneo, ikiwa ni pamoja na anwani ya IP, GPS, na vifaa vingine vya kubaini ambavyo, kwa mfano, vinaweza kupea Google maelezo kuhusu vifaa vilivyo karibu, maeneo ya kufikia Wi-Fi na minara ya mitandao.

    • Nambari za kipekee za programu

      Baadhi ya Huduma hujumuisha nambari ya kipekee ya programu. Nambari hii pamoja na maelezo kuhusu usakinishaji wako (kwa mfano, aina ya mfumo wa uendeshaji na nambari ya toleo la programu) huenda vikatumwa kwa Google unapoweka au kuondoa huduma hiyo au wakati huduma hiyo inapowasiliana mara kwa mara na seva zetu, kama vile kupata visasisho vya kiotomatiki.

    • Hifadhi ya ndani

      Tunaweza kukusanya na kuhifadhi maelezo (pamoja na maelezo ya kibinafsi) yaliyo kwenye kifaa chako kwa kutumia taratibu kama vile hifadhi ya kivinjari kwenye wavuti (pamoja na HTML 5) na akiba ya data ya programu.

    • Vidakuzi na teknolojia sawa

      Sisi na washirika wetu hutumia teknolojia mbalimbali kukusanya na kuhifadhi maelezo wakati unapotembelea huduma ya Google, na huenda hii ikajumuisha kutumia vidakuzi na teknolojia sawa ili kutambua kivinjari au kifaa chako. Tunatumia pia teknolojia hizi kukusanya na kuhifadhi maelezo wakati unapowasiliana na huduma tunazotoa kwa washirika wetu, kama vile huduma za matangazo au vipengee vya Google vinavyoweza kuonekana kwenye tovuti nyingine. Bidhaa yetu ya Uchanganuzi wa Google husaidia biashara na wamiliki wa tovuti kuchanganua trafiki kwenye tovuti na programu zao. Wakati inapotumiwa pamoja na huduma za utangazaji, kama zile zinazotumia kidakuzi cha DoubleClick, maelezo ya Uchanganuzi wa Google huunganishwa, na mteja wa Uchanganuzi wa Google au na Google, kwa kutumia teknolojia ya Google, na maelezo kuhusu matembeleo ya tovuti mbalimbali.

Maelezo tunayokusanya unapoingia katika akaunti ya Google pamoja na maelezo tunayokusanya kukuhusu kutoka kwa washirika, yanaweza kuhusishwa na Akaunti yako ya Google. Maelezo yanapohusishwa na Akaunti yako ya Google, tunayashughulikia kama maelezo ya kibinafsi. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kufikia, kudhibiti, au kufuta maelezo yanayohusishwa na Akaunti yako ya Google, tembelea sehemu ya Uwazi na chaguo ya sera hii.

Jinsi tunavyotumia maelezo tunayoyakusanya

Tunatumia maelezo tunayokusanya kwenye huduma zetu zote kutoa, kudumisha, kulinda na kuboresha huduma hizi, kubuni nyingine mpya, na kulinda Google na wateja wetu. Pia tunatumia maelezo haya kukupa maudhui ya kukufaa – kama vile matangazo na matokeo mwafaka zaidi ya utafutaji.

Tunaweza kutumia jina unalotoa kwenye Maelezo yako Mafupi ya Google kwenye huduma zote tunazotoa ambazo zinahitaji Akaunti ya Google. Zaidi ya hayo, tunaweza kubadilisha majina ya awali yanayohusishwa na Akaunti yako ya Google ili uwakilishwe kwa njia sawa kwenye huduma zetu zote. Ikiwa watumiaji wengine tayari wana barua pepe yako, au maelezo mengine ambayo yanakutambulisha, tunaweza kuwaonyesha Maelezo yako Mafupi ya Google yanaoonekana kwa umma, kama vile jina na picha yako.

Ikiwa una Akaunti ya Google, huenda tukaonyesha jina lako la Wasifu, picha ya Wasifu, na vitendo vyako kwenye Google au kwenye programu zingine zilizounganishwa kwenye Akaunti yako ya Google (kama vile +1, ukaguzi unaoandika na maoni unayochapisha) katika huduma zetu, ikiwa ni pamoja na kuonyesha katika matangazo na miktadha mingine ya kibiashara. Tutaheshimu chaguo zako zakuzuia mipangilio ya kushiriki au mwonekano katika Akaunti yako ya Google.

