Matangazo

Matangazo hukuwezesha kutumia Google na tovuti na huduma nyingi unazotumia bila malipo. Sisi hutia bidii kuhakikisha kuwa matangazo ni salama, yasiyosumbua na yanakufaa zaidi iwezekanavyo. Kwa mfano, hutaona matangazo ibukizi kwenye Google na tunazifunga akaunti za mamia ya maelfu ya wachapishaji na watangazaji wanaokiuka sera zetu kila mwaka – pamoja na matangazo yaliyo na programu hasidi, matangazo ya bidhaa bandia au matangazo yanayojaribu kutumia vibaya maelezo yako ya kibinafsi.

Huduma za utangazaji za Google zinajaribu njia mpya za kuendeleza uwasilishaji na upimaji wa utangazaji dijitali kwa namna ambazo zitalinda vizuri faragha ya watu mtandaoni kupitia mradi wa Mazingira ya Faragha kwenye Chrome na Android. Watumiaji ambao wamewasha mipangilio husika ya Mazingira ya Faragha katika Chrome au Android wanaweza kuona matangazo husika kutoka kwenye huduma za utangazaji za Google kulingana na Mada au data ya Hadhira Inayolindwa iliyohifadhiwa kwenye kifaa cha mkononi au kivinjari chao. Huduma za utangazaji za Google zinaweza pia kupima utendaji wa matangazo kwa kutumia data ya Ripoti za Uhusishaji iliyohifadhiwa kwenye kifaa cha mkononi au kivinjari chao. Maelezo zaidi kuhusu Mazingira ya Faragha.

Jinsi Google hutumia vidakuzi katika matangazo

Vidakuzi husaidia kufanya matangazo kuwa bora zaidi. Bila vidakuzi, ni vigumu kwa mtangazaji kufikia hadhira yake au kujua ni matangazo mangapi yaliyoonyeshwa na ni mibofyo mingapi iliyopokewa.

Tovuti nyingi, kama vile tovuti za habari na blogu, hushirikiana na Google kuonyesha matangazo kwa wageni wao. Tukifanya kazi na washirika wetu, tunaweza kutumia vidakuzi kwa madhumuni kadhaa, kama vile kukusitisha kuona tangazo sawa tena na tena, kugundua na kusitisha udanganyifu wa kubofya, na kuonyesha matangazo ambayo yana uwezekano wa kuwa wa maana zaidi (kama vile matangazo yanayolingana na tovuti ulizotembelea).

Tunahifadhi rekodi ya matangazo tunayoyatoa katika kumbukumbu zetu. Kumbukumbu hizi za seva kwa kawaida hujumuisha ombi lako la wavuti, anwani ya IP, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na wakati wa ombi lako na moja au zaidi ya vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari chako kipekee. Tunahifadhi data hii kwa sababu kadhaa, ya muhimu kabisa ni kuboresha huduma zetu na kudumisha usalama wa mifumo yetu. Sisi huondoa utambulisho wa data hii ya kumbukumbu kwa kuondoa sehemu ya anwani ya IP (baada ya miezi 9) na maelezo ya kidakuzi (baada ya miezi 18).

Vidakuzi vyetu vya utangazaji

Ili kusaidia washirika wetu kudhibiti matangazo yao na tovuti, sisi hutoa bidhaa nyingi, ikiwa ni pamoja na AdSense, AdWords, Google Analytics, na huduma mbalimbali zilizochapishwa za DoubleClick. Unapotembelea ukurasa au kuona tangazo linalotumia moja ya bidhaa hizi, iwe kwenye huduma za Google au kwenye tovuti na programu zingine, huenda vidakuzi mbalimbali vikatumwa kwenye kivinjari chako.

Vidakuzi vinaweza kuwekwa kutoka vikoa kadhaa tofauti, ikiwa ni pamoja na google.com, doubleclick.net, googlesyndication.com, googleadservices.com, au vikoa vya tovuti za washirika wetu. Baadhi ya bidhaa zetu za utangazaji huwezesha washirika wetu kutumia huduma nyingine kwa kushirikiana na bidhaa zetu (kama vile kipimo cha tangazo na huduma ya kuripoti) na huduma hizi zinaweza kutuma vidakuzi vyake kwenye kivinjari chako. Vidakuzi hivi vitawekwa kutoka vikoa vyao.

