Ripoti ya Uwazi Kuhusu Kufikia na Kufuta Data

Jinsi ilivyobainishwa katika Sera ya Faragha ya Google na Kituo cha Usaidizi wa Masuala ya Faragha, tuna zana mbalimbali zinazowasaidia watumiaji kusasisha, kudhibiti, kufikia, kusahihisha, kuhamisha na kufuta taarifa zao na kudhibiti faragha yao kwenye huduma za Google. Hasa, kila mwaka mamilioni ya watumiaji nchini Marekani hutumia kipengele cha Google cha Pakua data yako au hufuta baadhi ya data yao kwa kutumia kipengele cha Google cha Shughuli Zangu. Zana hizi huwawezesha watumiaji kuchagua aina mahususi za data kwenye huduma za Google ambazo wangependa kukagua, kupakua, au kufuta na maombi hayo huchakatwa kiotomatiki. Isitoshe, watumiaji wanaweza kutumia haki zao chini ya sheria mahususi za faragha kama vile Sheria ya California ya Ulinzi wa Faragha ya Watumiaji (“CCPA”) kwa kuwasiliana na Google.

Jedwali lililo hapa chini linatoa maelezo zaidi kuhusu matumizi ya zana hizi na mbinu za kuwasiliana mwaka wa 2023:

Aina ya ombiIdadi ya maombiMaombi yaliyokamilishwa kikamilifu au kwa kiasi fulaniMaombi yaliyokataliwa***Wastani wa muda wa kujibu kwa njia inayotosheleza
Matumizi ya Pakua data yako*Takribani milioni 8.8Takribani milioni 8.8Hamna (maombi yalichakatwa kiotomatiki)Chini ya siku 1 (maombi yalichakatwa kiotomatiki)
Matumizi ya Kufuta Shughuli Zangu*Takribani milioni 60.6Takribani milioni 60.6Hamna (maombi yalichakatwa kiotomatiki)Chini ya siku 1 (maombi yalichakatwa kiotomatiki)
Maombi ya kufahamu (kwa kuwasiliana na Google)**4244222Siku 6
Maombi ya kufuta (kwa kuwasiliana na Google)**32320Siku 7
Maombi ya kusahihisha (kwa kuwasiliana na Google)**000Hamna

Jinsi ilivyobainishwa kwenye Sera yetu ya Faragha, Google haiuzi taarifa binafsi za watumiaji wetu na hutumia taarifa binafsi ambazo CCPA inachukulia kuwa nyeti kwa madhumuni yaliyoruhusiwa na CCPA pekee. Vile vile, watumiaji wanapotuma maombi ya kujiondoa kwenye mpango wa kuuza taarifa binafsi au kudhibiti matumizi ya taarifa zao nyeti za binafsi, tunajibu maombi haya kwa kufafanua desturi na wajibu wetu. Pia tunawapa watumiaji maelezo kuhusu hali chache ambapo taarifa zao binafsi zinaweza kutumwa nje ya Google, udhibiti walio nao kuhusiana na utumaji wa taarifa husika na udhibiti wa ziada kuhusu kukusanya na kutumia taarifa nyeti, unaoweza kupatikana kulingana na huduma ya Google wanayotumia.

* Data ya watumiaji wanaoishi Marekani

** Data ya watumiaji wanaojitambulisha kuwa wakazi wa California

*** Kila ombi lililokataliwa mwaka wa 2023 lilikataliwa kwa sababu ombi halikuweza kuthibitishwa au mtumiaji aliondoa ombi husika

Programu za Google
Menyu kuu