Sera ya Faragha ya Google

Unapotumia huduma zetu, unaamini kuwa tutalinda maelezo yako. Tunaelewa kuwa hili ni jukumu kubwa na tunafanya tuwezalo ili kulinda maelezo yako na kuhakikisha kuwa unaweza kuyadhibiti.

Sera hii ya Faragha imekusudiwa kukusaidia uelewe maelezo tunayokusanya, sababu za kuyakusanya na jinsi unavyoweza kusasisha, kudhibiti, kuhamisha na kufuta maelezo yako.

Ukaguzi wa Faragha

Ungependa kubadilisha mipangilio yako ya faragha?

Fanya Ukaguzi wa Faragha

Inatumika kuanzia 28 Machi 2024 | Matoleo yaliyowekwa kwenye kumbukumbu | Pakua PDF

Tunaunda huduma mbalimbali zinazosaidia mamilioni ya watu kuwasiliana na kufahamu yanayotukia ulimwenguni kote kila siku kwa njia mpya. Huduma zetu zinajumuisha:

  • Programu, tovuti na vifaa vya Google kama vile Tafuta na Google, YouTube na Google Home
  • Mifumo kama vile kivinjari cha Chrome na mfumo wa uendeshaji wa Android
  • Bidhaa ambazo zinatumiwa na tovuti na programu za wengine, kama vile Google Ads, Google Analytics na Ramani za Google zilizopachikwa

Unaweza kutumia huduma zetu kwa njia mbalimbali ili kudhibiti faragha yako. Kwa mfano, unaweza kufungua Akaunti ya Google ikiwa ungependa kuunda na kudhibiti maudhui kama vile barua pepe na picha, au kuona matokeo ya utafutaji yanayokufaa zaidi. Unaweza pia kutumia huduma nyingi za Google ukiwa umeondoka kwenye akaunti au hata bila kufungua akaunti, kama vile kutafuta kwenye Google au kutazama video za YouTube. Unaweza pia kuchagua kuvinjari wavuti katika hali ya faragha, kama vile Hali fiche kwenye Chrome, ambayo inasaidia kufanya shughuli zako za kuvinjari zisionekana kwa watu wengine wanaotumia kifaa chako. Kwenye huduma zetu, unaweza kurekebisha mipangilio yako ya faragha ili udhibiti ikiwa tukusanye aina fulani ya data na tunavyoitumia.

Ili tuweze kufafanua mambo wazi kabisa, tumejumuisha mifano, video zenye maelezo na ufafanuzi wa masharti muhimu. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Sera hii ya Faragha, wasiliana nasi.

Maelezo ambayo Google hukusanya

Tungependa ujue maelezo tunayokusanya unapotumia huduma zetu

Sisi hukusanya maelezo ili kutoa huduma bora kwa watumiaji wetu wote — kutoka kubashiri vitu vya msingi kama vile lugha unayozungumza, hadi vitu changamani zaidi kama vile matangazo yanayokufaa, watu muhimu sana kwako mtandaoni, au video ambazo huenda utapenda kwenye YouTube. Maelezo yanayokusanywa na Google na jinsi yanavyotumika inategemea unavyotumia huduma zetu na unavyodhibiti vidhibiti vyako vya faragha.

Ikiwa hujaingia katika Akaunti ya Google, tunahifadhi maelezo tunayokusanya kupitia vitambulishi vya kipekee vilivyojumuishwa kwenye kivinjari, programu au kifaa unachotumia. Hali hii inaturuhusu tufanye mambo kama vile kudumisha mapendeleo yako katika vipindi vyote vya kuvinjari, kama vile lugha unayopendelea au iwapo tutakuonyesha matokeo ya utafutaji au matangazo yatakayokufaa zaidi kulingana na shughuli zako.

Ukiwa umeingia katika akaunti, sisi hukusanya pia maelezo tunayohifadhi kwenye Akaunti yako ya Google na tunayachukulia kuwa maelezo ya binafsi.

Maudhui unayounda au kutupa

Unapofungua Akaunti ya Google, unatupa taarifa binafsi zinazojumuisha jina na nenosiri lako. Unaweza pia kuchagua kuweka nambari ya simu au maelezo ya malipo kwenye akaunti yako. Hata kama hujaingia katika Akaunti ya Google, unaweza kuchagua kutupa maelezo — kama vile anwani ya barua pepe ili kuwasiliana na Google au kupokea taarifa kuhusu huduma zetu.

Sisi pia hukusanya maudhui unayounda, unayopakia, au kupokea kutoka kwa watu wengine unapotumia huduma zetu. Hii inajumuisha vipengee kama vile barua pepe unazotuma na kupokea, picha na video unazohifadhi, hati na malahajedwali unayounda na maoni unayotoa kwenye video za YouTube.

Maelezo tunayokusanya unapotumia huduma zetu

Programu, vivinjari na vifaa vyako

Google hukusanya maelezo kuhusu programu, vivinjari na vifaa unavyotumia kufikia huduma zake. Hii hutusaidia kutoa vipengele kama vile masasisho ya kiotomatiki ya bidhaa na kipengele cha kupunguza ung'avu wa skrini ikiwa betri yako inakaribia kuisha chaji.

Maelezo tunayokusanya ni pamoja na vitambulishaji vya kipekee, aina na mipangilio ya kivinjari, aina na mipangilio ya vifaa, mfumo wa uendeshaji, maelezo ya mtandao wa simu ikiwa ni pamoja na jina la mtoa huduma na nambari ya simu na nambari ya toleo la programu. Sisi hukusanya pia maelezo kuhusu mawasiliano kati ya programu, vivinjari na vifaa vyako na huduma zetu, ikiwemo Anwani ya IP, ripoti za kuacha kufanya kazi, shughuli za mfumo na tarehe, saa na URL ya kuelekeza ya ombi lako.

Tunakusanya maelezo haya wakati huduma ya Google kwenye kifaa chako inawasiliana na seva zetu — kwa mfano, unaposakinisha programu kutoka kwenye Duka la Google Play au wakati huduma inatafuta masasisho ya kiotomatiki. Ikiwa unatumia Kifaa cha Android chenye programu za Google, kifaa chako huwasiliana na seva za Google mara kwa mara ili kutoa maelezo kuhusu kifaa chako na muunganisho kwenye huduma zetu. Maelezo haya yanajumuisha mambo kama vile aina ya kifaa na jina la mtoa huduma, ripoti za matukio ya kuacha kufanya kazi, programu ambazo umesakinisha na kulingana na mipangilio ya kifaa chako, maelezo mengine kuhusu jinsi unavyotumia kifaa chako cha Android.

Shughuli zako

Sisi hukusanya maelezo ya shughuli zako kwenye huduma zetu. Maelezo haya hutumika kutekeleza mambo kama vile kukupendekezea video ambazo huenda ukapenda kwenye YouTube. Maelezo ya shughuli tunayokusanya yanajumuisha:

Ukitumia huduma zetu kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe, tunaweza kukusanya maelezo ya kumbukumbu ya simu na ujumbe kama vile nambari ya simu, nambari ya anayekupigia, nambari ya unayempigia, nambari za kusambaza simu, anwani ya barua pepe ya anayetuma na anayepokea, saa na tarehe za simu na ujumbe, muda wa kuongea kwenye simu, maelezo ya kuelekezwa kwa simu na aina na idadi ya simu na ujumbe.

Unaweza kutembelea Akaunti ya Google ili upate na kudhibiti maelezo ya shughuli ambayo yamehifadhiwa katika akaunti yako.

Maelezo mahali ulipo

Tunakusanya maelezo ya mahali unapotumia huduma zetu, hali inayotusaidia kutoa vipengele kama vile maelekezo ya safari kwa gari, matokeo ya utafutaji wa vitu vilivyo karibu nawe na matangazo kulingana na eneo uliko.

Kulingana na bidhaa unazotumia na mipangilio unayoteua, Google inaweza kutumia maelezo tofauti ya mahali kuwezesha bidhaa na huduma unazotumia zikufae zaidi. Maelezo haya ni pamoja na:

Aina za data ya mahali tunazokusanya na muda ambao tunazihifadhi zinategemea kwa kiwango fulani mipangilio ya kifaa na akaunti yako. Kwa mfano, unaweza kuwasha au kuzima kipengele cha mahali kwenye kifaa chako cha Android ukitumia programu ya mipangilio ya kifaa. Unaweza pia kuwasha kipengele cha Kumbukumbu ya Maeneo Yangu ikiwa ungependa kuunda ramani ya faragha ya unakokwenda ukiwa na vifaa ulivyotumia kuingia katika akaunti. Na iwapo umewasha mipangilio yako ya Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu, utafutaji unaofanya na shughuli nyingine kutoka kwenye Huduma za Google, ambazo zinaweza pia kujumuisha maelezo ya mahali, huhifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia maelezo ya mahali.


Katika hali fulani, Google pia hukusanya taarifa kukuhusu kutoka kwenye nyenzo zinazopatikana hadharani. Kwa mfano, ikiwa jina lako limeandikwa kwenye gazeti la eneo uliko, mtambo wa kutafuta kwenye Google unaweza kuainisha makala hayo na kuyaonyesha kwa watu wengine wakitafuta jina lako. Tunaweza pia kukusanya taarifa kukuhusu kutoka kwa washirika wanaoaminika, kama vile huduma za saraka, ambao hutupa maelezo ya biashara yatakayoonyeshwa kwenye huduma za Google; washirika wa biashara ambao hutupa maelezo kuhusu wateja watarajiwa wa huduma zetu za biashara; na washirika wa usalama ambao hutupa maelezo ili kulinda dhidi ya matumizi mabaya. Tunapokea pia taarifa kutoka kwa washirika ili kutoa huduma za utangazaji na utafiti kwa niaba yao.

Tunatumia teknolojia mbalimbali kukusanya na kuhifadhi maelezo, vikiwemo vidakuzi, lebo za pikseli, hifadhi za ndani kama vile hifadhi ya kivinjari au akiba za data ya programu, hifadhidata na kumbukumbu za seva.

