Jinsi Google inavyotumia vidakuzi

Ukurasa huu unafafanua aina za vidakuzi na teknolojia nyingine zinazotumiwa na Google. Unaelezea pia jinsi Google na washirika wetu hutumia vidakuzi katika utangazaji.

Vidakuzi ni vifungu vidogo vya maandishi yanayotumwa kwenye kivinjari chako na tovuti unayotembelea. Husaidia tovuti hiyo kukumbuka maelezo kuhusu ulikotembelea, hali inayoweza kurahisisha shughuli ya kutembelea tovuti tena na kufanya tovuti ikufae zaidi. Teknolojia nyingine, ikiwa ni pamoja na vitambulishi vya kipekee vinavyotumiwa kutambua kivinjari, programu au kifaa, pikseli na nafasi ya hifadhi, zinaweza pia kutumiwa kwa madhumuni haya. Vidakuzi na teknolojia nyingine kama zilivyofafanuliwa kote kwenye ukurasa huu zinaweza kutumiwa kwa madhumuni yaliyofafanuliwa hapa chini.

Angalia Sera ya Faragha ili upate maelezo kuhusu jinsi tunavyolinda faragha yako katika utumiaji wetu wa vidakuzi na maelezo mengine.

Aina za vidakuzi na teknolojia nyingine zinazotumiwa na Google

Baadhi ya vidakuzi au vidakuzi vyote au teknolojia nyingine zilizofafanuliwa hapa chini zinaweza kuhifadhiwa katika kivinjari, programu au kifaa chako. Ili udhibiti jinsi vidakuzi vinavyotumiwa, ikiwa ni pamoja na kukataa matumizi ya vidakuzi fulani, unaweza kutembelea g.co/privacytools. Unaweza pia kudhibiti vidakuzi kwenye kivinjari chako (ingawa huenda vivinjari vya vifaa vya mkononi visiwe na uonekanaji huu). Teknolojia nyingine zinazotumiwa kutambua programu na vifaa zinaweza kudhibitiwa katika mipangilio ya kifaa chako au katika mipangilio ya programu.

Utendaji

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazotumiwa katika utendaji hukuruhusu ufikie vipengele vya msingi vya huduma. Mambo yanayochukuliwa kuwa ya msingi kwa huduma yanajumuisha mapendeleo, kama vile lugha unayochagua, maelezo yanayohusiana na kipindi chako, kama vile maudhui ya kikapu cha ununuzi na maboresho ya bidhaa yanayosaidia kudumisha na kukuza huduma hiyo.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine hutumiwa kudumisha mapendeleo yako. Kwa mfano, watu wengi wanaotumia huduma za Google wana kidakuzi kinachoitwa ‘NID’ au ‘ENID’ katika vivinjari vyao, kulingana na chaguo zao za vidakuzi. Vidakuzi hivi hutumiwa kukumbuka mapendeleo yako na maelezo mengine, kama vile lugha unayopendelea, idadi ya matokeo ambayo ungependa yaonyeshwe kwenye ukurasa wa matokeo ya utafutaji (kwa mfano, 10 au 20) na iwapo ungependa kuwasha kichujio cha Utafutaji Salama kwenye Google. Muda wa kila kidakuzi cha ‘NID’ huisha baada ya miezi 6 kuanzia kinapotumiwa mara ya mwisho na mtumiaji. Kidakuzi cha ‘ENID’ hudumu kwa miezi 13. Vidakuzi vinavyoitwa ‘VISITOR_INFO1_LIVE’ na ‘YEC’ hufanya kazi sawa kwenye YouTube na pia hutumiwa kutambua na kutatua matatizo ya huduma. Vidakuzi hivi hudumu kwa miezi 6 na miezi 13, mtawalia.

