Mifumo ya kisheria ya kuhamisha data

Inatumika kuanzia 10 Februari 2022

Tuna seva duniani kote na maelezo yako yanaweza kuchakatwa kwenye seva zilizo nje ya nchi unakoishi. Sheria za ulinzi wa data ni tofauti katika kila nchi. Kuna nchi ambazo hutoa ulinzi zaidi kuliko nyingine. Maelezo yako yatashughulikiwa popote kwa kuzingatia sheria za ulinzi wa data kama ilivyofafanuliwa kwenye Sera ya Faragha. Pia, tunazingatia mifumo fulani ya kisheria ya kuhamisha data, kama vile mifumo iliyofafanuliwa hapa chini.

Uamuzi kuhusu ulinzi wa data

Tume ya Ulaya imebaini kuwa baadhi ya nchi zilizo washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA) zinatoa ulinzi wa kutosha wa data binafsi, hali inayomaanisha kuwa data inaweza kuhamishwa kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na Norwe, Lishensteni na Aisilandi kwenda nchi hiyo isiyoshiriki bila ulinzi wowote wa ziada kuhitajika. Uingereza na Uswisi zimeidhinisha uamuzi sawa kuhusu ulinzi wa data. Tunategemea uamuzi ufuatao kuhusu ulinzi wa data katika hali fulani:

Vipengele wastani vya mkataba

Vipengele wastani vya mkataba (SCC) ni makubaliano yaliyoandikwa kati ya washirika ambao wanaweza kutumiwa kama msingi wa uhamishaji wa data kutoka Umoja wa Ulaya kwenda nchi za nje kwa kutoa ulinzi unaofaa wa data. Vipengele wastani vya mkataba (SCC) vimeidhinishwa na Tume ya Ulaya na haviwezi kurekebishwa na washirika wanaovitumia (unaweza kuona Vipengele wastani vya mkataba (SCC) vinavyotumiwa na Tume ya Ulaya hapa, hapa na hapa). Vipengele kama hivyo pia vimeidhinishwa kwa ajili ya uhamishaji wa data kwenda nchi zilizo nje ya Uingereza na Uswisi. Tunategemea Vipengele Wastani vya Mkataba (SCC) kwa ajili ya uhamishaji wa data panapohitajika. Iwapo ungependa kupata nakala ya Vipengele Wastani vya Mkataba (SCC), unaweza kuwasiliana nasi.

Google pia inajumuisha Vipengele Wastani vya Mkataba (SCC) katika mikataba na wateja wa huduma za biashara zake, ikiwa ni pamoja na Google Workspace, Mfumo wa Wingu la Google, Google Ads na bidhaa nyingine za upimaji na matangazo. Pata maelezo zaidi katika privacy.google.com/businesses.

EU-U.S. na Swiss-U.S. Privacy Shield Frameworks

Kama ilivyoelezewa katika Uthibitisho wetu wa Privacy Shield (Mfumo wa Faragha), tunazingatia EU-U.S. na Swiss-U.S. Privacy Shield Frameworks kama ilivyobainishwa na Idara ya Biashara ya Marekani kuhusu ukusanyaji, utumiaji na uhifadhi wa taarifa binafsi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (ikiwa ni pamoja na nchi washirika wa EEA) na Uingereza na Uswizi mtawalia. Google, pamoja na Google LLC na kampuni zake tanzu zilizo Marekani (isipokuwa zile zilizotengwa kwa njia dhahiri), imethibitisha kuwa inatii Kanuni za Privacy Shield. Bado Google inawajibikia taarifa zako binafsi zinazoshirikiwa chini ya Kanuni ya Uhamishaji na washirika wengine kwa ajili ya uchakataji wa nje kwa niaba yetu, kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya “Kushiriki taarifa zako”. Ili upate maelezo zaidi kuhusu mpango wa Privacy Shield (Mfumo wa Faragha) na uangalie uthibitisho wa Google, tafadhali tembelea tovuti ya Privacy Shield (Mfumo wa Faragha).

Ikiwa una swali lolote kuhusu desturi zetu za faragha zinazohusiana na uthibitisho wetu wa Ngao ya Faragha (Privacy Shield), tunakuhimiza uwasiliane nasi. Google inategemea mamlaka ya uchunguzi na utekelezaji ya Tume ya Biashara ya Marekani (FTC). Pia unaweza kutuma malalamiko kwenye mamlaka inayolinda data ya eneo lako na tutashirikiana nayo kutatua tatizo lako. Katika hali fulani, Mfumo wa Ngao ya Faragha (Privacy Shield Framework) unatoa haki ya kutekeleza upatanishi wa kushurutishwa ili kusuluhisha malalamiko ambayo hayajasuluhishwa kwa njia nyingine, kama inavyoelezewa katika Kiambatisho cha I kwenye Kanuni za Ngao ya Faragha (Privacy Shield Principles) .

Kuanzia tarehe 16 Julai 2020, hatutegemei tena EU-U.S. Privacy Shield (Mfumo wa Faragha wa Ulaya-Marekani) ili kuhamisha data inayotoka EEA au Uingereza kwenda Marekani.

Programu za Google
Menyu kuu