Sababu ya Google kukusanya data

Tunatumia data tunayokusanya kuboresha huduma

Tunatumia maelezo tunayokusanya kutoka kwenye huduma zetu zote kwa madhumuni yafuatayo:

Kutoa huduma zetu

Tunatumia maelezo yako kutoa huduma zetu, kama vile kuchakata hoja unazotafuta ili kukupa matokeo au kukusaidia kushiriki maudhui kwa kukupendekezea wapokeaji kati ya watu unaowasiliana nao.

Kudumisha na kuboresha huduma zetu

Pia tunatumia maelezo yako kuhakikisha kuwa huduma zetu zinafanya kazi ipasavyo, kama vile kufuatilia hitilafu au kutatua matatizo unayoripoti kwetu. Tunatumia pia maelezo yako kuboresha huduma zetu — kwa mfano, kutambua hoja za utafutaji ambazo huendelezwa visivyo mara nyingi kunatusaidia kuboresha vipengele vya kikagua maendelezo vinavyotumika katika huduma zetu zote.

Kuunda huduma mpya

Tunatumia maelezo tunayokusanya katika huduma zilizopo kutusaidia kuunda huduma mpya. Kwa mfano, baada ya kuelewa jinsi watu wanavyopanga picha zao katika programu ya Picasa ambayo ndiyo programu ya kwanza ya picha ya Google, tuliweza kuunda na kuanzisha programu ya Picha kwenye Google.

Kutoa huduma zinazokufaa, ikiwa ni pamoja na maudhui na matangazo

Tunatumia maelezo tunayokusanya ili kukupa huduma zilizowekewa mapendeleo, ikiwemo kukupa mapendekezo, maudhui na matokeo ya utafutaji uliowekewa mapendeleo. Kwa mfano, huduma ya Ukaguzi wa Usalama hukupa vidokezo vya usalama vinavyotokana na jinsi unavyotumia bidhaa za Google. Na kulingana na mipangilio yako, Google Play inaweza kutumia maelezo kama vile programu ambazo tayari umeweka kwenye kifaa na video ulizotazama kwenye YouTube ili kupendekeza programu mpya unazoweza kupenda.

Kulingana na mipangilio yako, tunaweza pia kukuonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo kulingana na mambo yanayokuvutia kwenye huduma za Google. Kwa mfano, ukitafuta "baiskeli za kukwea milima" huenda ukaona matangazo ya vifaa vya spoti kwenye YouTube. Unaweza kudhibiti aina ya maelezo tunayotumia ili kukuonyesha matangazo kwa kutembelea mipangilio yako ya matangazo kwenye Kituo Changu cha Matangazo.

  • Hatutumii vigezo nyeti, kama vile rangi, dini, mwelekeo wa ngono au afya kukuonyesha matangazo yanayokufaa.
  • Hatukuonyeshi matangazo yaliyowekewa mapendeleo kulingana na maudhui yako kutoka huduma za Hifadhi, Gmail au Picha.
  • Hatushiriki maelezo yako yanayokutambulisha binafsi kwa watangazaji kama vile jina au anwani yako ya barua pepe isipokuwa utuombe kufanya hivyo. Kwa mfano, ukiona tangazo la duka la maua lililo karibu nawe kisha uchague "gusa ili upige simu", tutaunganisha simu yako na tunaweza kushiriki nambari yako ya simu na duka hilo la maua.

Pima utendaji

Tunatumia data katika uchanganuzi na upimaji ili kuelewa jinsi huduma zetu zinavyotumiwa. Kwa mfano, tunachanganua data kuhusu mara unazotembelea tovuti zetu ili kufanya mambo kama vile kuboresha muundo wa bidhaa. Tunatumia pia data kuhusu matangazo unayoangalia, ikiwa ni pamoja na shughuli zako zinazohusiana kwenye Tafuta na Google, ili kuwasaidia watangazaji kuelewa utendaji wa kampeni za matangazo yao. Tunatumia zana mbalimbali kutekeleza haya, ikiwemo Google Analytics. Unapotembelea tovuti au programu zinazotumia Google Analytics, mteja wa Google Analytics anaweza kuchagua kuruhusu Google iunganishe maelezo yanayohusu shughuli zako kutoka kwenye tovuti au programu hiyo na shughuli kutoka kwenye tovuti au programu nyingine zinazotumia huduma zetu za matangazo.

Kuwasiliana nawe

Tunatumia maelezo yako tunayokusanya, kama vile anwani yako ya barua pepe ili kuwasiliana nawe moja kwa moja. Kwa mfano, tunaweza kukuarifu tunapogundua shughuli za kutiliwa shaka kama vile jaribio la kuingia katika Akaunti yako ya Google kutoka mahali ambapo si pa kawaida. Au tunaweza kukujulisha kuhusu mabadiliko au maboresho yajayo kwenye huduma zetu. Na unapowasiliana na Google, tutaweka rekodi ya ombi lako ili tukusaidie kutatua tatizo lolote unalokumbana nalo.

Kulinda Google, watumiaji wetu na umma

Tunatumia maelezo ili kusaidia kuboresha usalama na uaminifu wa huduma zetu. Hii ni pamoja na kutambua, kuzuia na kushughulikia ulaghai, matumizi mabaya, hatari za usalama na matatizo ya kiufundi yanayoweza kuathiri Google, watumiaji wetu, au umma.


Tunatumia teknolojia tofauti kuchakata maelezo yako kwa madhumuni haya. Tunatumia mifumo ya kiotomatiki ambayo huchanganua maudhui yako ili kukupa huduma kama vile matokeo ya utafutaji yaliyoboreshwa, matangazo yanayokufaa au vipengele vingine kulingana na jinsi unavyotumia huduma zetu. Tunachanganua pia maudhui yako ili tuweze kugundua matumizi mabaya kama vile barua taka, programu hasidi na maudhui yasiyo halali. Pia tunatumia algoriti ili kutambua ruwaza katika data. Kwa mfano, Tafsiri na Google huwasaidia watu wa lugha tofauti kuwasiliana kwa kuchunguza ruwaza za kawaida za lugha katika vifungu vya maneno ambavyo ungependa itafsiri.

Tunaweza kutumia maelezo tunayokusanya kwenye huduma zetu na kwenye vifaa vyako kwa madhumuni yaliyobainishwa hapo juu. Kwa mfano, kulingana na mipangilio yako, ukitazama video za wacheza gita kwenye YouTube, unaweza kuona tangazo la mafunzo ya kucheza gita kwenye tovuti inayotumia bidhaa zetu za matangazo. Kulingana na mipangilio ya akaunti yako, shughuli zako kwenye programu na tovuti zingine zinaweza kuhusishwa na taarifa zako binafsi ili kuboresha huduma na matangazo ya Google.

Ikiwa watumiaji wengine tayari wana anwani yako ya barua pepe au maelezo yako mengine ya binafsi, tunaweza kuwaonyesha maelezo yako ya Akaunti ya Google yanayoonekana kwa umma, kama vile jina na picha yako. Kwa mfano, hatua hii huwasaidia watu kutambua barua pepe inayotoka kwako.

Tutaomba idhini yako kabla ya kutumia maelezo yako kwa madhumuni ambayo hayajatajwa katika Sera hii ya Faragha.

Vidhibiti vyako vya faragha

Unaweza kuchagua maelezo tunayoweza kukusanya na jinsi tunavyoyatumia

Sehemu hii inafafanua vidhibiti muhimu vya kudhibiti faragha yako katika huduma zetu zote. Unaweza pia kutembelea Ukaguzi wa Faragha, ambapo utaweza kukagua na kubadilisha mipangilio muhimu ya faragha. Mbali na zana hizi, tunatoa pia mipangilio maalum ya faragha katika bidhaa zetu - unaweza kupata maelezo zaidi kwenye Mwongozo wetu wa Faragha ya Bidhaa.

Kudhibiti, kukagua na kusasisha maelezo yako

Ukiwa umeingia katika akaunti, unaweza kukagua na kusasisha maelezo wakati wowote kwa kutembelea huduma unazotumia. Kwa mfano, Picha kwenye Google na Hifadhi ya Google zimeundwa ili kukusaidia kudhibiti aina mahususi za maudhui ambayo umehifadhi kwenye Google.

Pia unaweza kukagua na kudhibiti maelezo yaliyohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google. Akaunti yako ya Google inajumuisha:

Vidhibiti vya faragha

Vidhibiti vya Shughuli

Teua aina za shughuli ambazo ungependa kuhifadhi katika akaunti yako. Kwa mfano, iwapo umewasha mipangilio ya Historia ya YouTube, video unazotazama na mambo unayotafuta huhifadhiwa kwenye akaunti yako ili uweze kupata mapendekezo bora na ukumbuke ulikoachia. Na iwapo umewasha mipangilio ya Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu, utafutaji unaofanya na shughuli kutoka huduma nyingine za Google huhifadhiwa kwenye akaunti yako ili upate hali za utumiaji zinazokufaa zaidi kama vile utafutaji wa haraka na mapendekezo muhimu zaidi ya programu na maudhui. Mipangilio ya Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu pia ina mipangilio midogo inayokuruhusu udhibiti iwapo maelezo kuhusu shughuli zako kwenye tovuti, programu na vifaa vingine vinavyotumia Huduma za Google, kama vile programu unazosakinisha na kutumia kwenye Android, yanahifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google na kutumiwa kuboresha Huduma za Google.

Nenda kwenye Vidhibiti vya Shughuli

Mipangilio ya matangazo

Dhibiti mapendeleo yako ya matangazo unayoona kwenye Google na kwenye tovuti na programu zinazoshirikiana na Google kuonyesha matangazo. Unaweza kubadilisha mambo yanayokuvutia, kuchagua ikiwa maelezo yako ya binafsi yanaweza kutumiwa kukuonyesha matangazo yanayokufaa na kuwasha au kuzima huduma fulani za matangazo.

Nenda kwenye Kituo changu cha Matangazo

Kukuhusu

Dhibiti taarifa binafsi katika Akaunti yako ya Google na udhibiti wanaoweza kuziona kwenye Huduma za Google.

Nenda kwenye sehemu ya Kukuhusu

Mapendekezo kutoka miduara yako

Chagua ikiwa ungependa jina na picha yako zionekana kando ya shughuli zako, kama vile maoni na mapendekezo yanayoonekana katika matangazo.