Tazama maelezo zaidi kuhusu aina za vidakuzi vinavyotumiwa na Google na washirika wetu, na jinsi tunavyovitumia.

Jinsi unavyoweza kudhibiti vidakuzi vya utangazaji

Unaweza kutumia mipangilio ya matangazo kudhibiti matangazo ya Google unayoona na kuzima matangazo yaliyowekewa mapendeleo. Hata ukizima matangazo yaliyowekewa mapendeleo, huenda bado ukaona matangazo kulingana na vigezo kama vile mahali uliko kwa jumla kutokana na Anwani yako ya IP, aina ya kivinjari chako na hoja zako za utafutaji.

Unaweza pia kudhibiti vidakuzi vya kampuni nyingi vinavyotumiwa kwa utangazaji wa mtandaoni kupitia zana za chaguo za wateja chini ya programu za kujidhibiti katika nchi nyingi, kama vile ukurasa wa nchini Marekani unaoitwa aboutads.info choices au programu ya Ulaya inayoitwa Your Online Choices.

Hatimaye, unaweza kudhibiti vidakuzi katika kivinjari chako .

Teknolojia zingine zinazotumika katika utangazaji

Mifumo ya Google ya utangazaji inaweza kutumia teknolojia zingine, ikiwa ni pamoja na Flash na HTML5, kwa utendakazi kama uonyeshaji wa maumbizo ya kuingiliana ya matangazo. Tunaweza kutumia anwani ya IP, kwa mfano, ili kutambua eneo lako kwa jumla. Pia tunaweza kuchagua utangazaji kulingana na maelezo kuhusu kompyuta au kifaa chako, kama vile muundo wa kifaa chako, aina ya kivinjari, au kitambuzi katika kifaa chako kama kipima uchapuzi.

Eneo

Bidhaa za matangazo ya Google zinaweza kupokea au kutambua maelezo kuhusu mahali ulipo kutoka vyanzo tofauti. Kwa mfano, tunaweza kutumia anwani ya IP kutambua mahali pa jumla ulipo; tunaweza kupokea mahali sahihi ulipo kutoka kifaa chako cha mkononi. Tunaweza kukisia mahali ulipo kutokana na hoja ulizotafuta; na tovuti au programu ambazo unatumia zinaweza kututumia maelezo kuhusu mahali ulipo. Google hutumia maelezo ya mahali katika bidhaa zake za matangazo kutambua maelezo ya kidemografia ili kuboresha umuhimu wa matangazo unayoona, kutathmini utendaji wa tangazo na kuripoti kuhusu takwimu za jumla kwa watangazaji.

Vitambulishaji vya utangazaji vya programu za vifaa vya mkononi

Kutoa matangazo katika huduma ambazo teknolojia ya vidakuzi huenda haipatikani (kwa mfano, katika programu za vifaa vya mkononi), tunaweza kutumia teknolojia zinazotekeleza kazi sawa na vidakuzi. Wakati mwingine, Google huunganisha kitambulishi kinachotumika kutangaza kwenye programu za vifaa vya mkononi kwenye kidakuzi cha matangazo kwenye kifaa sawa ili kuratibu matangazo kwenye programu zote za kifaa chako cha mkononi na kivinjari cha kifaa chako. Kwa mfano, hili linaweza kutokea unapoona tangazo kwenye programu inayofungua ukurasa wa wavuti katika kivinjari cha kifaa chako cha mkononi. Hii pia hutusaidia kuimarisha ripoti tunazotoa kwa watangazaji wetu kuhusu ufanisi wa kampeni zao.

Matangazo unayoona kwenye kifaa chako yanaweza kuwekewa mapendeleo kulingana na Kitambulisho cha Matangazo cha kifaa hicho. Kwenye vifaa vya Android, unaweza:

 • Kubadilisha kitambulisho cha matangazo cha kifaa chako, hatua ambayo hubadilisha kitambulisho cha sasa na kuweka kipya. Bado programu zinaweza kukuonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo, lakini huenda matangazo hayo yasikufae au kukuvutia kwa muda.
 • Kufuta kitambulisho cha matangazo cha kifaa chako, hatua inayofuta kitambulisho cha matangazo na haiweki kitambulisho kipya. Bado programu zinaweza kukuonyesha matangazo, lakini huenda matangazo hayo yasikufae au kukuvutia. Hutaona matangazo yanayolingana na kitambulisho hiki cha matangazo, lakini huenda bado ukaona matangazo yanayolingana na vigezo vingine, kama vile maelezo ambayo umeshiriki na programu.