Wakati unapowasiliana na Google, tunaweka rekodi ya mawasiliano yako ili kusaidia kutatua masuala yoyote unayoweza kukabiliana nayo. Tunaweza kutumia anwani yako ya barua pepe kukujulisha kuhusu huduma zetu, kama vile kukujulisha kuhusu mabadiliko yanayokuja au uboreshaji.

Tunatumia maelezo yaliyokusanywa kutokana na vidakuzi na teknolojia zingine, kama lebo za pikseli, ili kuboresha matumizi yako na ubora wa kijumla wa huduma zetu. Moja ya bidhaa tunazotumia kufanya hivi kwenye huduma zetu wenyewe ni Uchanganuzi wa Google. Kwa mfano, kwa kuhifadhi mapendeleo yako ya lugha, tutaweza kufanya huduma zetu zionekane kwa lugha unayopendelea. Tunapokuonyesha matangazo yanayokulenga, hatutahusisha kitambulishi kwenye vidakuzi au teknolojia sawa na mambo nyeti, kama vile rangi, dini, mwelekeo wa ngono au afya.

Mifumo yetu ya kiotomatiki huchanganua maudhui yako (ikiwa ni pamoja na barua pepe) ili kukupa kibinafsi vipengele husika vya bidhaa, kama vile matokeo ya utafutaji yaliobinafsishwa, utangazaji ulio binafsishwa, na ugunduaji wa barua taka na programu hasidi.

Huenda tukaunganisha maelezo ya kibinafsi kutoka huduma moja na maelezo, yakiwemo maelezo ya kibinafsi, kutoka huduma zingine za Google - kwa mfano kukurahisishia kushiriki vitu na watu unaowajua. Kulingana na mipangilio ya akaunti yako, shughuli zako kwenye tovuti na programu nyingine huenda zikahusishwa na maelezo yako ya kibinafsi ili kuimarisha huduma za Google na matangazo yanayotolewa na Google.

Tutaomba ruhusa yako kabla ya kutumia maelezo kwa madhumuni mengine yoyote kando na yale yaliyowekwa katika Sera hii ya Faragha.

Google huchakata maelezo ya kibinafsi kwenye seva zetu katika nchi nyingi duniani. Tunaweza kuchakata maelezo yako ya kibinafsi kwenye seva iliyo nje ya nchi unamoishi.

Uwazi na chaguo

Watu wana shauku tofauti za faragha. Lengo letu ni kuwa na uwazi kuhusu ni maelezo yapi tunayoyakusanya, ili uwezo kufanya uamuzi wa maana kuhusu jinsi yanavyotumika. Kwa mfano, unaweza:

  • Kagua na usasishe vidhibiti vyako vya shughuli za Google ili uamue ni aina gani ya data, kama vile video ambazo umetazama kwenye YouTube au mambo uliyotafuta awali ambayo ungependa kuhifadhi na akaunti yako unapotumia huduma za Google. Pia unaweza kutembelea vidhibiti ili kuamua ikiwa shughuli fulani zinahifadhiwa katika kidakuzi au teknolojia sawa kwenye kifaa chako unapotumia huduma zetu ukiwa umeondoka kwenye akaunti yako.
  • Kukagua na kudhibiti aina fulani ya maelezo yaliyowekwa kwenye Akaunti yako ya Google kwa kutumia Dashibodi ya Google.
  • Tazama na ubadilishe mapendeleo yako kuhusu matangazo kutoka Google yanayoonyeshwa kwako kwenye Google na kwenye wavuti, kama vile aina zinazoweza kukuvutia, kwa kutumia Mipangilio ya Matangazo. Hapa, unaweza pia kuamua kujitoa kwenye baadhi ya huduma za matangazo ya Google.
  • Rekebisha jinsi Wasifu unaohusishwa na Akaunti yako ya Google unavyotokea kwa wengine.
  • Dhibiti ni nani unayeshiriki maelezo naye kupitia Akaunti yako ya Google.
  • Ondoa maelezo yanayohusishwa na Akaunti yako ya Google kutoka kwa huduma zetu nyingi.
  • Chagua kama jina la Wasifu wako na picha ya Wasifu itatokea katika mapendekezo kutoka miduara yako ambayo yanatokea katika matangazo.