Nenda kwenye ukurasa wa Mapendekezo kutoka miduara yako

Tovuti na programu ambazo hutumia Huduma za Google

Dhibiti maelezo ambayo tovuti na programu zinazotumia Huduma za Google, kama vile Google Analytics, zinaweza kushiriki na Google unapotembelea au kutumia huduma zake.

Nenda kwenye sehemu ya Jinsi Google inavyotumia maelezo kutoka kwenye tovuti au programu zinazotumia huduma zetu

Jinsi ya kukagua na kusasisha maelezo yako

Shughuli Zangu

Kipengele cha Shughuli Zangu hukuwezesha kukagua na kudhibiti data ambayo imehifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google ukiwa umeingia katika akaunti na unapotumia Huduma za Google, kama vile utafutaji uliofanya au kutembelea Google Play. Unaweza kuvinjari kulingana na tarehe na mada na kufuta baadhi ya shughuli au shughuli zako zote.

Tembelea ukurasa wa Shughuli Zangu

Dashibodi ya Google

Dashibodi ya Google inakuwezesha kudhibiti maelezo yanayohusiana na bidhaa mahususi.

Nenda kwenye Dashibodi

Maelezo yako ya binafsi

Dhibiti maelezo yako ya mawasiliano, kama vile jina, anwani ya barua pepe na nambari yako ya simu.

Nenda kwenye ukurasa wa Maelezo ya Binafsi

Ukiwa umeondoka katika akaunti, unaweza kudhibiti maelezo yanayohusiana na kivinjari au kifaa chako, ikiwa ni pamoja na:

Kuhamisha, kuondoa na kufuta maelezo yako

Unaweza kuhamishia nakala ya maudhui kwenye Akaunti yako ya Google ikiwa ungependa kuhifadhi nakala yake au kuitumia katika huduma isiyo ya Google.

Ili ufute maelezo yako, unaweza:

Kidhibiti cha Akaunti Isiyotumika kinakuruhusu kumpa mtu mwingine uwezo wa kufikia sehemu za Akaunti yako ya Google endapo hutaweza kutumia akaunti yako kutokana na matukio yasiyotarajiwa.

Na mwishowe, unaweza pia kuomba kuondoa maudhui kwenye huduma mahususi za Google kulingana na sheria zinazotumika na sera zetu.


Kuna njia nyingine za kudhibiti maelezo ambayo Google hukusanya iwe umeingia au hujaingia katika Akaunti ya Google, ikiwa ni pamoja na:

  • Mipangilio ya kivinjari: Kwa mfano, unaweza kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili kikuarifu Google inapoweka kidakuzi katika kivinjari chako. Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili uzuie vidakuzi vyote vya kikoa mahususi au vikoa vyote. Lakini kumbuka kuwa huduma zetu zinategemea vidakuzi ili zifanye kazi ipasavyo, kwa mambo kama vile kukumbuka mapendeleo yako ya lugha.
  • Mipangilio ya kifaa: Huenda kifaa chako kina vidhibiti vinavyobaini maelezo tunayoweza kukusanya. Kwa mfano, unaweza kubadilisha mipangilio ya mahali kwenye kifaa chako cha Android.

Kushiriki maelezo yako

Unaposhiriki maelezo yako

Huduma zetu nyingi hukuruhusu kushiriki maelezo na watu wengine na unaweza kudhibiti jinsi unavyoshiriki. Kwa mfano, unaweza kushiriki video kwenye YouTube kwa umma au uziweke kwa faragha. Kumbuka, unaposhiriki maelezo kwa umma, maudhui yako yanaweza kufikiwa kupitia mitambo ya kutafuta, ikiwemo Huduma ya Tafuta na Google.

Unapotumia huduma fulani za Google ukiwa umeingia katika akaunti, kama vile kutoa maoni kuhusu video kwenye YouTube au kuhusu programu kwenye Google Play, jina na picha yako zitaonekana kando ya shughuli zako. Tunaweza pia kuonyesha maelezo haya katika matangazo kulingana na mipangilio yako ya Mapendekezo kutoka miduara yako.

Google inaposhiriki maelezo yako

Hatushiriki maelezo yako ya binafsi na kampuni, mashirika au watu binafsi nje ya Google isipokuwa mojawapo ya hali zifuatazo itokee:

Kwa idhini yako

Tutashiriki taarifa binafsi nje ya Google ukikubali. Kwa mfano, iwapo unatumia Google Home kuweka nafasi kupitia huduma ya kuweka nafasi, tutaomba ruhusa yako kabla ya kushiriki jina au nambari yako ya simu na mkahawa. Pia, tutakupa vidhibiti vya kukagua na kudhibiti tovuti na programu za wengine ambazo umezipa uwezo wa kufikia data kwenye Akaunti yako ya Google. Tutaomba idhini yako dhahiri ili kushiriki taarifa zozote binafsi zilizo nyeti.

Na wasimamizi wa kikoa

Ikiwa wewe ni mwanafunzi au unafanya kazi katika shirika linalotumia huduma za Google, msimamizi wa kikoa chako na wauzaji wanaodhibiti akaunti yako wataweza kufikia Akaunti yako ya Google. Wanaweza:

  • Kufikia na kudumisha maelezo yaliyohifadhiwa katika akaunti yako, kama vile barua pepe zako
  • Kuona takwimu kuhusu akaunti yako, kama vile idadi ya programu unazosakinisha
  • Kubadilisha nenosiri la akaunti yako
  • Kusimamisha au kukomesha ufikiaji wa akaunti yako
  • Kupokea maelezo ya akaunti yako ili kutimiza sheria, kanuni, mchakato wa kisheria, au ombi husika la kutekelezeka la kiserikali
  • Kuzuia uwezo wako wa kufuta au kubadilisha maelezo au mipangilio yako ya faragha

Kwa mchakato wa nje

Tunatoa taarifa binafsi kwa washirika wetu na kwa biashara au watu wengine tunaowaamini ili wazichakate kwa niaba yetu, kulingana na maagizo yetu na kwa kufuata Sera yetu ya Faragha na hatua nyingine zozote zinazofaa za usiri na usalama. Kwa mfano, tunatumia watoa huduma ili kusaidia kuendesha vituo vyetu vya data, kutoa huduma na bidhaa zetu, kuboresha michakato yetu ya ndani ya biashara na kutoa usaidizi wa ziada kwa wateja na watumiaji. Pia, tunatumia watoa huduma ili kusaidia kukagua maudhui kwenye video ya YouTube kwa ajili ya usalama wa umma na kuchanganua na kusikiliza sampuli za sauti ya watumiaji iliyohifadhiwa ili kusaidia kuboresha teknolojia za Google za utambuzi wa sauti.

Kwa sababu za kisheria

Tutatuma taarifa binafsi nje ya Google ikiwa tunaamini kwa nia njema kwamba ufumbuzi wa maelezo hayo unafaa kiuadilifu katika:

Tunaweza kushiriki maelezo ya jumla yasiyoweza kukutambulisha kibinafsi kwa umma na pia na washirika wetu — kama vile wachapishaji, watangazaji, wasanidi programu au wenye hakimiliki. Kwa mfano, tunashiriki maelezo kwa umma ili kuonyesha mitindo kuhusu utumiaji wa jumla wa huduma zetu. Pia tunaruhusu washirika mahususi kukusanya maelezo kutoka kwenye kivinjari au kifaa chako kwa madhumuni ya matangazo na kupima kwa kutumia vidakuzi vyao au teknolojia sawa.

Ikiwa Google itahusishwa katika muungano na kampuni nyingine, ununuzi au uuzaji wa mali, tutadumisha usiri wa maelezo yako ya binafsi na kuwajulisha watumiaji walioathirika kabla ya kuhamisha maelezo yao ya binafsi au kuyaweka chini ya sera tofauti ya faragha.

Kulinda maelezo yako

Tunadumisha usalama katika huduma zetu ili kulinda maelezo yako

Bidhaa zote za Google zina vipengele thabiti vya usalama ambavyo hulinda maelezo yako kila wakati. Ufahamu tunaopata kutokana na kudumisha huduma zetu hutusaidia kukulinda kwa kutambua na kuzuia kiotomatiki vitisho vya usalama. Ikiwa tutagundua vitisho vya usalama ambavyo tunaamini unapaswa kujua, tutakuarifu na kukupa hatua za kuchukua ili kujilinda vyema.

Tunajitahidi kukulinda wewe pamoja na Google dhidi ya ufikiaji, mabadiliko, ufumbuzi au uharibifu usioidhinishwa wa maelezo tuliyoweka, ikiwa ni pamoja na:

  • Tunatumia usimbaji fiche ili kuweka data yako faraghani tunapoihamisha
  • Tuna vipengele mbalimbali vya usalama vinavyokuwezesha kulinda akaunti yako. Vipengele hivi ni kama vile Kuvinjari Salama, Ukaguzi wa Usalama na Uthibitishaji wa Hatua Mbili
  • Tunakagua desturi zetu za maelezo tunayokusanya, hifadhi na uchakataji wake, ikiwa ni pamoja na hatua halisi za usalama, ili kulinda mifumo yetu dhidi ya ufikiaji ambao haujaidhinishwa.
  • Maelezo ya binafsi yanaweza kufikiwa tu na waajiriwa wa Google, wanakandarasi na mawakala ambao tumewaruhusu kuchakata maelezo hayo. Mtu yeyote aliye na idhini ya kufikia maelezo haya anapaswa kuzingatia kikamilifu wajibu wa usiri wa mkataba na anaweza kuadhibiwa au kusimamishwa ikiwa atakiuka wajibu huu.

Kuhamisha na kufuta maelezo yako

Unaweza kuhamishia au kufuta nakala ya maelezo kwenye Akaunti yako ya Google wakati wowote.

Unaweza kuhamishia nakala ya maudhui kwenye Akaunti yako ya Google ikiwa ungependa kuhifadhi nakala yake au kuitumia katika huduma isiyo ya Google.