Ili ufanye mabadiliko kwenye kitambulisho cha matangazo katika kifaa chako cha Android, fuata maagizo yaliyo hapa chini.

Android

Kubadilisha kitambulisho cha matangazo cha kifaa chako

Ili ubadilishe kitambulisho cha matangazo cha kifaa chako:

 1. Kwenye kifaa chako cha Android, nenda kwenye Mipangilio.
 2. Gusa Faragha > Matangazo.
 3. Gusa Badilisha kitambulisho cha matangazo kisha uthibitishe mabadiliko uliyofanya.
Kufuta kitambulisho cha matangazo cha kifaa chako

Ili ufute kitambulisho cha matangazo cha kifaa chako:

 1. Kwenye kifaa chako cha Android, nenda kwenye Mipangilio.
 2. Gusa Faragha > Matangazo.
 3. Gusa Futa kitambulisho cha matangazo kisha uthibitishe mabadiliko uliyofanya.

Kitambulisho chako cha matangazo kitabadilishwa au kufutwa, lakini huenda programu zikawa na mipangilio yake kwa kutumia aina nyingine za vitambulishi, hali ambayo inaweza pia kuathiri aina za matangazo unayoona.

Kwenye baadhi ya matoleo ya zamani ya Android

Iwapo toleo la Android la kifaa chako ni 4.4 au la zamani:

 1. Fungua Mipangilio
 2. Gusa Faragha > Mipangilio ya Kina > Matangazo
 3. Washa Jiondoe kwenye Mipangilio ya Kuweka Mapendeleo ya Matangazo kisha uthibitishe mabadiliko uliyofanya.

iOS

Vifaa vyenye iOS hutumia Kitambulishi cha Utangazaji cha Apple. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu uamuzi wako wa kutumia kitambulishi hiki, tembelea programu ya Mipangilio kwenye kifaa chako.

Televisheni Iliyounganishwa au Uuzaji wa Moja kwa Moja

Vitambulishi vya matangazo vya televisheni iliyounganishwa

Televisheni zilizounganishwa ni sehemu nyingine ambapo teknolojia ya vidakuzi haipatikani; badala yake, Google itategemea vitambulishi vilivyo kwenye kifaa vilivyobuniwa vitumiwe katika utangazaji ili kuonyesha matangazo. Vifaa vingi vya televisheni iliyounganishwa hutumia kitambulishi cha utangazaji ambacho kinafanana katika utendaji na vitambulishi vya vifaa vya mkononi. Vitambulishi hivi hubuniwa ili kuwapa watumiaji chaguo la kuvibadilisha au kujiondoa kabisa kwenye utangazaji uliowekewa mapendeleo.

Mipangilio ifuatayo ya “Matangazo” inapatikana kwenye televisheni zilizo na lugha ifuatayo kila wakati:

 • Badilisha kitambulisho cha matangazo
 • Futa kitambulisho cha matangazo
 • Jiondoe kwenye mipangilio ya Kuweka Mapendeleo ya Matangazo (washa au uzime)
 • Matangazo kutoka Google (viungo vinavyoelekeza kwenye sehemu ya Kuhusu kuweka mapendeleo ya matangazo kwenye Google)
 • Kitambulisho chako cha matangazo (mfuatano mrefu)

Mipangilio hii ya Matangazo inapatikana katika njia zifuatazo kwenye Google TV na Android TV mtawalia.

Google TV

Njia isiyobadilika ya Matangazo:

 1. Mipangilio
 2. Faragha
 3. Matangazo

Android TV

Mipangilio ya matangazo huonekana katika mojawapo ya njia mbili za jumla kwenye Android TV kulingana na mtengenezaji au muundo wa TV. Katika Android TV, washirika wana uhuru wa kutumia wapendavyo njia ya Mipangilio. Mshirika ataamua njia ambayo angependa kutumia itakayofaa zaidi hali yake maalum ya TV lakini zifuatazo ni njia za kawaida za Mipangilio ya matangazo.

