Masharti muhimu
- Akaunti ya Google
- Algoriti
- Anwani ya IP
- Hifadhi ya kivinjari cha wavuti
- Hifadhi ya ndani ya data ya programu
- Kifaa
- Kumbukumbu za seva
- Lebo ya Pixeli
- Maelezo nyeti ya kibinafsi
- Maelezo ya kibinafsi
- Maelezo yasiyotambulisha kibinafsi
- URL Iliyoelekeza
- Vidakuzi
- Vitambulishaji vya kipekee
- Washirika
Akaunti ya Google
Unaweza kufikia baadhi ya huduma zetu kwa kufungua Akaunti ya Google na kutoa baadhi ya maelezo yako ya binafsi (kwa kawaida jina lako, anwani ya barua pepe na nenosiri). Maelezo haya ya akaunti hutumiwa kukuthibitisha unapofikia huduma za Google na kulinda akaunti yako isifikiwe na watu ambao hujawaidhinisha. Unaweza kubadilisha maelezo kwenye akaunti au kuifunga wakati wowote kupitia mipangilio ya Akaunti yako ya Google.
Algoriti
Mchakato au taratibu zinazofuatwa na kompyuta kutatua matatizo.
Anwani ya IP
Kila kifaa kinachounganishwa kwenye Intaneti kimepangiwa namba inayojulikana kama anwani ya Itifaki ya Wavuti (IP). Kwa kawaida namba hizi hupangwa katika vikundi vya kijiografia. Mara nyingi anwani ya IP inaweza kutumiwa kutambua mahali ambako kifaa kinatumiwa kuunganisha kwenye Intaneti. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia maelezo ya mahali.
Hifadhi ya kivinjari cha wavuti
Hifadhi ya kivinjari huwezesha tovuti kuhifadhi data katika kivinjari kwenye kifaa. Unapoitumia katika hali ya "hifadhi ya ndani", inakuwezesha kuhifadhi data katika vipindi vyote. Hii inakuwezesha kupata data hata baada ya kufunga na kufungua upya kivinjari. Teknolojia moja ambayo inawezesha kuhifadhi kwenye wavuti ni HTML 5.
Hifadhi ya ndani ya data ya programu
Hifadhi ya ndani ya data ya programu ni hifadhi ya data kwenye kifaa. Inaweza, kwa mfano, kuwezesha programu ya wavuti kuendeshwa bila muunganisho wa intaneti na kuboresha utendaji wa programu kwa kuwezesha upakiaji wa haraka wa maudhui.
Kifaa
Kifaa ni kompyuta ambayo inaweza kutumika ili kufikia huduma za Google. Kwa mfano, kompyuta za mezani, kompyuta kibao, spika mahiri na simu mahiri, zote zinachukuliwa kuwa vifaa.
Kumbukumbu za seva
Kama tovuti mingi, seva zetu hurekodi maombi ya ukurasa yanayofanywa unapotembelea tovuti zetu kiotomatiki. “Kumbukumbu za seva” kwa kawaida hujumuisha ombi lako la wavuti, anwani ya IP, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na wakati wa ombi lako na moja au zaidi ya vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari chako kipekee.
Huu ni mfano wa kumbukumbu ambapo utafutaji ni wa “magari”:
123.45.67.89 - 25/Mar/2003 10:15:32 -
http://www.google.com/search?q=cars -
Chrome 112; OS X 10.15.7 -
740674ce2123e969
123.45.67.89
ni anwani ya IP inayotolewa kwa mtumiaji na mtoa huduma za intaneti. Kulingana na huduma ya mtumiaji, anwani tofauti inaweza kutolewa kwa mtumiaji na mtoa huduma wake kila wakati anapounganisha kwenye Intaneti.25/Mar/2003 10:15:32
ndiyo tarehe na saa ya hoja.http://www.google.com/search?q=cars
ndiyo URL iliyoombwa, ikiwemo hoja ya utafutaji.Chrome 112; OS X 10.15.7
ndicho kivinjari na mfumo wa uendeshaji unaotumika.740674ce2123a969
ndicho kitambulisho cha kipekee cha kidakuzi kilichotolewa kwa kompyuta hii mara ya kwanza ilipotumika kutembelea Google. (Vidakuzi vinaweza kufutwa na watumiaji. Ikiwa mtumiaji amefuta kidakuzi kwenye kompyuta kutoka wakati wa mwisho alipotembelea Google, kitambulisho cha kipekee cha kidakuzi kitatolewa kwa mtumiaji atakapotembelea Google tena akitumia kompyuta hiyo).