Ili ufute maelezo yako, unaweza:

Kuhifadhi taarifa zako

Tunahifadhi data ambayo tunakusanya kwa vipindi tofauti kwa kutegemea aina ya data, jinsi tunavyoitumia na jinsi unavyoweka mipangilio yako:

  • Unaweza kufuta baadhi ya data wakati wowote unaopenda, kama vile taarifa zako binafsi au maudhui unayobuni au kupakia, kama vile picha na hati. Unaweza pia kufuta maelezo ya shughuli yaliyohifadhiwa katika akaunti yako, au uchague yafutwe kiotomatiki baada ya kipindi kilichobainishwa. Tutahifadhi data hii kwenye Akaunti yako ya Google hadi utakapoiondoa au kuchagua kuruhusu iondolewe.
  • Data nyingine hufutwa au utambulisho wake hufichwa kiotomatiki baada ya kipindi kilichobainishwa, kama vile data ya utangazaji katika kumbukumbu za seva.
  • Tunahifadhi baadhi ya data hadi utakapofuta Akaunti yako ya Google, kama vile maelezo kuhusu mara ambazo unatumia huduma zetu.
  • Na tunahifadhi baadhi ya data kwa vipindi virefu panapohitajika kwa madhumuni halali ya kibiashara au kisheria, kama vile kulinda usalama, kuzuia ulaghai na matumizi mabaya au kuweka rekodi za kifedha.

Unapofuta data, tunazingatia mchakato wa kufuta ili kuhakikisha kwamba data yako imeondolewa kabisa kwenye seva zetu kwa njia salama au imehifadhiwa tu kwa namna inayoficha utambulisho wake. Tunajitahidi kuhakikisha kuwa huduma zetu zinalinda taarifa ili yasifutwe kimakosa au kwa nia ya kudhuru. Kwa sababu hii, huenda ikachukua muda kuondoa kitu unachofuta kwenye mifumo yetu inayofanya kazi na kwenye mifumo ya kuhifadhi nakala.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu vipindi vya kuhifadhi data kwenye Google, ikiwa ni pamoja na muda tunaohifadhi taarifa zako kabla ya kuzifuta.

Uzingatiaji na ushirikiano na wasimamizi

Sisi hukagua Sera hii ya Faragha mara kwa mara na kuhakikisha kwamba tunachakata maelezo yako kwa kuzingatia sera hii.

Uhamishaji data

Tuna seva duniani kote na maelezo yako yanaweza kuchakatwa kwenye seva zilizo nje ya nchi unakoishi. Sheria za ulinzi wa data hutofautiana katika kila nchi. Kuna nchi ambazo hutoa ulinzi zaidi kuliko nyingine. Popote maelezo yako yanapochakatwa tunazingatia sheria za ulinzi wa data kama ilivyofafanuliwa kwenye sera hii. Pia, tunatii mifumo fulani ya kisheria inayohusiana na uhamishaji wa data.

Tunapopokea malalamiko yaliyoandikwa kirasmi, tunayachakata kwa kuwasiliana na mtu aliyetoa malalamiko hayo. Tunafanya kazi na mamlaka ya sheria inayohusika, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kulinda data ya eneo, ili kutatua malalamiko yoyote kuhusiana na uhamishaji wa data yako ambayo hatuwezi kutatua na wewe moja kwa moja.

Masharti ya kisheria ya majimbo ya Marekani

Baadhi ya Sheria za faragha za majimbo ya Marekani huhitaji ufumbuzi mahususi.

Sera hii ya Faragha imetungwa kukusaidia uelewe jinsi Google hushughulikia taarifa yako:

  • Tunaelezea aina za taarifa ambazo Google hukusanya na vyanzo vya taarifa hizo katika sehemu ya Taarifa ambazo Google hukusanya.
  • Tunafafanua sababu za Google kukusanya na kutumia taarifa katika sehemu ya Kwa nini Google hukusanya data.
  • Tunafafanua hali ambazo Google inaweza kufumbua taarifa katika sehemu ya Kushiriki maelezo yako. Google haiuzi taarifa zako binafsi. Google pia "haishiriki" taarifa zako binafsi jinsi neno hilo lilivyofafanuliwa katika Sheria ya California ya Ulinzi wa Faragha ya Watumiaji (CCPA).
  • Tunafafanua jinsi Google inavyohifadhi taarifa katika sehemu ya Kuhifadhi taarifa zako. Pia, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyoficha utambulisho wa data. Kama ilivyoelezwa kwenye sehemu husika, Google inapoficha utambulisho wa data ili kulinda faragha yako, tunadumisha sera na hatua za kiufundi ili kuepuka uwezekano wa kutambua tena taarifa hizo.

Sheria za faragha za majimbo ya Marekani pia hutoa haki ya kuomba maelezo kuhusu jinsi Google hukusanya, kutumia na kufumbua taarifa zako. Pia, sheria hizo zinakupatia haki ya kufikia taarifa zako, wakati mwingine katika muundo wa kubebeka; kusahihisha taarifa zako; na kuomba Google ifute taarifa hizo. Sheria hizi nyingi hutoa pia haki ya kujiondoa kwenye aina fulani za matangazo yanayolengwa na kuchanganua. Hutoa pia haki ya kutobaguliwa kwa kutumia haki hizi za faragha. Zaidi ya hayo, CCPA huchukulia aina fulani za taarifa, kama vile data ya afya, kuwa nyeti; wakati watumiaji hutoa taarifa hii, Google huitumia tu kwa madhumuni yanayoruhusiwa na CCPA, kama vile kutoa huduma ambazo zimeombwa na kutarajiwa na watumiaji wetu.

Sheria ya Washington ya Afya Yangu Data Yangu na Mswada wa 370 wa Seneti ya Nevada zinatoa haki mahususi kando na haki zilizo hapo juu, zinazotumika kwa maelezo ya afya. Unapotoa maelezo haya, Google huyachakata tu kwa idhini yako na hukuruhusu kuondoa idhini yako.

Tunafafanua chaguo ulizo nazo za kudhibiti faragha na data yako kwenye huduma za Google katika Vidhibiti vyako vya faragha. Zana hizi zinakuwezesha ufikie, ukague, usasishe na ufute taarifa zako, pamoja na kutuma na kupakua nakala ya taarifa hizo. Pia, unaweza kudhibiti aina ya taarifa tunazotumia ili kukuonyesha matangazo au kuzima matangazo yaliyowekewa mapendeleo, kwa kutembelea Kituo Changu cha Matangazo.

Unapotumia zana hizi, tutaidhinisha ombi lako kwa kuthibitisha kuwa umeingia katika Akaunti yako ya Google. Iwapo una maswali au maombi yanayohusiana na haki zako chini ya Sheria za faragha za majimbo ya Marekani, wewe (au mwakilishi wako rasmi) mnaweza pia kuwasiliana na Google. Na ikiwa hukubali uamuzi kuhusu ombi lako, unaweza kuiomba Google iliangalie upya kwa kujibu barua pepe yetu.

Tunatoa pia maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyoshughulikia maombi ya CCPA.

Baadhi ya Sheria za faragha za majimbo ya Marekani huhitaji pia maelezo ya kanuni za data kwa kutumia aina mahususi. Jedwali hili linatumia aina hizi kupanga taarifa katika Sera hii ya Faragha.

Aina za taarifa tunazokusanya

Vitambulishi au taarifa zinazohusiana kama vile jina lako na nenosiri, nambari ya simu na anwani pamoja na vitambulishi vya kipekee vinavyohusishwa na kivinjari, programu au kifaa unachokitumia. Baadhi ya huduma za Google kama vile Studio ya YouTube hutoa chaguo la kuwasilisha kitambulisho halali (kama vile pasipoti au leseni ya udereva) ili kuthibitisha utambulisho wako ili utumie vipengele vya ziada.

Maelezo ya demografia, kama vile umri, jinsia na lugha yako. Iwapo utachagua kutumia vipengele vya hiari kama vile YouTube Creator Demographics, unaweza pia kutoa taarifa za ziada kama vile utambulisho wako wa kijinsia au mbari na kabila.

Maelezo ya biashara kama vile maelezo ya malipo na historia ya ununuzi unaofanya kwenye huduma za Google.

Maelezo ya kibayometriki iwapo utachagua kuyatoa, kama vile alama za vidole kwenye tafiti za kubuni bidhaa za Google.

Intaneti, mtandao na taarifa nyingine za shughuli kama vile hoja zako za utafutaji, mara ambazo umetazama na kutumia maudhui na matangazo; historia ya kuvinjari kwenye Chrome ambayo umesawazisha kwenye Akaunti yako ya Google; taarifa kuhusu utumiaji wa programu, vivinjari, na vifaa vyako kwenye huduma zetu (kama vile Anwani ya IP, ripoti ya kuacha kufanya kazi na shughuli za mfumo); na shughuli kwenye tovuti na programu za wengine zinazotumia huduma zetu. Unaweza kukagua na kudhibiti data ya shughuli inayohifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google katika sehemu ya Shughuli Zangu.

Data ya kutambulisha mahali, jinsi inavyoweza kubainishwa na GPS, Anwani ya IP na data nyingineyo kutoka vitambuzi vilivyo kwenye kifaa chako au karibu nacho, kulingana kwa kiasi fulani na mipangilio ya akaunti na kifaa chako. Kulingana na mipangilio hii, huenda ikajumuisha data ya eneo mahususi, kwa mfano data ya GPS kwa vipengele vya Android kama vile uelekezaji au kutafuta simu yako. Pata maelezo zaidi kuhusu Jinsi Google inavyotumia taarifa ya mahali.

Taarifa za sauti, elektroniki, video na taarifa sawa na hizo, kama vile taarifa za sauti na matamshi.

Data ya mawasiliano, kama vile barua pepe, ikiwa unatumia huduma zetu kutuma na kupokea ujumbe.

Maelezo ya afya iwapo utaamua kutoa maelezo hayo, kama vile historia ya matibabu, viashiria muhimu vya mwili, vipimo vya afya (kama vile kiwango cha sukari kwenye damu) na maelezo mengine kama hayo yanayohusu afya yako ya mwili au akili, wakati unatumia huduma za Google zenye vipengele vinavyohusiana na afya, kama vile Programu ya Google Health Studies, vifaa vya Pixel au Fitbit.

Taarifa za kitaalamu, kikazi na kielimu, kama vile taarifa unazotoa au zinazohifadhiwa kupitia shirika linalotumia huduma za Google unakofanyia kazi au kusomea.