Njia ya A:

 1. Mipangilio
 2. Kuhusu
 3. Maelezo ya Kisheria
 4. Matangazo

Njia ya B:

 1. Mipangilio
 2. Mapendeleo ya Vifaa
 3. Kuhusu
 4. Maelezo ya Kisheria
 5. Matangazo
Vifaa Visivyo vya Google

Vifaa vingi vya televisheni zilizounganishwa hutumia vitambulishi vya utangazaji na hutoa mbinu za watumiaji kujiondoa kwenye utangazaji uliowekewa mapendeleo. Orodha kamili ya vifaa hivyo na njia ambazo watumiaji wanaweza kujiondoa, husasishwa kwenye tovuti ya Mpango wa Utangazaji wa Mtandao hapa: https://thenai.org/opt-out/connected-tv-choices/.

Je, ni nini kinachoamua matangazo ambayo ninaona ya Google?

Maamuzi mengi hufanywa ili kuamua ni tangazo lipi unaloona.

Wakati mwingine tangazo unaloliona linalingana na mahali ulipo sasa au ulipokuwa awali. Kwa kawaida, anwani yako ya IP ni ishara nzuri ya ukadiriaji wa eneo ulipo. Kwa hivyo huenda ukaona tangazo kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube.com linalotangaza filamu inayopangiwa kutolewa hivi karibuni nchini mwako, au utafutaji wa "piza" unaweza kukupa matokeo ya mikahawa ya piza mjini mwako.

Wakati mwingine tangazo unaloona linalingana na muktadha wa ukurasa. Ikiwa unatazama ukurasa wa vidokezo vya kilimo cha bustani, unaweza kuona matangazo ya vifaa vya kilimo cha bustani.

Wakati mwingine unaweza kuona tangazo kwenye wavuti kulingana na shughuli zako za programu, au shughuli kwenye huduma za Google; tangazo kwenye programu kulingana na shughuli zako kwenye wavuti; au tangazo kulingana na shughuli zako kwenye kifaa kingine.

Wakati mwingine tangazo unaloona kwenye ukurasa linatolewa na Google lakini limechaguliwa na kampuni nyingine. Kwa mfano, unaweza kuwa umejisajili na tovuti ya gazeti. Kutoka kwa maelezo ambayo umetoa kwa gazeti, inaweza kutoa uamuzi kuhusu ni matangazo yapi ya kukuonyesha, na inaweza kutumia bidhaa za Google za kutoa matangazo ili kuwasilisha matangazo hayo.

Pia unaweza kuona matangazo kwenye bidhaa na huduma za Google, ikiwa ni pamoja na Huduma ya Tafuta na Google, Gmail, na YouTube, kulingana na maelezo kama vile anwani yako ya barua pepe uliyowapa watangazaji na baadaye watangazaji wakaishiriki na Google.

Je, kwa nini ninaona matangazo ya Google kwa bidhaa ambazo nimetazama?

Unaweza kuona matangazo ya bidhaa ulizotazama awali. Kwa mfano tuchukulie umetembelea tovuti ambayo inauza vifaa vya gofu, lakini hununui vifaa hivyo katika ziara yako ya kwanza. Mmiliki wa tovuti anaweza kuamua kukuhimiza urejee na ukamilishe ununuzi wako. Google hutoa huduma ambazo huwaruhusu waendeshaji wavuti kuelekeza matangazo yao kwa watu ambao wametembelea kurasa zao.

Ili hatua hii ifanye kazi, Google husoma kidakuzi ambacho tayari kiko katika kivinjari chako au huhifadhi kidakuzi katika kivinjari chako unapotembelea tovuti hiyo ya gofu, (ikichukuliwa kwamba kivinjari chako huruhusu kuhifadhi vidakuzi).

Unapotembelea wavuti nyingine ambayo inafanya kazi na Google, ambayo haina chochote cha kufanya na gofu, unaweza kuona tangazo la vifaa hivyo vya gofu. Hiyo ni kwa sababu kivinjari chako hutumia Google kidakuzi hicho hicho. Kwa upande mwingine, tunaweza kutumia kidakuzi hicho kukupa tangazo ambalo linaweza kukuhimiza ununue vifaa hivyo vya gofu.

Tembeleo lako kwenye tovuti ya gofu pia linaweza kutumiwa na Google kukuonyesha matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia utakapotafuta vifaa vya gofu kwenye Google.

Tumeweka vikwazo kuhusu aina hii ya tangazo. Kwa mfano, tunawakataza watangazaji kuchagua hadhira kulingana na maelezo nyeti, kama vile maelezo kuhusu afya au imani za kidini.

Pata maelezo zaidi kuhusu matangazo ya Google.

Programu za Google
Menyu kuu