Ripoti ya Uwazi Kuhusu Kufikia na Kufuta Data

Jinsi ilivyobainishwa katika Sera ya Faragha ya Google na Kituo cha Usaidizi kuhusu Faragha, tuna zana mbalimbali zinazowasaidia watumiaji kusasisha, kudhibiti, kufikia, kutuma na kufuta taarifa zao; na kudhibiti faragha yao kwenye huduma za Google. Hasa, kila mwaka mamilioni ya watumiaji nchini Marekani hutumia kipengele cha Google cha Pakua data yako au hufuta baadhi ya data yao kwa kutumia kipengele cha Google cha Shughuli Zangu. Zana hizi huwawezesha watumiaji kuchagua aina mahususi za data kwenye huduma za Google ambazo wangependa kukagua, kupakua, au kufuta na maombi hayo huchakatwa kiotomatiki. Isitoshe, watumiaji wanaweza kutumia haki zao chini ya sheria mahususi za faragha kama vile Sheria ya California ya Ulinzi wa Faragha ya Watumiaji kwa kuwasiliana na Google.

Jedwali lililo hapa chini linatoa maelezo zaidi kuhusu matumizi ya zana hizi na mbinu za kuwasiliana mwaka wa 2021:

Aina ya ombiIdadi ya maombiMaombi yaliyokamilishwa kikamilifu au kwa kiasi fulaniMaombi yaliyokataliwa***Wastani wa muda wa kujibu kwa njia inayotosheleza
Matumizi ya Pakua data yako*Takribani milioni 3.9Takribani milioni 3.9Hamna (maombi yalichakatwa kiotomatiki)Chini ya siku 1 (maombi yalichakatwa kiotomatiki)
Matumizi ya Kufuta Shughuli Zangu*Takribani milioni 18.9Takribani milioni 18.9Hamna (maombi yalichakatwa kiotomatiki)Chini ya siku 1 (maombi yalichakatwa kiotomatiki)
Maombi ya kufahamu (kwa kuwasiliana na Google)**6836794Siku 15
Maombi ya kufuta (kwa kuwasiliana na Google)**62620Siku 15

Jinsi ilivyobainishwa katika Sera yetu ya Faragha, Google haiuzi taarifa binafsi za watumiaji wetu. Vile vile, wakati watumiaji wanatuma maombi ya kujiondoa kwenye mpango wa uuzaji wa taarifa binafsi, tunajibu maombi hayo kwa kufafanua juhudi na wajibu wetu na kuwapa maelezo kuhusu hali chache ambapo taarifa zao binafsi zinaweza kushirikiwa nje ya Google na udhibiti walio nao katika mchakato huo wa kushiriki.

* Data ya watumiaji wanaoishi Marekani

** Data ya watumiaji wanaojitambulisha kuwa wakazi wa California

*** Kila ombi lililokataliwa mwaka wa 2021 lilikataliwa kwa kuwa halikuweza kuthibitishwa

Programu za Google
Menyu kuu