Taarifa nyingine unazotunga au kutoa, kama vile maudhui unayobuni, kupakia au kupokea (kama vile picha na video au barua pepe, hati na malahajedwali). Dashibodi ya Google hukuruhusu udhibiti taarifa zinazohusiana na bidhaa mahususi.

Maelezo yanayotokana na taarifa hapo juu, kama vile aina za matangazo yanayokuvutia.

Madhumuni ya biashara ambayo maelezo yanaweza kutumika au kufumbuliwa

Kutoa ulinzi dhidi ya tishio za usalama, matumizi mabaya na shughuli haramu: Google hutumia na inaweza kufumbua taarifa ili kutambua, kuzuia na kushughulikia matukio ya kiusalama na kutoa ulinzi dhidi ya shughuli zingine hasidi, za kupotosha, za ulaghai au haramu. Kwa mfano, ili kulinda huduma zetu, huenda Google ikapokea au ikafichua taarifa kuhusu anwani za IP ambazo zimeathiriwa na watumiaji hasidi.

Hesabu na vipimo: Google hutumia taarifa za takwimu na vipimo ili kuelewa jinsi huduma zetu zinavyotumika, pamoja na kutimiza wajibu kwa washirika wetu kama vile wachapishaji, watangazaji, wasanidi programu au wenye hakimiliki. Tunaweza kufumbua taarifa zisizomtambulisha mtu mahususi hadharani na kwa washirika hawa, ikiwa ni pamoja na kwa madhumuni ya kufanya hesabu.

Kudumisha huduma zetu: Google hutumia taarifa kuhakikisha kuwa huduma zetu zinafanya kazi ipasavyo, kama vile kufuatilia matatizo na kutatua hitilafu na matatizo mengine unayoripoti kwetu.

Utafiti na ubunifu: Google hutumia taarifa kuboresha huduma zetu na kubuni bidhaa, vipengele na teknolojia mpya ambazo huwafaa watumiaji wetu na umma. Kwa mfano, tunatumia taarifa zinazopatikana hadharani kusaidia kufunza miundo ya AI ya Google na kubuni bidhaa na vipengele kama vile Google Tafsiri, Programu za Gemini na uwezo wa AI ya Wingu.

Utumiaji wa watoa huduma: Google hushiriki taarifa na watoa huduma ili kutoa huduma kwa niaba yetu, kwa kutii Sera yetu ya Faragha na hatua nyingine zinazofaa za usiri na usalama. Kwa mfano, tunaweza kutegemea watoa huduma ili kutusaidia kutoa usaidizi kwa wateja.

Utangazaji: Google huchakata taarifa ili kuonyesha matangazo, ikiwa ni pamoja na vitambulishi vya mtandaoni, shughuli za kuvinjari na utafutaji na maelezo kuhusu mahali ulipo na unavyotumia matangazo. Hali hii hufanya huduma za Google, tovuti na huduma nyinginezo unazotumia zitolewe bila malipo. Unaweza kudhibiti aina ya taarifa tunazotumia ili kukuonyesha matangazo kwa kutembelea mipangilio yako ya matangazo kwenye Kituo Changu cha Matangazo.

Sababu za kisheria: Google pia hutumia taarifa kutii kanuni au sheria zinazotumika na hufichua taarifa zikihitajika katika mchakato wa kisheria au maombi ya serikali yanayoweza kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa sheria. Tunatoa taarifa kuhusu idadi na aina ya maombi tunayopokea kutoka kwa serikali katika Ripoti yetu ya Uwazi.

Washirika ambao tunaweza kuwafumbulia taarifa

Watu wengine unaochagua kuruhusu wafikie taarifa zako, kama vile hati au picha, video au maoni kwenye YouTube au maelezo ya afya kupitia vipengele vya kijamii vya Fitbit na programu za wengine.

Washirika wengine wenye idhini yako, kama vile huduma ambazo hujumuishwa na huduma za Google. Unaweza kukagua na kudhibiti programu na tovuti za washirika wengine zenye uwezo wa kufikia data kwenye Akaunti yako ya Google. Angalia maelezo zaidi kuhusu wakati Google huruhusu maelezo yako yafikiwe.

Watoa huduma, biashara au watu wanaoaminika na ambao huchakata taarifa kwa niaba ya Google, kulingana na maagizo yetu na kwa kutii Sera yetu ya Faragha na hatua nyingine zozote zinazofaa za usiri na usalama.

Wasimamizi wa vikoa, iwapo unafanya kazi au kusoma katika shirika linalotumia huduma za Google.

Watekelezaji wa sheria au washirika wengine, kwa sababu za kisheria zilizoelezewa katika sehemu ya Kushiriki taarifa zako.

Kuhusu sera hii

Sera hii inapotumika

Sera hii ya Faragha inatumika kwa huduma zote za Google LLC na washirika wake wadogo, ikiwa ni pamoja na YouTube, Android na huduma kwenye tovuti nyingine kama vile huduma za matangazo. Sera hii ya Faragha haitumiki kwa huduma ambazo zina sera tofauti za faragha ambazo hazijumuishi Sera hii ya Faragha.

Sera hii ya Faragha haitumiki kwa:

  • Desturi za mawasiliano za kampuni na mashirika mengine yanayotangaza huduma zetu
  • Huduma zinazotolewa na kampuni au watu wengine, ikiwa ni pamoja na tovuti au bidhaa wanazotoa ambazo zinaweza kujumuisha Huduma za Google ambazo zinasimamiwa na sera hii, au bidhaa au tovuti unazoonyeshwa katika matokeo ya utafutaji, au zilizounganishwa kutoka kwenye huduma zetu

Mabadiliko kwenye sera hii

Sera hii ya Faragha hubadilishwa mara kwa mara. Hatutapunguza haki zako kwa mujibu wa Sera hii ya Faragha bila kibali chako dhahiri. Tunahakikisha kuwa tumeonyesha tarehe ambayo sera ilibadilishwa mara ya mwisho na tunakupa idhini ya kufikia matoleo yaliyohifadhiwa kwenye kumbukumbu ili uweze kuyakagua. Ikiwa mabadiliko ni muhimu, tutakuarifu kwa kina zaidi (pamoja na, kwa huduma fulani, utaarifiwa kupitia barua pepe kuhusu mabadiliko ya Sera ya Faragha).

Desturi za faragha zinazohusiana

Huduma mahususi za Google

Ilani zifuatazo za faragha hutoa maelezo ya ziada kuhusu huduma fulani za Google:

Ikiwa wewe ni mwanachama wa shirika linalotumia Google Workspace au Mfumo wa Wingu la Google, pata maelezo kuhusu jinsi huduma hizi hukusanya na kutumia taarifa zako binafsi katika Ilani ya Faragha ya Wingu la Google.

Nyenzo nyingine muhimu

Viungo vifuatavyo vinaonyesha nyenzo muhimu za kupata maelezo zaidi kuhusu desturi na mipangilio yetu ya faragha.

Masharti muhimu

Akaunti ya Google

Unaweza kufikia baadhi ya huduma zetu kwa kufungua Akaunti ya Google na kutoa baadhi ya maelezo yako ya binafsi (kwa kawaida jina lako, anwani ya barua pepe na nenosiri). Maelezo haya ya akaunti hutumiwa kukuthibitisha unapofikia huduma za Google na kulinda akaunti yako isifikiwe na watu ambao hujawaidhinisha. Unaweza kubadilisha maelezo kwenye akaunti au kuifunga wakati wowote kupitia mipangilio ya Akaunti yako ya Google.

Algoriti

Mchakato au taratibu zinazofuatwa na kompyuta kutatua matatizo.

Anwani ya IP

Kila kifaa kinachounganishwa kwenye Intaneti kimepangiwa namba inayojulikana kama anwani ya Itifaki ya Wavuti (IP). Kwa kawaida namba hizi hupangwa katika vikundi vya kijiografia. Mara nyingi anwani ya IP inaweza kutumiwa kutambua mahali ambako kifaa kinatumiwa kuunganisha kwenye Intaneti. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia maelezo ya mahali.

Hifadhi ya kivinjari cha wavuti

Hifadhi ya kivinjari huwezesha tovuti kuhifadhi data katika kivinjari kwenye kifaa. Unapoitumia katika hali ya "hifadhi ya ndani", inakuwezesha kuhifadhi data katika vipindi vyote. Hii inakuwezesha kupata data hata baada ya kufunga na kufungua upya kivinjari. Teknolojia moja ambayo inawezesha kuhifadhi kwenye wavuti ni HTML 5.

Hifadhi ya ndani ya data ya programu

Hifadhi ya ndani ya data ya programu ni hifadhi ya data kwenye kifaa. Inaweza, kwa mfano, kuwezesha programu ya wavuti kuendeshwa bila muunganisho wa intaneti na kuboresha utendaji wa programu kwa kuwezesha upakiaji wa haraka wa maudhui.

Kifaa

Kifaa ni kompyuta ambayo inaweza kutumika ili kufikia huduma za Google. Kwa mfano, kompyuta za mezani, kompyuta kibao, spika mahiri na simu mahiri, zote zinachukuliwa kuwa vifaa.

Kumbukumbu za seva

Kama tovuti mingi, seva zetu hurekodi maombi ya ukurasa yanayofanywa unapotembelea tovuti zetu kiotomatiki. “Kumbukumbu za seva” kwa kawaida hujumuisha ombi lako la wavuti, anwani ya IP, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na wakati wa ombi lako na moja au zaidi ya vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari chako kipekee.