Unaweza pia kupanga kipitiaji chako kizuie kuki zote, pamoja na kuki zinazohusiana na huduma zetu, au kuonyesha ni wakati gani kuki inapangwa na sisi. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba huduma zetu nyingi zinaweza zisifanye kazi vizuri kama kuki zako zimeondolewa uwezo. Kwa mfano, tunaweza tusikumbuke hiari yako ya lugha.

Maelezo unayoshirikisha

Huduma zetu nyingi zinakuruhusu ushiriki maelezo na watu wengine. Kumbuka kwamba unaposhirikisha maelezo hadharani, yanaweza kufaharisiwa na injini za utafutaji, ikiwemo Google. Huduma zetu hukupa hiari tofauti za kushiriki na kuondoa maudhui yako.

Kufikia na kusasisha maelezo yako binafsi

Wakati wowote unapotumia huduma zetu, tunalenga kukupa ufikiaji wa maelezo yako ya kibinafsi. Kama maelezo hayo sio sahihi, tunajitahidi kukupa njia za kusasisha maelezo hayo haraka au kuyafuta - isipokuwa iwe tunatakikana tuyaweke maelezo hayo kwa ajili halali ya kibiashara au madhumuni ya kisheria. Unaposasisha maelezo ya kibinafsi, tunaweza kukuomba uthibitishe utambulisho wako kabla hatujaweza kushughulikia ombi lako.

Tunaweza kukataa maombi ambayo yanajirudiarudia kupindukia, yanayohitaji juhudi zisizofaa za kiufundi (kwa mfano, kutengeneza mfumo mpya au kubadilisha kimsingi desturi yoyote iliyopo), yanayohatarisha faragha ya wengine, au yasiyofaa kabisa (kwa mfano, maombi yanayohusu maelezo ya mifumo ya hifadhi rudufu).

ambapo tunaweza kutoa maelezo ya utumiaji na usahihishaji , tutafanya hivyo bila malipo, isipokuwa pale itahitaji juhudi kubwa mno. kudumisha huduma zetu kwa njia ambayo inalinda habari kutokana na uharibifu wa maelezo ama kwa bahati mbaya au kwa kukusudia. Kwa sababu hii, baada ya kufuta maelezo kutoka kwenye huduma zetu, huenda tusifute mara moja nakala zilizosalia kutoka kwa seva zetu amilifu na huenda tusitoe maelezo kutoka kwa mifumo yetu yenye nakala saidizi.

Maelezo tunayoshirikisha

Hatushirikishi maelezo ya kibinafsi na kampuni, mashirika, na watu binafsi nje ya Google isipokuwa mojawapo ya hali zifuatazo itokee:

  • Kwa idhini yako

    Tutashirikisha maelezo ya kibinafsi na kampuni, mashirika, na watu wa nje ya Google tukiwa na idhini yako ya kufanya hivyo. Tunahitaji kibali cha uamuzi wa kuingia cha kushirikisha maelezo yoyote nyeti ya kibinafsi.

  • Na wasimamizi wa kikoa

    Kama Akaunti ya Google yako imedhibitiwa na msimamizi wa kikoa(kwa mfano, kwa watumiaji wa Google Apps) basi msimamizi wako wa kikoa chako na wauzaji ambao hutoa usaidizi wa kiufundi kwa watumiaji kwenye shirika lako watafikia maelezo ya akaunti yako ya Google (zikiwemo barua pepe na data zingine). Msimamizi wako wa kikoa anaweza pia:

    • kuona takwimu kuhusu akaunti yako, kama takwimu zinazohusu programu unazosakinisha.
    • kubadilisha nenosiri la akaunti yako.
    • kusitisha au kukomesha ufikiaji wa akaunti yako.
    • kufikia au kuweka maelezo yaliyohifadhiwa kama sehemu ya akaunti yako.
    • kupokea maelezo ya akaunti yako ili kuridhisha sheria inayotumika, kanuni, mchakato wa sheria, au ombi la kulazimishwa kutoka kwa serikali.
    • kuzuia uwezo wako wa kufuta au kuhariri maelezo au kupanga faragha.

    Tafadhali rejelea sera ya faragha ya msimamizi wako wa kikoa kwa maelezo zaidi.

  • Kwa mchakato wa nje

    Tunatoa maelezo ya kibinafsi kwa washirika wetu wadogo au biashara zingine tunazoamini au watu ili kuichakata kwa niaba yetu, kulingana na maagizo yetu na kwa kufuata Sera yetu ya Faragha na hatua zingine zozote zinazofaa za faragha na usalama.

