Washirika wa Google ni nani?

Google hushirikiana na mashirika na biashara kwa njia mbalimbali. Sisi hurejelea biashara na mashirika haya kama "washirika". Kwa mfano, tovuti na programu zaidi ya milioni 2 zisizo za Google hushirikiana na Google kuonyesha matangazo. Mamilioni ya washirika wasanidi programu huchapisha programu zao kwenye Google Play. Washirika wengine husaidia Google kwa kuimarisha usalama wa huduma zetu; maelezo kuhusu vitisho vya usalama yanaweza kutusaidia kukujulisha ikiwa tunahofia kuwa akaunti yako imeathiriwa (ambapo tunaweza kukusaidia kuchukua hatua za kulinda akaunti yako).

Kumbuka kuwa sisi pia hushirikiana na biashara zinazoaminika ili zifanye kazi kama "wachakataji wa data" badala ya washirika, kumaanisha kuwa wanachakata maelezo kwa niaba yetu, kusaidia utoaji huduma zetu, kulingana na maagizo yetu na kwa kutii Sera yetu ya Faragha na hatua nyinginezo za siri na usalama. Sera ya Faragha ya Google ina maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia wachakataji wa data.

Hatuwapi washirika wetu wa matangazo maelezo ambayo yanakutambua binafsi, kama vile jina lako au anwani ya barua pepe, isipokuwa ukituomba tufanye hivyo. Kwa mfano, ukiona tangazo la duka la maua lililo karibu nawe kisha uchague kitufe cha "gusa ili upige simu", tutaunganisha simu yako na tunaweza kushiriki nambari yako ya simu na duka hilo la maua.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu maelezo ambayo Google hukusanya, ikijumuisha kutoka kwa washirika, katika Sera ya Faragha.

Programu za Google
Menyu kuu