Huu ni mfano wa kumbukumbu ambapo utafutaji ni wa “magari”:

123.45.67.89 - 25/Mar/2003 10:15:32 -
http://www.google.com/search?q=cars -
Chrome 112; OS X 10.15.7 -
740674ce2123e969
  • 123.45.67.89 ni anwani ya IP inayotolewa kwa mtumiaji na mtoa huduma za intaneti. Kulingana na huduma ya mtumiaji, anwani tofauti inaweza kutolewa kwa mtumiaji na mtoa huduma wake kila wakati anapounganisha kwenye Intaneti.
  • 25/Mar/2003 10:15:32 ndiyo tarehe na saa ya hoja.
  • http://www.google.com/search?q=cars ndiyo URL iliyoombwa, ikiwemo hoja ya utafutaji.
  • Chrome 112; OS X 10.15.7 ndicho kivinjari na mfumo wa uendeshaji unaotumika.
  • 740674ce2123a969 ndicho kitambulisho cha kipekee cha kidakuzi kilichotolewa kwa kompyuta hii mara ya kwanza ilipotumika kutembelea Google. (Vidakuzi vinaweza kufutwa na watumiaji. Ikiwa mtumiaji amefuta kidakuzi kwenye kompyuta kutoka wakati wa mwisho alipotembelea Google, kitambulisho cha kipekee cha kidakuzi kitatolewa kwa mtumiaji atakapotembelea Google tena akitumia kompyuta hiyo).

Lebo ya Pixeli

Lebo ya pikseli ni aina ya teknolojia inayowekwa kwenye tovuti au katika kiini cha barua pepe kwa lengo la kufuatilia shughuli fulani kwenye tovuti, kama vile tovuti inapotembelewa au barua pepe zinapofunguliwa. Lebo za pikseli kwa kawaida hutumiwa pamoja na vidakuzi.

Maelezo nyeti ya kibinafsi

Hii ni aina mahususi ya maelezo ya binafsi yanayohusiana na maelezo ya siri ya afya, asili ya mbari au kabila, imani za kisiasa au dini au mwelekeo wa jinsia.

Maelezo ya kibinafsi

Haya ni maelezo ambayo unatupa yanayokutambulisha binafsi, kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, au maelezo ya malipo, au data nyingine ambayo inaweza kuhusishwa kwa kawaida na maelezo kama hayo na Google, kama vile maelezo tunayohusisha na Akaunti yako ya Google.

Maelezo yasiyotambulisha kibinafsi

Haya ni maelezo yanayorekodiwa kuhusu watumiaji ili yasionyeshe wala kurejelea tena mtumiaji binafsi anayetambulika.

URL Iliyoelekeza

URL Iliyoelekeza (Uniform Resource Locator) ni maelezo yanayowasilishwa na kivinjari kwenye ukurasa lengwa wa wavuti, kwa kawaida unapobofya kiungo cha ukurasa huo. URL Iliyoelekeza ina URL ya ukurasa wa mwisho wa wavuti uliovinjari.

Vidakuzi

Kidakuzi ni faili ndogo iliyo na msururu wa herufi inayotumwa kwenye kompyuta yako unapotembelea tovuti fulani. Unapotembelea tovuti tena, kidakuzi kinaruhusu tovuti hiyo kutambua kivinjari chako. Vidakuzi vinaweza kuhifadhi mapendeleo ya mtumiaji na maelezo mengine. Unaweza kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili kisitumie vidakuzi au kikuarifu kidakuzi kinapotumwa. Hata hivyo, vipengee vingine vya tovuti au huduma huenda visifanye kazi vizuri bila vidakuzi. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia vidakuzi na data, vikiwemo vidakuzi, unapotumia tovuti au programu za washirika wetu.

Vitambulishaji vya kipekee

Kitambulishaji cha kipekee ni mfuatano wa herufi ambao unaweza kutumika kutambua kivinjari, programu au kifaa maalum. Vitambulishaji tofauti hutofautiana kulingana na muda vinaodumu, ikiwa vinaweza kubadilishwa na mtumiaji na jinsi vinavyoweza kufikiwa.

Vitambulishaji vya kipekee vinaweza kutumika kwa madhumuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na usalama na ugunduaji ulaghai, kusawazisha huduma kama vile barua pepe zako, kukumbuka mapendeleo yako na kukuonyesha matangazo yanayokufaa. Kwa mfano, vitambulishaji vya kipekee vilivyohifadhiwa kwenye vidakuzi vinasaidia tovuti unayovinjari kuonyesha maudhui katika lugha unayopendelea. Unaweza kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili kisitumie vidakuzi au kikuarifu kidakuzi kinapotumwa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia vidakuzi.

Kwenye mifumo mingine kando na vivinjari, vitambulishaji vya kipekee hutumika kutambua kifaa au programu maalum kwenye kifaa hicho. Kwa mfano, kitambulishaji cha kipekee kama vile Kitambulisho cha kifaa kwa ajili ya Matangazo hutumika kutoa matangazo yanayofaa kwenye vifaa vya Android na kinaweza kudhibitiwa kwenye mipangilio ya kifaa chako. Vitambulishaji vya kipekee vinaweza pia kujumuishwa kwenye kifaa na mtengenezaji (wakati mwingine huitwa kitambulisho cha kipekee ulimwenguni au UUID), kama vile nambari ya IMEI ya simu ya mkononi. Kwa mfano, kitambulisho cha kipekee cha kifaa kinaweza kutumika kukupa huduma zinazokufaa au kukagua matatizo ya kifaa yanayohusiana na huduma zetu.

Washirika

Mshirika ni kampuni ambayo ipo kwenye kundi la kampuni za Google, zikiwemo kampuni zifuatazo zinazotoa huduma za watumiaji katika Umoja wa Ulaya: Google Ireland Limited, Google Commerce Ltd, Google Payment Corp na Google Dialer Inc. Pata maelezo zaidi kuhusu kampuni zinazotoa huduma za biashara katika Umoja wa Ulaya.

Muktadha wa Ziada

aina nyeti

Tunapokuonyesha matangazo yanayokufaa, tunatumia mada ambazo tunadhania zinaweza kukuvutia kulingana na shughuli zako. Kwa mfano, unaweza kuona matangazo ya vitu kama vile "Kupika na Mapishi" au "Usafiri wa Ndege.” Huwa hatutumii mada au kuonyesha matangazo yanayokufaa kulingana na aina nyeti kama vile rangi, dini, mwelekeo wa kingono au afya. Na huwa tunahitaji kuona hivyo kutoka kwa watangazaji wanaotumia huduma zetu.

Data ya sensa kutoka kwenye kifaa chako

Huenda kifaa chako kina vitambuzi vinavyoweza kutumiwa kuelewa vyema mahali uliko na unakoenda. Kwa mfano, kipima mchapuko kinaweza kutumiwa kubaini kasi yako na gurudumu tuzi kubaini mweleko wa safari yako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia maelezo ya mahali.

huduma mahususi za Google

Kwa mfano, unaweza kufuta blogu yako kwenye Blogger au tovuti ya Google unayomiliki kwenye Tovuti za Google. Pia unaweza kufuta maoni ulioacha kwenye programu, michezo na maudhui mengine katika Duka la Google Play.

huduma za kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe

Mifano ya huduma hizi inajumuisha:

  • Google Voice, kwa ajili ya kupiga na kupokea simu, kutuma SMS na kudhibiti ujumbe wa sauti
  • Google Meet, kwa ajili ya kupiga na kupokea simu za video
  • Gmail, kwa ajili ya kutuma na kupokea barua pepe
  • Google Chat, kwa ajili ya kutuma na kupokea ujumbe
  • Google Duo, kwa ajili ya kupiga na kupokea simu za video na kutuma na kupokea ujumbe
  • Google Fi, kwa mpango wa simu

huduma za kutangaza na utafiti kwa niaba yao

Kwa mfano, wauzaji wanaweza kupakia data kutoka kwenye mipango yao ya kadi ya kutuza uaminifu ili wajumuishe maelezo ya uaminifu katika matokeo ya utafutaji au ununuzi, au kuelewa vyema utendaji wa kampeni zao za utangazaji. Tunatoa tu ripoti zilizojumlishwa kwa watangazaji, ambazo hazifichui maelezo kuhusu watu mahususi.

Google Analytics hutegemea vidakuzi vya mtu wa kwanza, kumaanisha kuwa vidakuzi vimewekwa na mteja wa Google Analytics. Kwa kutumia mifumo yetu, data inayozalishwa kupitia Uchanganuzi wa Google inaweza kuunganishwa na mteja wa Google Analytics na Google kwenye vidakuzi vya wahusika wengine ambavyo vinahusiana na matembeleo ya tovuti nyingine. Kwa mfano, mtangazaji anaweza kutaka kutumia data yake ya Google Analytics ili kuunda matangazo muhimu zaidi, au kuchanganua trafiki yake zaidi. Pata maelezo zaidi

hutegemea vidakuzi ili kufanya kazi vizuri

Kwa mfano, tunatumia kidakuzi kinachoitwa 'Ibcs' ambacho kinakuwezesha kufungua Hati nyingi za Google katika kivinjari kimoja. Kuzuia kidakuzi hiki kunaweza kuzuia Hati za Google kufanya kazi inavyotakikana. Pata maelezo zaidi

iliyosawazisha na Akaunti yako ya Google

Historia yako ya kuvinjari kwenye Chrome inahifadhiwa tu kwenye akaunti yako ikiwa umeruhusu usawazishaji wa Chrome na Akaunti yako ya Google. Pata maelezo zaidi

Kifaa cha Android kilicho na programu za Google

Vifaa vya Android vilivyo na programu za Google ni pamoja na vifaa vinavyouzwa na Google au na mmojawapo wa washirika wetu na inajumuisha simu, kamera, magari, vifaa vya kuvaliwa na runinga. Vifaa hivi hutumia Huduma za Google Play na programu ambazo zilisanikishwa awali ambazo ni pamoja na huduma kama vile Gmail, Ramani, kamera ya simu yako na kipiga simu, ubadilishaji wa maandishi kwenda usemi, kibodi na vipengele vya ulinzi. Pata maelezo zaidi kuhusu Huduma za Google Play.

kuboresha

Kwa mfano, tunatumia vidakuzi ili kuchanganua jinsi watu wanavyotumia huduma zetu. Na uchanganuzi huo unaweza kutusaidia kutengeneza bidhaa bora. Kwa mfano, unaweza kutusaidia kugundua kwamba inachukua watu muda mrefu kukamilisha kazi fulani au wanatatizika kabisa kumaliza hatua. Hivyo tunaweza kuunda tena kipengele hicho na kuboresha bidhaa kwa kila mtu.

kuhakikisha kuwa huduma zetu zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa

Kwa mfano, sisi huendelea kufuatilia mifumo yetu ili tutatue matatizo. Na tukipata hitilafu kwenye kipengele mahususi, kukagua maelezo ya shughuli yaliyokusanywa kabla ya tatizo kuanza, hutusaidia kutatua matatizo kwa haraka zaidi.

kuhakikisha na kuboresha

Kwa mfano, tunachanganua jinsi watu wanavyotumia utangazaji kuboresha utendaji wa matangazo yetu.

kulinda dhidi ya matumizi mabaya

Kwa mfano, maelezo kuhusu vitisho vya usalama yanaweza kutusaidia kukuarifu ikiwa tunadhani akaunti yako imeathiriwa (ambapo kutoka hapo tunaweza kukusaidia kuchukua hatua za kulinda akaunti yako).