Vidakuzi na teknolojia nyingine hutumiwa kudumisha na kuboresha hali yako ya utumiaji katika kipindi mahususi. Kwa mfano, YouTube hutumia kidakuzi cha ‘PREF’ kuhifadhi maelezo kama vile mipangilio ya ukurasa unaopendelea na mapendeleo ya uchezaji kama vile chaguo mahususi za kucheza kiotomatiki, kuchanganya maudhui na ukubwa wa kichezaji. Kwenye YouTube Music, mapendeleo haya yanajumuisha kiwango cha sauti, hali ya kujirudia na kucheza kiotomatiki. Muda wa kidakuzi hiki huisha baada ya miezi 8 kuanzia kinapotumiwa mara ya mwisho na mtumiaji. Kidakuzi cha ‘pm_sess’ pia husaidia kudumisha kipindi cha kivinjari na huduma kwa dakika 30.

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinaweza pia kutumiwa kuboresha utendaji wa huduma za Google. Kwa mfano, kidakuzi cha ‘CGIC’ huboresha utoaji wa matokeo ya utafutaji kwa kukamilisha kiotomatiki hoja za utafutaji kulingana na maudhui ambayo mtumiaji aliweka awali. Kidakuzi hiki hudumu kwa miezi 6.

Google hutumia kidakuzi cha ‘CONSENT’, ambacho huduma kwa miaka 2, ili kuhifadhi hali ya mtumiaji kuhusu chaguo zake za vidakuzi. Kidakuzi kingine, ‘SOCS’, hudumu kwa miezi 13 na pia hutumiwa kuhifadhi hali ya mtumiaji kuhusu chaguo zake za vidakuzi.

Usalama

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazotumiwa kwa ajili ya usalama husaidia kuthibitisha watumiaji, kuzuia ulaghai na kukulinda unapotumia huduma fulani.

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazotumiwa kuthibitisha watumiaji husaidia kuhakikisha kuwa mmiliki halisi wa akaunti ndiye tu anayeweza kufikia akaunti hiyo. Kwa mfano, vidakuzi vinavyoitwa ‘SID’ na ‘HSID’ huwa na rekodi zilizotiwa saini dijitali na zilizosimbwa kwa njia fiche, za kitambulisho cha Akaunti ya Google ya mtumiaji na muda wa hivi majuzi zaidi wa kuingia katika akaunti. Mseto wa vidakuzi hivi huruhusu Google kuzuia aina nyingi za mashambulizi, kama vile majaribio ya kuiba maudhui ya fomu zinazotumwa kwenye huduma za Google.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine hutumiwa kuzuia taka, ulaghai na matumizi mabaya. Kwa mfano, vidakuzi vya ‘pm_sess’, ‘YSC’, na ‘AEC’ huhakikisha kuwa maombi katika kipindi cha kuvinjari yanafanywa na mtumiaji, wala si tovuti nyingine. Vidakuzi hivi huzuia tovuti hasidi zisichukue hatua kwa niaba ya mtumiaji bila yeye kufahamu. Kidakuzi cha ‘pm_sess’ hudumu kwa dakika 30 na kidakuzi cha ‘AEC’ hudumu kwa miezi 6. Kidakuzi cha ‘YSC’ hudumu kwa kipindi ambacho mtumiaji anavinjari.

Takwimu

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazotumiwa kwa ajili ya takwimu husaidia kukusanya data inayoruhusu huduma kuelewa jinsi unavyotumia huduma mahususi. Maarifa haya huruhusu huduma kuboresha maudhui na kubuni vipengele bora zaidi vinavyoimarisha hali yako ya utumiaji.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine husaidia tovuti na programu kuelewa jinsi wageni wanavyotumia huduma zake. Kwa mfano, Google Analytics hutumia mseto wa vidakuzi kukusanya maelezo na kuripoti takwimu za matumizi ya tovuti bila kuwatambulisha wageni mahususi kwenye Google. ‘_ga’, ndicho kidakuzi kikuu kinachotumiwa na Google Analytics na huwezesha huduma kutofautisha mgeni mmoja na mwingine na hudumu kwa miaka 2. Tovuti yoyote inayotekeleza Google Analytics, ikiwa ni pamoja na huduma za Google, hutumia kidakuzi cha ‘_ga’. Kila kidakuzi cha ‘_ga’ ni mahususi kwenye kipengee mahususi, kwa hivyo hakiwezi kutumiwa kumfuatilia mtumiaji au kivinjari fulani kwenye tovuti zisizohusiana.

