Huduma za utangazaji za Google zinajaribu njia mpya za kuendeleza uwasilishaji na upimaji wa utangazaji dijitali kwa namna ambazo zitalinda vizuri faragha ya watu mtandaoni kupitia mradi wa Mazingira ya Faragha kwenye Chrome na Android. Watumiaji ambao wamewasha mipangilio husika ya Mazingira ya Faragha katika Chrome au Android wanaweza kuona matangazo husika kutoka kwenye huduma za utangazaji za Google kulingana na Mada au data ya Hadhira Inayolindwa iliyohifadhiwa kwenye kifaa cha mkononi au kivinjari chao. Huduma za utangazaji za Google zinaweza pia kupima utendaji wa matangazo kwa kutumia data ya Ripoti za Uhusishaji iliyohifadhiwa kwenye kifaa cha mkononi au kivinjari chao. Maelezo zaidi kuhusu Mazingira ya Faragha.
Jinsi Google inavyotumia maelezo kutoka kwenye tovuti au programu zinazotumia huduma zetu
Tovuti na programu nyingi hutumia huduma za Google kuboresha maudhui yao na kuendelea kuyatoa bila malipo. Zinapounganisha huduma zetu, tovuti na programu hizi hushiriki maelezo na Google.
Kwa mfano, unapotembelea tovuti inayotumia huduma za matangazo kama vile AdSense, ikiwa ni pamoja na zana za takwimu kama vile Google Analytics, au inayopachika maudhui ya video kutoka YouTube, kivinjari chako hutuma maelezo fulani kwa Google kiotomatiki. Hii inajumuisha URL ya ukurasa unaotembelea na anwani yako ya IP. Tunaweza pia kuweka vidakuzi kwenye kivinjari chako au kusoma vidakuzi ambavyo tayari vipo. Programu zinazotumia huduma za matangazo za Google pia hushiriki maelezo kwa Google, kama vile jina la programu na kitambulishaji cha kipekee kwa ajili ya matangazo.
Google hutumia maelezo yanayoshirikiwa na tovuti na programu kutoa huduma zetu, kuzidumisha na kuziboresha, kutayarisha huduma mpya, kupima ufanisi wa matangazo, kuzuia ulaghai na matumizi mabaya na kuboresha maudhui na matangazo unayoona kwenye Google na kwenye tovuti na programu za washirika wetu. Tembelea Sera yetu ya Faragha ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyochakata data kwa madhumuni yote haya na tembelea ukurasa wetu wa Utangazaji upate maelezo zaidi kuhusu matangazo ya Google, jinsi maelezo yako yanavyotumiwa katika mazingira ya utangazaji na urefu wa muda ambao Google huhifadhi maelezo haya.
Sera yetu ya Faragha hufafanua misingi ya kisheria ambayo Google hutegemea kuchakata taarifa yako — kwa mfano, tunaweza kuchakata taarifa yako ukituruhusu au kutokana na sababu halali kama vile kutoa, kudumisha na kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wetu.
Wakati mwingine, tunapochakata taarifa zinazoshirikiwa nasi na tovuti na programu, tovuti na programu hizo zitaomba idhini yako kabla ya kuruhusu Google ichakate taarifa zako. Kwa mfano, unaweza kuona bango kwenye tovuti likiomba idhini ili Google ichakate taarifa ambazo tovuti hukusanya. Hilo likifanyika, tutatii madhumuni yaliyofafanuliwa kwenye idhini utakayotoa kwa tovuti au programu, badala ya misingi ya kisheria iliyofafanuliwa katika Sera ya Faragha ya Google. Iwapo ungependa kubadilisha au kuondoa idhini yako, unapaswa kutembelea tovuti au programu husika ili ufanye hivyo.
Kuweka mapendeleo ya matangazo
Ikiwa kipengele cha kuweka mapendeleo ya matangazo kimewashwa, Google itatumia maelezo yako kuyafanya matangazo yakufae zaidi. Kwa mfano, tovuti ambayo huuza baiskeli za kuendeshwa milimani inaweza kutumia huduma za matangazo ya Google. Baada ya kutembelea tovuti hiyo, unaweza kuona tangazo la baiskeli za kuendeshwa milimani kwenye tovuti nyingine inayoonyesha matangazo yaliyotangazwa na Google.