Watu wengi wakianza kutafuta kitu, shughuli hizo zinaweza kutoa maelezo muhimu kuhusu mitindo maalum wakati huo. Google Trends hukusanya utafutaji kwenye wavuti katika Google ili kukadiria umaarufu wa utafutaji uliofanywa katika kipindi fulani na hushiriki matokeo hayo hadharani kwa kijumla. Pata maelezo zaidi

kushirikiana na Google

Kuna tovuti na programu zaidi ya milioni 2 zisizo za Google zinazoshirikiana na Google kuonyesha matangazo. Pata maelezo zaidi

kutambua matumizi mabaya

Tunapotambua taka, programu hasidi, maudhui yasiyo halali (ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa watoto kingono na nyenzo za unyanyasaji) na matumizi mengine mabaya kwenye mifumo yetu, yanayokiuka sera zetu, tunaweza kufunga akaunti yako au kuchukua hatua nyingine inayofaa. Katika hali fulani, tunaweza pia kuripoti ukiukaji huu kwa mamlaka inayofaa.

kutumia maelezo tunayokusanya kwenye huduma zetu

Kulingana na mipangilio yako, baadhi ya mifano ya jinsi tunavyotumia maelezo tunayokusanya kwenye huduma zetu ni pamoja na:

  • Wakati umeingia katika Akaunti yako ya Google na kutafuta kwenye Google, unaweza kuona matokeo ya utafutaji kutoka kwenye wavuti wa umma, pamoja na maelezo yanayohusiana kutoka kwenye maudhui uliyo nayo katika bidhaa nyingine za Google, kama vile Gmail au Kalenda ya Google. Hii inaweza kujumuisha vitu kama vile hali ya safari zako zijazo za ndege, mkahawa na kuweka nafasi za hoteli au picha zako. Pata maelezo zaidi
  • Ikiwa umewasiliana na mtu kupitia Gmail na unataka kumwongeza kwenye Hati za Google au tukio katika Kalenda ya Google. Google inarahisisha kufanya hivyo kwa kukamilisha anwani yake ya barua pepe kiotomatiki unapoanza kuandika jina lake. Kipengee hiki hurahisisha kushiriki vitu na watu unaowajua. Pata maelezo zaidi
  • Programu ya Google inaweza kutumia data uliyohifadhi katika bidhaa zingine za Google ili kukuonyesha maudhui yaliyowekewa mapendeleo, kulingana na mipangilio yako. Kwa mfano, ukiwa na utafutaji uliohifadhiwa katika Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu, programu ya Google inaweza kukuonyesha makala ya habari na maelezo mengine kuhusu mambo yanayokuvutia, kama vile matokeo ya spoti, kulingana na shughuli zako.
  • Ukiunganisha Akaunti yako ya Google kwenye Google Home, unaweza kudhibiti maelezo yako na kukamilisha shughuli kupitia programu ya Mratibu wa Google. Kwa mfano, unaweza kuweka matukio kwenye Kalenda yako ya Google au upate ratiba ya siku yako, uombe taarifa za hali ya safari yako ya ndege ijayo au utume maelezo kama vile maelekezo ya safari kwa gari kwenye simu yako. Pata maelezo zaidi
  • Ikiwa wewe ni mtumiaji unayeishi katika Umoja wa Ulaya, maamuzi unayofanya kuhusu uunganishaji wa huduma yataathiri jinsi huduma fulani za Google zinavyoweza kutumia data kwenye huduma zetu.

kuwasilisha huduma zetu

Mifano ya jinsi tunavyotumia maelezo yako ili kuwasilisha huduma zetu ni pamoja na:

  • Tunatumia anwani ya IP ya kifaa chako ili tukutumie data uliyoomba kama vile kupakia video ya YouTube
  • Tunatumia vitambulishaji vya kipekee vilivyohifadhiwa katika vidakuzi kwenye kifaa chako ili kutusaidia kukuthibitisha kuwa mtu anayeweza kufikia Akaunti yako ya Google
  • Picha na video unazopakia katika programu ya Picha kwenye Google hutumiwa kukusaidia kubuni albamu, kolagi na kazi nyingine unazoweza kushiriki. Pata maelezo zaidi
  • Barua pepe unayopokea ya kuthibitisha usafiri wa ndege inaweza kutumiwa kuunda kitufe cha kuripoti kuwa umefika ambacho huonekana katika Gmail yako.
  • Unapolipia huduma au bidhaa halisi kutoka kwetu, huenda ukatoa maelezo kama vile anwani yako ya mahali bidhaa zitakapopelekwa au maagizo ya usafirishaji bidhaa. Tunatumia maelezo haya kwa madhumuni kama vile kuchakata, kutekeleza na kusafirisha bidhaa unazoagiza na kutoa usaidizi kuhusu huduma au bidhaa unazonunua.

maelezo kama hayo yanayohusiana na afya yako ya mwili au akili

Ukitumia bidhaa na programu za siha tunazotoa, kama vile Fitbit, Pixel Watch, Nest au Google Fit, huwa tunakusanya data unayotoa, kama vile kimo na uzani wako. Pia tunakusanya maelezo kutoka programu na vifaa hivi, kama vile mitindo yako ya kulala, mapigo ya moyo, halijoto ya ngozi, kiasi cha kalori ulizotumia na idadi ya hatua ulizotembea.

maelezo kuhusu vitu vilivyo karibu na kifaa chako

Ikiwa unatumia Huduma za Mahali za Google kwenye Android, tunaweza kuboresha utendaji wa programu zinazotegemea mahali ulipo, kama vile Ramani za Google. Ikiwa unatumia Huduma za Mahali za Google, kifaa chako hutuma maelezo kwa Google kuhusu mahali kilipo, sensa (kama vile kipima mchapuko) na minara ya mitandao iliyo karibu na maeneo ya kufikia Wi-Fi (kama vile anwani ya MAC na uthabiti wa mawimbi). Vitu hivi vyote husaidia kubainisha mahali ulipo. Unaweza kutumia mipangilio ya kifaa chako ili kuwasha huduma za Mahali za Google. Pata maelezo zaidi

maelezo ya malipo

Kwa mfano, ikiwa utaongeza kadi yako ya mikopo au njia nyingine ya kulipa kwenye akaunti yako ya Google, unaweza kuitumia kununua bidhaa katika huduma zetu zote, kama vile programu katika Duka la Google Play. Pia, tunaweza kukuomba utupe maelezo mengine, kama vile nambari ya ushuru ya biashara ili itusaidie kuchakata malipo yako. Katika hali nyingine, pia tunaweza kuhitaji kuthibitisha utambulisho wako na tunaweza kukuomba utupe maelezo ili tufanye hivyo.

Pia, tunaweza kutumia maelezo ya malipo ili kuthibitisha kwamba unatimiza masharti ya umri, ikiwa kwa mfano, utaandika tarehe ya kuzaliwa isiyo sahihi ambayo inaonyesha kwamba huna umri wa kutosha kuwa na Akaunti ya Google. Pata maelezo zaidi

Maeneo unayowekea lebo kama vile nyumbani na kazini

Unaweza kuchagua kuhifadhi maelezo ya maeneo muhimu katika Akaunti yako ya Google, kama vile nyumbani au kazini kwako. Ukiweka anwani zako za nyumbani au kazini, zinaweza kutumiwa kukusaidia kufanya mambo kwa urahisi zaidi, kama vile kupata maelekezo au matokeo ya maeneo yaliyo karibu na nyumbani au kazini na pia kupokea matangazo yanayokufaa zaidi.

Unaweza kubadilisha au kufuta anwani zako za nyumbani au kazini wakati wowote katika Akaunti yako ya Google.

matangazo ambayo utapata ni muhimu zaidi

Kwa mfano, ikiwa unatazama video kwenye YouTube kuhusu kuoka keki, unaweza kuona matangazo zaidi yanayohusiana na kuoka, unapovinjari wavuti. Pia, tunaweza kutumia anwani yako ya IP ili kukadiria mahali, ili tuweze kukuonyesha matangazo ya huduma ya karibu ya usafirishaji piza ukitafuta "piza." Pata maelezo zaidi kuhusu matangazo ya Google na sababu ya kuweza kuona matangazo maalum.

matangazo yanayokufaa

Pia unaweza kuona matangazo yanayokufaa kulingana na maelezo kutoka kwa mtangazaji. Kwa mfano, ikiwa umenunua kwenye tovuti ya mtangazaji, anaweza kutumia maelezo ya kuingia kwenye tovuti yake kukuonyeshe matangazo. Pata maelezo zaidi

Kwa mfano, wakati umeingia kwenye Akaunti yako ya Google na umewasha kidhibiti cha Shughuli za Wavuti na Programu, unaweza kupata matokeo yanayokufaa zaidi ya utafutaji kulingana na utafutaji na shughuli za awali kutoka kwenye huduma nyingine za Google. Unaweza kupata maelezo zaidi hapa. Pia, unaweza kupata matokeo ya utafutaji yaliyoboreshwa hata ukiwa umeondoka kwenye akaunti. Ikiwa hutaki kiwango hiki cha utafutaji ulioboreshwa, unaweza kutafuta na kuvinjari faraghani au uzime utafutaji unaokufaa ambao umeondolewa kwenye akaunti.