Lebo ya Pixeli
Lebo ya pikseli ni aina ya teknolojia inayowekwa kwenye tovuti au katika kiini cha barua pepe kwa lengo la kufuatilia shughuli fulani kwenye tovuti, kama vile tovuti inapotembelewa au barua pepe zinapofunguliwa. Lebo za pikseli kwa kawaida hutumiwa pamoja na vidakuzi.
Maelezo nyeti ya kibinafsi
Hii ni aina mahususi ya maelezo ya binafsi yanayohusiana na maelezo ya siri ya afya, asili ya mbari au kabila, imani za kisiasa au dini au mwelekeo wa jinsia.
Maelezo ya kibinafsi
Haya ni maelezo ambayo unatupa yanayokutambulisha binafsi, kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, au maelezo ya malipo, au data nyingine ambayo inaweza kuhusishwa kwa kawaida na maelezo kama hayo na Google, kama vile maelezo tunayohusisha na Akaunti yako ya Google.
Maelezo yasiyotambulisha kibinafsi
Haya ni maelezo yanayorekodiwa kuhusu watumiaji ili yasionyeshe wala kurejelea tena mtumiaji binafsi anayetambulika.
URL Iliyoelekeza
URL Iliyoelekeza (Uniform Resource Locator) ni maelezo yanayowasilishwa na kivinjari kwenye ukurasa lengwa wa wavuti, kwa kawaida unapobofya kiungo cha ukurasa huo. URL Iliyoelekeza ina URL ya ukurasa wa mwisho wa wavuti uliovinjari.
Vidakuzi
Kidakuzi ni faili ndogo iliyo na msururu wa herufi inayotumwa kwenye kompyuta yako unapotembelea tovuti fulani. Unapotembelea tovuti tena, kidakuzi kinaruhusu tovuti hiyo kutambua kivinjari chako. Vidakuzi vinaweza kuhifadhi mapendeleo ya mtumiaji na maelezo mengine. Unaweza kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili kisitumie vidakuzi au kikuarifu kidakuzi kinapotumwa. Hata hivyo, vipengee vingine vya tovuti au huduma huenda visifanye kazi vizuri bila vidakuzi. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia vidakuzi na data, vikiwemo vidakuzi, unapotumia tovuti au programu za washirika wetu.
Vitambulishaji vya kipekee
Kitambulishaji cha kipekee ni mfuatano wa herufi ambao unaweza kutumika kutambua kivinjari, programu au kifaa maalum. Vitambulishaji tofauti hutofautiana kulingana na muda vinaodumu, ikiwa vinaweza kubadilishwa na mtumiaji na jinsi vinavyoweza kufikiwa.
Vitambulishaji vya kipekee vinaweza kutumika kwa madhumuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na usalama na ugunduaji ulaghai, kusawazisha huduma kama vile barua pepe zako, kukumbuka mapendeleo yako na kukuonyesha matangazo yanayokufaa. Kwa mfano, vitambulishaji vya kipekee vilivyohifadhiwa kwenye vidakuzi vinasaidia tovuti unayovinjari kuonyesha maudhui katika lugha unayopendelea. Unaweza kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili kisitumie vidakuzi au kikuarifu kidakuzi kinapotumwa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia vidakuzi.
Kwenye mifumo mingine kando na vivinjari, vitambulishaji vya kipekee hutumika kutambua kifaa au programu maalum kwenye kifaa hicho. Kwa mfano, kitambulishaji cha kipekee kama vile Kitambulisho cha kifaa kwa ajili ya Matangazo hutumika kutoa matangazo yanayofaa kwenye vifaa vya Android na kinaweza kudhibitiwa kwenye mipangilio ya kifaa chako. Vitambulishaji vya kipekee vinaweza pia kujumuishwa kwenye kifaa na mtengenezaji (wakati mwingine huitwa kitambulisho cha kipekee ulimwenguni au UUID), kama vile nambari ya IMEI ya simu ya mkononi. Kwa mfano, kitambulisho cha kipekee cha kifaa kinaweza kutumika kukupa huduma zinazokufaa au kukagua matatizo ya kifaa yanayohusiana na huduma zetu.
Washirika
Mshirika ni kampuni ambayo ipo kwenye kundi la kampuni za Google, zikiwemo kampuni zifuatazo zinazotoa huduma za watumiaji katika Umoja wa Ulaya: Google Ireland Limited, Google Commerce Ltd, Google Payment Corp na Google Dialer Inc. Pata maelezo zaidi kuhusu kampuni zinazotoa huduma za biashara katika Umoja wa Ulaya.