Ikiwa kipengele cha kuweka mapendeleo ya matangazo kimezimwa, Google haitakusanya wala kutumia maelezo yako kuunda wasifu wa matangazo wala kuweka mapendeleo ya matangazo ambayo Google inakuonyesha. Bado utaona matangazo, lakini huenda yasikufae. Matangazo bado yanaweza kutegemea mada ya tovuti au programu unayotumia, hoja za utafutaji unazotumia sasa, au mahali ulipo kwa jumla, lakini si mambo yanayokuvutia, historia ya mambo uliyotafuta au historia ya mambo uliyovinjari. Maelezo yako bado yanaweza kutumika kwa madhumuni mengine yaliyotajwa hapo juu, kama vile kupima ufanisi wa matangazo na kuzuia ulaghai na matumizi mabaya.
Unapotumia tovuti au programu ambayo hutumia huduma za Google, huenda ukaombwa kuchagua ikiwa unataka kuona matangazo yaliyowekwa mapendeleo kutoka kwa watoa huduma za matangazo, ikiwa ni pamoja na Google. Bila kubagua chaguo lako, Google haitaweka mapendeleo ya matangazo unayoyaona ikiwa mipangilio yako ya kuweka mapendeleo ya matangazo imezimwa au akaunti yako haitimizi masharti ya kuonyesha matangazo yaliyowekwa mapendeleo.
Unaweza kuona na kudhibiti maelezo tunayotumia kukuonyesha matangazo kwa kutembelea mipangilio yako ya matangazo.
Jinsi unavyoweza kudhibiti maelezo yaliyokusanywa na Google kwenye tovuti na programu hizi
Hizi ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kudhibiti maelezo yanayoshirikiwa na kifaa chako unapotembelea au kutumia tovuti na programu zinazotumia huduma za Google:
- Mipangilio ya Matangazo hukusaidia kudhibiti matangazo unayoyaona kwenye huduma za Google (kama vile Huduma ya Tafuta na Google au YouTube), au kwenye tovuti na programu zisizo za Google ambazo hutumia huduma za matangazo kutoka Google. Unaweza pia kupata maelezo kuhusu jinsi matangazo yanavyowekwa mapendeleo, kuchagua kutopokea mapendeleo ya matangazo na kuzuia watangazaji mahususi.
- Ikiwa umeingia katika Akaunti yako ya Google na kulingana na mipangilio ya Akaunti yako, kipengele cha Shughuli Zangu kinakuwezesha kukagua na kudhibiti data inayoundwa wakati unatumia huduma za Google, ikiwa ni pamoja na maelezo tunayokusanya kutoka kwenye tovuti na programu ambazo umetembelea. Unaweza kuvinjari kulingana na tarehe na mada na kufuta baadhi ya shughuli zako au shughuli zote.
- Tovuti na programu nyingi hutumia Google Analytics ili kuelewa jinsi wageni wanavyotumia tovuti au programu zao. Ikiwa hutaki Google Analytics itumiwe katika kivinjari chako, unaweza kusakinisha programu jalizi ya kivinjari cha Google Analytics. Pata maelezo zaidi kuhusu Google Analytics na faragha.
- Hali fiche katika Chrome hukuwezesha kuvinjari wavuti bila kurekodi kurasa za wavuti na faili katika kivinjari chako au Historia ya akaunti (isipokuwa ukiamua kuingia katika akaunti yako). Vidakuzi hufutwa baada ya kufunga madirisha na vichupo vyako vyote vya hali fiche na maalamisho na mipangilio yako huhifadhiwa hadi unapoifuta. Pata maelezo zaidi kuhusu vidakuzi. Kutumia Hali fiche kwenye kivinjari cha Chrome au hali nyingine za kuvinjari kwa faragha hakuzuii ukusanyaji wa data unapotembelea tovuti zinazotumia huduma za Google na Google bado inaweza kukusanya data unapotembelea tovuti kwa kutumia vivinjari hivi.
- Vivinjari vingi, ikiwa ni pamoja na Chrome, hukuwezesha kuzuia vidakuzi vya washirika wengine. Unaweza pia kufuta vidakuzi vyovyote vilivyopo kwenye kivinjari chako. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti vidakuzi katika Chrome.