Huduma za Google pia hutumia vidakuzi vya ‘NID’ na ‘ENID’ kwenye huduma ya Tafuta na Google na vidakuzi vya ‘VISITOR_INFO1_LIVE’ na ‘YEC’ kwenye YouTube, kwa ajili ya takwimu.

Matangazo

Google hutumia vidakuzi katika utangazaji, ikiwa ni pamoja na kuonyesha na kutekeleza matangazo, kuweka mapendeleo kwenye matangazo (kulingana na mipangilio yako katika myadcenter.google.com na adssettings.google.com/partnerads), kudhibiti mara ambazo tangazo huonyeshwa kwa mtumiaji, kupuuza matangazo ambayo umechagua kuacha kuona na kupima ufaafu wa matangazo.

Kidakuzi cha ‘NID’ hutumiwa kuonyesha matangazo ya Google katika huduma za Google kwa watumiaji walioondoka katika akaunti, huku vidakuzi vya ‘ANID’ na ‘IDE’ hutumiwa kuonyesha matangazo ya Google kwenye tovuti zisizo za Google. Iwapo umewasha mipangilio ya matangazo yanayowekewa mapendeleo, kidakuzi cha ‘ANID’ hutumiwa kukumbuka mipangilio hii na hudumu kwa miezi 13 kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA), Uswizi na Uingereza (UK) na hudumu kwa miezi 24 kwingineko. Iwapo umezima matangazo yanayowekewa mapendeleo, kidakuzi cha ‘ANID’ hutumiwa kuhifadhi mipangilio hiyo hadi 2030. Muda wa kidakuzi cha ‘NID’ huisha miezi 6 kuanzia kinapotumiwa mara ya mwisho na mtumiaji. Kidakuzi cha ‘IDE’ hudumu kwa miezi 13 kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya, Uswizi na Uingereza (UK) na kwa miezi 24 kwingineko.

Kulingana na mipangilio yako ya matangazo, huduma nyingine za Google kama vile YouTube zinaweza pia kutumia vidakuzi na teknolojia hizi na nyingine, kama vile kidakuzi cha ‘VISITOR_INFO1_LIVE’, katika utangazaji.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine zinazotumiwa katika utangazaji ni za watumiaji wanaoingia katika akaunti ili kutumia huduma za Google. Kwa mfano, kidakuzi cha ‘DSID’ hutumiwa kumtambua mtumiaji ambaye ameingia katika akaunti kwenye tovuti zisizo za Google na kukumbuka iwapo mtumiaji amekubali kuweka mapendeleo ya matangazo. Hudumu kwa wiki 2.

Kupitia mfumo wa utangazaji wa Google, biashara zinaweza kutangaza kwenye huduma za Google na pia kwenye tovuti zisizo za Google. Baadhi ya vidakuzi huruhusu Google kuonyesha matangazo kwenye tovuti za wengine na huwekwa kwenye vikoa vya tovuti unazotembelea. Kwa mfano, kidakuzi cha ‘_gads’ huwezesha tovuti kuonyesha matangazo ya Google. Vidakuzi vinavyoanza kwa ‘_gac_’ hutoka kwenye Google Analytics na hutumiwa na watangazaji kupima shughuli za watumiaji na utendaji wa kampeni zao za utangazaji. Vidakuzi vya ‘_gads’ hudumu kwa miezi 13 na vidakuzi vya ‘_gac_’ hudumu kwa siku 90.

Baadhi ya vidakuzi na teknolojia nyingine hutumiwa kupima utendaji wa matangazo na kampeni na asilimia za walioshawishika kutokana na matangazo ya Google kwenye tovuti unayotembelea. Kwa mfano, vidakuzi vinavyoanza kwa ‘_gcl_’ hutumiwa kimsingi kuwasaidia watangazaji kubaini mara ambazo watumiaji wanaobofya matangazo yao hushawishika kuchukua hatua kwenye tovuti yao, kama vile kufanya ununuzi. Vidakuzi vinavyotumiwa kupima asilimia za walioshawishika havitumiwi kuweka mapendeleo kwenye matangazo. Vidakuzi vya ‘_gcl_’ hudumu kwa siku 90.

