Jinsi Google hutumia utambuzi wa ruwaza

Jinsi Google hutumia utambuzi wa ruwaza ili kupata maana ya picha

Kompyuta "hazioni" picha na video kwa njia sawa ambayo watu huona. Unapoangalia picha, unaweza kumwona rafiki yako wa dhati akiwa amesimama mbele ya nyumba yake. Kwa mtazamo wa kompyuta, picha hiyo hiyo inachukuliwa kuwa mkusanyiko wa data unaofasiriwa kama maumbo na maelezo ya mfululizo wa rangi. Ingawa kompyuta haitafanya kama wewe ufanyavyo unapoona picha hiyo, kompyuta inaweza kufunzwa kutambua ruwaza fulani za rangi na maumbo. Kwa mfano, kompyuta inaweza kufunzwa kutambua ruwaza za kawaida za maumbo na rangi zinazotumika kutengeneza picha ya dijitali ya mandhari kama vile ufuo au kitu kama gari. Teknolojia hii inasaidia huduma ya Picha kwenye Google kupanga picha zako na kuwezesha watumiaji kupata picha yoyote kwa kutafuta tu.

Kompyuta pia inaweza kufunzwa kutambua ruwaza za kawaida za maumbo na rangi zinazotumika kutengeneza picha ya dijitali ya uso. Mchakato huu unajulikana kama utambuaji nyuso. Google inatumia teknolojia hii kulinda faragha yako kwenye huduma kama vile Taswira ya Mtaa, ambapo kompyuta hujaribu kutambua na kisha kutia ukungu nyuso za watu ambao wanaweza kuwa wamesimama mtaani gari la Taswira ya Mtaa linapopita.

Katika kiwango cha juu, teknolojia hiyo ya utambuzi wa ruwaza inayotumika kutambua nyuso inaweza kusaidia kompyuta kuelewa sifa za uso ambao imetambua. Kwa mfano, kunaweza kuwa na ruwaza fulani zinazoonyesha kuwa uso unatabasamu au macho yake yamefumbwa. Maelezo kama haya yanaweza kutumiwa kusaidia kwa vipengele kama vile kutoa mapendekezo ya filamu na madoido mengine yanayoundwa kutokana na picha na video zako katika Picha kwenye Google .

Teknolojia sawa inatumika katika kipengele cha kupanga picha katika makundi kulingana na nyuso za waliomo kinachopatikana katika Picha kwenye Google katika baadhi ya nchi. Kipengele hiki kinawezesha kompyuta kutambua nyuso zinazofanana na kuziweka pamoja katika makundi, hivyo watumiaji wanaweza kutafuta na kudhibiti picha zao kwa urahisi. Pata maelezo zaidi kuhusu kupanga picha katika makundi kulingana na nyuso za waliomo katika Kituo cha Usaidizi cha Picha kwenye Google.

Jinsi Kutafuta kwa Kutamka hufanya kazi

Kipengele cha Kutafuta kwa Kutamka kinakuwezesha kutamka hoja ya utafutaji kwenye programu ya seva teja ya huduma ya tafuta na Google kwenye kifaa badala ya kuandika hoja hiyo. Hutumia utambuaji wa ruwaza kunukuu maneno yaliyosemwa kuwa maandishi. Huwa tunatuma matamshi kwenye seva za Google ili kutambua ulichosema.

Huwa tunahifadhi lugha, nchi na kisio la mfumo wetu la unachosema kwa kila hoja ya utafutaji unayotamka ukitumia kipengele cha Kutafuta kwa Kutamka. Huwa tunahifadhi matamshi ili kuboresha huduma zetu, ikiwemo kufunza mfumo jinsi ya kugundua kwa usahihi zaidi hoja za utafutaji iwapo umetuidhinisha kutumia data yako kwa madhumuni haya. Hatutumi tamko lolote kwa Google isipokuwa uwe umeonyesha nia ya kutumia kipengele cha Kutafuta kwa Kutamka (kwa mfano, kubonyeza aikoni ya maikrofoni katika upau wa utafutaji wa haraka au katika kibodi pepe au kwa kusema "Google" wakati upau wa utafutaji wa haraka unaashiria kwamba kipengele cha Kutafuta kwa Kutamka kinapatikana).

Programu za Google
Menyu kuu