  • Kwa sababu za kisheria

    Tutashirikisha maelezo ya kibinafsi na makampuni, mashirika au watu walioko nje ya Google ikiwa tuna imani kwamba ufikiaji, matumizi, uhifadhi au ufichuzi wa maelezo hayo ni muhimu ili:

    • kutimiza sheria, kanuni, mchakato wa kisheria au ombi lolote la kutekelezeka la kiserikali ambalo linatumika.
    • kutekeleza Masharti husika ya Huduma, ikiwa ni pamoja na uchungzi wa ukiukaji unaowezekana kutokea.
    • kugundua, kuzuia, au kushughulikia ulaghai, masuala ya usalama au kiufundi.
    • kulinda dhidi ya madhara ya haki, mali au usalama wa Google, watumiaji wetu au umma kama inavyotakikana au kuruhusiwa na sheria.

Tunaweza kushiriki hadharani au na washirika wetu – kama vile wachapishaji, watangazaji au tovuti zinazohusiana maelezo yasiyoweza kukutambulisha. Kwa mfano, tunaweza kushiriki maelezo hadharani ili kuonyesha mitindo kuhusu utumiaji wa jumla wa huduma zetu.

Kama Google itahusishwa katika muungano na kampuni zingine, kuchukuliwa au kufilisishwa, tutaendelea kuhakikisha usiri wa habari yoyote ya kibinafsi na kuwapa watumiaji walioathiriwa ilani kabla maelezo ya kibinafsi hayajahamishwa au kuwekwa chini ya sera tofauti ya faragha.

Usalama wa maelezo

Tunafanya bidii kulinda Google na watumiaji wetu dhidi ya ufikiaji ambao haujaidhinishwa au mabadiliko yasiyoidhinishwa, uchakachuaji haramu au uharibifu wa maelezo tuliyoweka. Hasusani

  • Huduma zetu nyingi tunazisimbisha tukitumia SSL.
  • Unapotaka kuingia kwenye Akaunti yako ya Google, tunakuhitaji ujithibitishe mara mbili,na chombo Kipitiaji Salama cha Google Chrome
  • Tunatathmini mkusanyo wetu wa maelezo, uhifadhi na desturi za kuyashughulikia, zikiwemo askari wa usalama kulinda, dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa kwenye mitambo.
  • Tunazuia ufikiaji wa maelezo ya kibinafsi kwa waajiriwa wa Google, wakandarasi na mawakala ambao wanahitaji kujua maelezo hayo ili kuichakata kwa niaba yetu, na ambao wako chini ya majukumu makali ya mkataba ya faragha na wanaweza wakaadhibiwa au kufutwa kazi ikiwa watashindwa kuyatimiza majukumu haya.

Wakati Sera hii ya Faragha hutumika

Sera yetu ya Faragha hutumika kwa huduma zote zinazotolewa na Google Inc. na washirika wake wadogo, ikiwa ni pamoja na YouTube, huduma zinazotolewa na Google kwenye vifaa vya Android na huduma zinazotolewa kwenye tovuti nyingine (kama vile huduma zetu za matangazo), lakini haijumuishi huduma ambazo zina sera tofauti za faragha ambazo hazijumuishi Sera hii ya Faragha.

Sera yetu ya Faragha haitumiki kwenye huduma zinazotolewa na makampuni mengine au watu binafsi, ikiwa ni pamoja na bidhaa au tovuti ambazo zinaweza kuonyeshwa kwako kama matokeo ya utafutaji, tovuti ambazo zinaweza kujumuisha huduma za Google, au tovuti zingine zinazounganishwa kutokana na huduma zetu Sera yetu ya Faragha haishughulikii utumiaji wa maelezo ya makampuni na mashirika mengine ambayo yanatangaza huduma zetu, na ambao wanaweza kutumia kuki, vibandiko vya pikseli na teknolojia zingine ili kuhudumia na kutoa matangazo husika.

Kufuata na kushirikiana na mamlaka ya usimamizi

Tunatathmini mara kwa mara azma yetu ya kutii Sera yetu ya Faragha. Tunafuata pia mifumo kadhaa inayojidhibiti. Wakati tunapopokea malalamiko rasmi kimaandishi, tutawasiliana na mtu aliyetoa malalamiko hayo ili tufuatilie Tunafanya kazi na mamlaka dhibiti husika, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kulinda data za eneo, ili kutatua malalamiko yoyote kuhusiana na uhamishaji wa data za kibinafsi, ambayo hatuwezi kuyatatua na watumiaji wetu moja kwa moja.