Angalia maelezo zaidi kuhusu vidakuzi vinavyotumiwa kwa utangazaji hapa.

Kuweka Mapendeleo

Vidakuzi na teknolojia nyingine zinazotumiwa kuweka mapendeleo huboresha hali yako ya utumiaji kwa kutoa maudhui na vipengele vilivyowekewa mapendeleo, kulingana na mipangilio yako katika g.co/privacytools au mipangilio ya programu na kifaa chako.

Vipengele na maudhui ambayo yamewekewa mapendeleo hujumuisha mambo kama vile matokeo na mapendekezo yanayofaa zaidi, ukurasa wa kwanza wa YouTube uliowekewa mapendeleo na matangazo yanayolenga mambo yanayokuvutia. Kwa mfano, kidakuzi cha ‘VISITOR_INFO1_LIVE’ kinaweza kuruhusu mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo kwenye YouTube kulingana na utazamaji na utafutaji wa awali. Na kidakuzi cha ‘NID’ huwezesha vipengele vilivyowekewa mapendeleo vya kukamilisha kiotomatiki katika huduma ya Tafuta unapoandika hoja za utafutaji. Muda wa vidakuzi hivi huisha miezi 6 kuanzia vinapotumiwa mara ya mwisho na mtumiaji. Kidakuzi kingine cha kuweka mapendeleo, ‘UULE’, hutuma maelezo sahihi ya mahali kutoka kwenye kivinjari chako hadi kwenye seva za Google ili Google iweze kukuonyesha matokeo yanayofaa mahali uliko. Matumizi ya kidakuzi hiki yanategemea mipangilio ya kivinjari chako na iwapo umechagua kuwasha mipangilio ya mahali kwenye kivinjari chako. Kidakuzi cha ‘UULE’ hudumu kwa hadi saa 6.

Maudhui na vipengele ambavyo havijawekewa mapendeleo ni tofauti na maudhui na vipengele vilivyowekewa mapendeleo kwa kuwa huathiriwa na mambo kama vile maudhui ambayo unaangalia sasa, utafutaji unaofanya sasa kwenye Google na mahali uliko kwa jumla.

Kudhibiti vidakuzi katika kivinjari chako

Vivinjari vingi hukuruhusu udhibiti jinsi vidakuzi huwekwa na kutumiwa unapovinjari na kufuta data ya kuvinjari na vidakuzi. Pia, kivinjari chako kinaweza kuwa na mipangilio inayokuruhusu udhibiti vidakuzi kulingana na tovuti. Kwa mfano, mipangilio ya Google Chrome katika chrome://settings/cookies hukuruhusu ufute vidakuzi vilivyopo, uruhusu au uzuie vidakuzi vyote na uweke mapendeleo ya vidakuzi kwenye tovuti. Google Chrome pia ina Hali Fiche, ambayo hufuta historia yako ya kuvinjari na huondoa vidakuzi kwenye kifaa chako ukishafunga Madirisha Fiche.

Kudhibiti teknolojia nyingine katika programu na vifaa vyako

Programu na vifaa vingi vya mkononi hukuruhusu udhibiti jinsi teknolojia nyingine, kama vile vitambulishi mahususi vinavyotumiwa kutambua kivinjari, programu au kifaa, huwekwa na kutumiwa. Kwa mfano, Kitambulisho cha Matangazo kwenye vifaa vya Android au Kitambulisho cha Matangazo kwenye Apple vinaweza kudhibitiwa kwenye mipangilio ya kifaa chako, huku vitambulishi mahususi vya programu vikiweza kudhibitiwa kwa kawaida katika mipangilio ya programu.

Programu za Google
Menyu kuu