Kama kampuni nyingine za teknolojia na mawasiliano, Google hupokea maombi kutoka kwa serikali na mahakama duniani kote mara kwa mara ili kufumbua data ya mtumiaji. Kuheshimu faragha na usalama wa data inayohifadhi kwenye Google ndiyo kanuni tanayofuata tunapopokea maombi haya ya kisheria. Timu yetu ya sheria hukagua kila ombi, bila kubagua aina na mara nyingi sisi hukataa ombi linaloonekana kuwa pana sana au lisilofuatilia mchakato sahihi. Pata maelezo zaidi katika Ripoti yetu ya Uwazi.

nambari ya simu

Ikiwa utaongeza nambari yako ya simu kwenye akaunti yako, inaweza kutumika kwa madhumuni tofauti ya huduma zote za Google, kulingana na mipangilio yako. Kwa mfano, nambari yako ya simu inaweza kutumiwa ili ikusaidie kufikia akaunti yako iwapo utasahau nenosiri yako, kusaidia watu kukupata na kuunganika nawe na kufanya matangazo unayoyaona yakufae zaidi. Pata maelezo zaidi

seva duniani kote

Kwa mfano, tunasimamia vituo vya data vilivyo duniani kote ili kusaidia kufanya bidhaa zetu ziendelee kupatikana kwa ajili ya watumiaji bila kukoma.

Sheria za faragha za majimbo ya Marekani

Sheria hizi ni pamoja na:

  • Sheria ya California ya Ulinzi wa Faragha ya Watumiaji (CCPA);
  • Sheria ya Virginia ya Ulinzi wa Data ya Watumiaji (VCDPA);
  • Sheria ya Faragha ya Colorado (CPA);
  • Sheria ya Connecticut Inayohusu Faragha ya Data Binafsi na Ufuatiliaji wa Mtandaoni (CTDPA); na
  • Sheria ya Utah ya Faragha ya Watumiaji (UCPA)
  • Sheria ya Washington ya Afya Yangu Data Yangu (MHMD)
  • Mswada wa 370 wa Seneti ya Nevada

Shughuli kwenye Huduma za Google

Ikiwa umeingia katika Akaunti yako ya Google na umewasha kipengele cha Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu, data ya shughuli zako kwenye tovuti, programu na huduma za Google huenda ikahifadhiwa kwenye Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu katika akaunti yako. Baadhi ya shughuli zinaweza kujumuisha maelezo kuhusu eneo la jumla ambako ulikuwepo ulipokuwa ukitumia huduma ya Google. Unapotafuta kitu ukiwa kwenye eneo la jumla, utafutaji wako utahusisha eneo la angalau kilomita 3 mraba, au utapanuliwa ili eneo husika liwe na angalau watu 1,000. Hii husaidia kulinda faragha yako.

Wakati mwingine, maelezo ya maeneo ambako ulikuwepo ulipofanya utafutaji hapo awali huenda yakatumika kukadiria eneo sahihi kwa utafutaji wako. Kwa mfano, ukitafuta maduka ya kahawa ukiwa Chelsea, huenda Google ikakuonyesha matokeo ya Chelsea katika utafutaji wako wa baadaye.

Unaweza kuangalia na kudhibiti Historia ya Shughuli zako kwenye Wavuti na Programu katika ukurasa wa Shughuli Zangu.

shughuli zako kwenye programu au tovuti nyingine zinazotumia huduma zetu

Programu na tovuti zinazotumia huduma za Google kama vile matangazo na takwimu hututumia maelezo.

Maelezo haya hukusanywa bila kujali kivinjari au hali ya kuvinjari unayotumia. Kwa mfano, ingawa Hali fiche kwenye kivinjari cha Chrome inaweza kufanya historia yako ya kuvinjari kuwa faragha kwa wengine wanaotumia kifaa chako, programu na tovuti za wengine zinazotumia huduma zetu bado zinaweza kutuma maelezo kwa Google unapozitembelea.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu baadhi ya njia unazoweza kutumia kudhibiti maelezo yanayotumwa unapotembelea au kutumia programu na tovuti zinazotumia huduma za Google.

shughuli zako kwenye tovuti na programu nyingine

Shughuli hizi huenda zitokane na matumizi yako ya huduma za Google kama vile usawazishaji wa akaunti yako na Chrome au tovuti na programu zako unazotembelea ambazo zinashirikiana na Google. Tovuti na programu nyingi hushirikiana na Google kuboresha maudhui na huduma zao. Kwa mfano, tovuti inaweza kutumia huduma zetu za matangazo (kama vile AdSense) au zana za uchanganuzi (kama vile Google Analytics), au inaweza kupachika maudhui mengine (kama vile video kutoka YouTube). Huduma hizi huenda zikashiriki taarifa kuhusu shughuli zako na Google, na kulingana na mipangilio ya akaunti yako na bidhaa unazotumia (kwa mfano, mshirika anapotumia Google Analytics pamoja na huduma zetu za matangazo), data hii huenda ikahusishwa na maelezo yako ya binafsi.

Pata maelezo zaidi kuhusu namna Google hutumia data unapotumia tovuti au programu za washirika wetu.

Taarifa za sauti na matamshi

Kwa mfano, unaweza kuchagua iwapo ungependa Google ihifadhi rekodi ya sauti kwenye Akaunti yako ya Google unapotumia programu za Mratibu, Tafuta na Ramani za Google. Wakati kifaa chako kinatambua amri ya kuwasha kipengele cha sauti, kama vile “Ok Google,” Google hurekodi sauti na matamshi yako pamoja na sauti ya matukio yanayofanyika sekunde chache kabla ya kuwasha. Pata maelezo zaidi

umma

Kwa mfano, tunachakata maelezo kuhusu maombi ya kuondoa maudhui kwenye huduma zetu chini ya sera za Google za kuondoa maudhui au sheria zinazotumika ili kukagua ombi na kuhakikisha uwazi, kuboresha uwajibikaji na kuzuia matumizi mabaya na ulaghai katika mbinu hizi.

Unavyotazama na kutumia maudhui na matangazo

Kwa mfano tunakusanya maelezo kuhusu mara ulizotazama, pamoja na mawasiliano na matangazo ili tuweze kutoa ripoti za ujumlisho kwa watangazaji, kama vile kuwaambia iwapo tuliweka tangazo lao kwenye ukurasa na iwapo mtazamaji aliweza kuliona tangazo. Pia tunaweza kupima utumiaji mwingine, kama vile unavyosogeza kipanya chako juu ya tangazo au ikiwa unatumia ukurasa ambapo tangazo linaonekana.

usalama na kuaminika

Baadhi ya mifano ya jinsi tunavyotumia maelezo yako ili yatusaidie kuweka huduma zetu salama na za kuaminika ni pamoja na:

  • Kukusanya na kuchanganua anwani za IP na data ya vidakuzi ili kulinda dhidi ya matumizi mabaya ya kiotomatiki. Matumizi haya mabaya huchukua njia nyingi, kama vile kutuma taka kwa watumiaji wa Gmail, kuiba pesa kwa ulaghai kutoka kwa watangazaji kwa kubofya visivyo kwenye matangazo, au kukomesha maudhui kwa kuzindua uvamizi wa Distributed Denial of Service (DDoS).
  • Kipengele cha “shughuli za hivi punde za akaunti” katika Gmail kinaweza kukusaidia kujua ikiwa mtu aliingia katika akaunti yako ya barua pepe na wakati alifanya hivyo bila ufahamu wako. Kipengele hiki hukuonyesha maelezo kuhusu shughuli za hivi majuzi katika Gmail, kama vile anwani za IP ambazo zilifikia barua pepe yako, eneo linalohusiana, pamoja na wakati na tarehe. Pata maelezo zaidi

vifaa

Kwa mfano, tunaweza kutumia maelezo kutoka kwenye vifaa vyako ili yakusaidie kujua ni kifaa kipi ungependa kutumia kusakinisha programu au kutazama filamu unayonunua kutoka Google play. Pia tunatumia maelezo haya ili tusaidie kulinda akaunti yako.

vyanzo vinavyofikiwa na umma

Kwa mfano, tunaweza kukusanya taarifa zinazopatikana mtandaoni kwa umma au kutoka kwenye vyanzo vingine vya umma ili kusaidia kufunza miundo ya AI ya Google na kubuni bidhaa na vipengele kama vile Google Tafsiri, Programu za Gemini na uwezo wa AI ya Wingu. Au, iwapo maelezo ya biashara yako yanaonekana kwenye tovuti, tunaweza kuyaainisha na kuyaonyesha kwenye huduma za Google.

washirika mahususi

Kwa mfano, tunaruhusu wabunifu na watangazaji wa YouTube kufanya kazi na kampuni za vipimo ili kupata maelezo zaidi kuhusu watazamaji wa video au matangazo yao ya YouTube, kwa kutumia vidakuzi au teknolojia zinazofanana. Mfano mwingine ni wauzaji kwenye kurasa zetu za ununuzi, ambao hutumia vidakuzi kuelewa jinsi watu tofauti huona bidhaa zao kwenye ukurasa unaoorodhesha bidhaa. Pata maelezo zaidi kuhusu washirika hawa na jinsi wanavyotumia maelezo yako.

watu ambao ni muhimu kwako zaidi mtandaoni

Kwa mfano, unapocharaza anwani katika sehemu ya Kwa, Nakala kwa, au Nakala fiche kwa ya barua pepe unayoandika, Gmail itapendekeza anwani kutoka kwa watu unaowasiliana nao mara nyingi.

watu wengine

Kwa mfano, tunachakata maelezo yako ili turipoti takwimu za matumizi kwa wamiliki wa haki kuhusu vile maudhui yao yalivyotumika katika huduma zetu. Pia tunaweza kuchakata maelezo yako ikiwa watu watatafuta jina lako na tutaonyesha matokeo ya utafutaji kwa tovuti zilizo na maelezo yanayokuhusu ambayo yanapatikana kwa umma.

watumiaji wetu

Kwa mfano, ili kuzuia matumizi mabaya na kukuza uwazi na uwajibikaji kwenye desturi zetu za udhibiti wa maudhui mtandaoni, Google hushiriki data kuhusu maombi ya kuondoa maudhui kwenye huduma zetu kupitia Lumen, ambayo hukusanya na kuchanganua maombi haya ili kuwezesha utafiti wa kuwasaidia watumiaji wa Intaneti wafahamu haki zao. Pata maelezo zaidi.

Programu za Google
Menyu kuu