Mabadiliko

Sera yetu ya Faragaha inaweza kubadilika mara kwa mara. Hatutapunguza haki zako chini ya Sera ya Faragha hii bila idhini yako dhahiri. Tutachapisha mabadiliko yoyote ya sera ya faragha kwenye ukurasa huu na, kama mabadiliko ni muhimu, tutatoa taarifa inayoonekana zaidi (inayojumuisha, kwa huduma fulani, taarifa ya barua pepe ya mabadiliko ya sera ya faragha). Pia tutaweka toleo za awali za Sera ya Faragha hii katika kumbukumbu kwa tathmini yako.

Desturi maalumu za bidhaa

Taarifa zifuatazo zinaelezea desturi maalumu za faragha kulingana na bidhaa fulani za Google na huduma unazoweza kutumia:

Kwa maelezo zaidi kuhusu baadhi ya huduma zetu maarufu unaweza kutembeleaMwongozo wa Faragha wa Bidhaa za Google.

Nyenzo zaidi muhimu zinazohusika za faragha na usalama zinaweza kupatikana kupitia kurasa za Google za sera na kanuni, ikiwa ni pamoja na:

"ufikiaji kwenye maelezo yako ya kibinafsi"

Kwa mfano, ukiwa na Dashibodi ya Google unaweza kuona kwa haraka na kwa urahisi baadhi ya data iliyohusishwa na Akaunti yako ya Google Pata maelezo zaidi.

"matangazo ambayo utapata ni muhimu zaidi"

Kwa mfano, ikiwa mara kwa mara unatembelea tovuti na blogu kuhusu kilimo cha bustani, unaweza kuona matangazo kuhusu kilimo cha bustani unapovinjari wavuti. Pata maelezo zaidi.

"huduma za utangazaji"

Kwa mfano, ikiwa mara kwa mara unatembelea tovuti na blogu kuhusu kilimo cha bustani ambazo zinaoonyesha matangazo yetu, unaweza kuanza kuona matangazo yanayohusiana na kipendwa hiki unapovinjari wavuti. Pata maelezo zaidi.

"Na vifaa vingine vya kubaini"

Huenda kifaa chako kikawa na vifaa vya kubaini ambavyo hutoa maelezo ili kusaidia kuelewa vyema eneo lako. Kwa mfano, kipima mchapuko kinaweza kutumiwa kubainisha vitu kama kasi, au gurudumu tuzi ili kujua mwelekeo wa usafiri. Pata maelezo zaidi.

"kusanya maelezo"

Hii inajumuisha maelezo kama data yako ya matumizi na mapendeleo, barua za Gmail, wasifu kwenye Google+, picha, video, historia ya kuvinjari, utafutaji ramani, hati, au maudhui mengine yaliowekwa na Google. Pata maelezo zaidi.

"unganisha maelezo ya kibinafsi kutoka kwa huduma moja na maelezo, ikiwa ni pamoja na maelezo ya kibinafsi, kutoka kwa huduma zingine za Google"

Kwa mfano, wakati umeingia katika Akaunti yako ya Google na utafute kwenye Google, unaweza kuona matokeo ya utafutaji kutoka kwenye wavuti ya umma, pamoja na kurasa, picha, na machapisho ya Google+ kutoka kwa marakifi wako na watu wanaokujua au wanaokufuata kwenye Google+ wanaweza kuona machapisho yako na wasifu katika matokeo yao. Pata maelezo zaidi.

"ungana na watu"

Kwa mfano, unaweza kupata mapendekezo ya watu ambao unaweza kujua au unataka kuungana nao kwenye Google+, kulingana na miunganisho uliyo nayo na watu kwenye bidhaa zingine za Google, kama Gmail na watu walio na muunganisho nawe wanaweza kuona wasifu wako kama pendekezo. Pata maelezo zaidi.

"kadi ya mkopo"

Ingawa kwa sasa hatuulizi kadi ya mkopo wakati wa kujisajili, kuthibitisha umri wako kupitia shughuli ndogo ya kadi ya mkopo ni njia moja ya kuthibitisha ya kwamba unatimiza mahitaji yetu ya umri ikiwa akaunti yako ilizimwa baada ya kuingiza tarehe ya kuzaliwa inayoonyesha ya kwamba huna umri wa kutosha kuwa na Akaunti ya Google. Pata maelezo zaidi.

"tengeneza mpya"

Kwa mfano, programu ya Google ya kukagua tahajia ilisanidiwa kwa kuchanganua utafutaji wa awali ambapo watumiaji walikuwa wamesahihisha tahajia yao wenyewe. Pata maelezo zaidi.

"vitambua vifaa"

Vitambulishi vya kifaa hujulisha Google ni kifaa kipi cha kipekee unachotumia kufikia huduma zetu, hii inaweza kutumika kubinafsisha huduma yetu kwa kifaa chako au kuchanganua tatizo zozote za kifaa zinazohusiana na huduma zetu. Pata maelezo zaidi.

"maelezo maalum ya kifaa"

Kwa mfano, unapotembelea Google Play kutoka kwa eneo-kazi lako, Google inaweza kutumia maelezo haya kukusaidia kuamua ni vifaa vipi ungependa ununuzi wako kupatikana kwa matumizi. Pata maelezo zaidi.

"boresha matumizi yako"

Kwa mfano,vidakuzi vinaturuhusu kuchanganua jinsi watumiaji wanavyowasiliana na huduma zetu. Pata maelezo zaidi.

Kama makampuni mengine ya teknolojia na mawasiliano, mara kwa mara Google hupokea maombi kutoka kwa serikali na mahakama duniani kote ya kutoa data ya mtumiaji. Timu yetu ya sheria hukagua kila ombi, bila kubagua aina, na mara nyingi sisi hukataa maombi yanayoonekana kuwa mapana sana au yasiyofuatilia utaratibu sahihi. Pata maelezo zaidi.

"zuia mipangilio ya kushiriki au mwonekano"

Kwa mfano, unaweza kuchagua mipangilio yako ili jina na picha yako zisionekane katika tangazo. Pata maelezo zaidi.

"imeunganishwa na maelezo kuhusu matembeleo ya tovuti mbalimbali"

Uchanganuzi wa Google unategemea vidakuzi vya mhusika wa kwanza. Data inayozalishwa kupitia Uchanganuzi wa Google inaweza kuunganishwa, na mteja wa Uchanganuzi wa Google au na Google, kwa kutumia teknolojia ya Google, kwa vidakuzi vya wahusika wengine, vinavyohusiana na matembeleo ya tovuti zingine, kwa mfano wakati mtangazaji anapotaka kutumia data yake ya Uchanganuzi wa Google kuunda matangazo yanayofaa zaidi, au kuchanganua trafiki yake zaidi. Pata maelezo zaidi.

"kudumisha"

Kwa mfano, sisi huendelea kufuatilia mifumo yetu ili kukagua kuwa inafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kugundua na kutatua matatizo. Pata maelezo zaidi.

"huenda ikakusanya na kuchakata maelezo kuhusu eneo lako halisi"

Kwa mfano, Ramani za Google zinaweza kuweka mwonekano wa ramani wa eneo lako la sasa. Pata maelezo zaidi.

"inaweza kosa kufanya kazi vizuri"

Kwa mfano, tunatumia kidakuzi kinachoitwa 'Ibcs' ambacho kinafanya iwezekane kwako kufungua Hati nyingi za Google katika kivinjari kimoja. Pata maelezo zaidi.

"na washirika wetu"

Tunaruhusu wanabiashara wanaoaminika kutumia vidakuzi au teknolojia kama hizo kwa malengo ya utangazaji na utafiti kwenye huduma zetu. Pata maelezo zaidi.

"nambari ya simu"

Kwa mfano, ukiongeza nambari ya simu kama chaguo la urejeshi, ukisahau nenosiri lako Google inaweza kukutumia SMS iliyo na msimbo ili kukuwezesha kuliweka upya. Pata maelezo zaidi.

"linda Google na watumiaji wetu"

Kwa mfano, ikiwa una wasiwasi kuhusu ufikiaji ambao hujaidhinishwa kwa barua pepe yako, "Shughuli ya mwisho ya akaunti" katika Gmail inakuonyesha habari kuhusu shughuli ya hivi karibuni katika barua pepe yako, kama vile anwani za IP ambazo zilifikia barua pepe yako, eneo linalohusiana, pamoja na wakati na tarehe. Pata maelezo zaidi.

"kulinda"

Kwa mfano, sababu moja sisi hukusanya na kutathmini anwani za IP na vidakuzi ni kulinda huduma zetu dhidi ya matumizi mabaya otomati. Pata maelezo zaidi.

"kutoa"

Kwa mfano, anwani ya IP iliyohawilishwa kwa kifaa chako hutumiwa kurejesha tena data uliyoomba kwenye kifaa chako. Pata maelezo zaidi.

"kushiriki"

Kwa mfano, kwenye Google+, una chaguo mbalimbali za kushiriki. Pata maelezo zaidi.

"Kushiriki na wengine kwa haraka na kwa urahisi"

Kwa mfano, ikiwa tayari unawasiliana na mtu, Google itakamilisha jina lake ikiwa unataka kumwongeza kwenye barua katika Gmail. Pata maelezo zaidi.

"Watu ambao ni muhimu kwako zaidi mtandaoni"

Kwa mfano, unapocharaza anwani katika sehemu ya Kwa, Cc, au Bcc ya ujumbe unaotunga, Gmail itapendekeza anwani kutoka kwa orodha yako ya Unaowasiliana nao. Pata maelezo zaidi.

"Ili kuifanya iwe rahisi kushiriki mambo na watu unaowajua"

Kwa mfano, ikiwa umewasiliana na mtu kupitia Gmail na unataka kumwongeza kwenye Hati za Google au tukio katika Google Kalenda. Google inaifanya iwe rahisi kufanya hivyo kwa kukamilisha anwani yake ya barua pepe kiotomatiki unapoanza kuandika jina lake. Pata maelezo zaidi.

"tazama na uwasiliane na matangazo yetu"

Kwa mfano, mara kwa mara tunaripoti kwa watangazaji ikiwa tulitoa tangazo lao kwenye ukurasa na ikiwa tangazo hilo lilikuwa na uwezekano wa kuonekana na watumiaji (kinyume na, kwa mfano, kuwa kwenye sehemu ya ukurasa ambayo watumiaji hawakuvinjari). Pata maelezo zaidi.

"Tunaweza kushiriki hadharani maelezo ya jumla, yasioweza kukutambulisha"

Wakati watu wengi wanaanza kutafuta kitu, inaweza kutoa maelezo muhimu kuhusu mitindo maalum wakati huo. Pata maelezo zaidi.

"Maeneo ya kufikia Wi-Fi na minara ya mitandao"

Kwa mfano, Google inaweza kukadiria mahali pa kifaa chako kulingana na mahali panapojulikana pa minara ya mitandao iliyo karibu. Pata maelezo zaidi.

"matokeo muhimu zaidi ya utafutaji"

Kwa mfano, tunaweza kufanya utafutaji kufaa na kupendeza zaidi kwako kwa kujumuisha picha, machapisho na zaidi kutoka kwako na marafiki wako. Pata maelezo zaidi.

"kuondoa maudhui yako"

Kwa mfano, unaweza kufuta Shughuli zako za Programu na Wavuti, blogu yako, Tovuti ya Google unayomiliki, Kituo chako cha YouTube, wasifu wako kwenye Google+ au akaunti yako yote ya Google. Pata maelezo zaidi.

Unaweza kuona baadhi ya hizi katika Google Trends na YouTube Trends. Pata maelezo zaidi.

"shughuli zako kwenye tovuti na programu nyingine"

Shughuli hizi huenda zitokane na matumizi yako ya bidhaa za Google kama vile Usawazishaji wa Chrome au tovuti na programu unazotembelea zinazoshirikiana na Google. Tovuti na programu nyingi hushirikiana na Google kuboresha maudhui na huduma zao. Kwa mfano, tovuti inaweza kutumia huduma zetu za matangazo (kama vile AdSense) au zana za uchanganuzi (kama vile Google Analytics). Bidhaa hizi hushiriki maelezo kuhusu shughuli zako na Google na, kulingana na mipangilio ya akaunti yako na bidhaa unazotumia (kwa mfano, mshirika anapotumia Google Analytics pamoja na huduma zetu za matangazo), data hii huenda ikahusishwa na maelezo yako ya kibinafsi. Pata maelezo zaidi.

Programu za Google
Menyu kuu