Jinsi Google inavyohifadhi data inayokusanya

Tunakusanya data unapotumia huduma za Google. Sera yetu ya Faragha inafafanua kuhusu data tunayokusanya, sababu za kuikusanya na jinsi unavyoweza kudhibiti maelezo yako. Sera hii ya kuhifadhi data inaelezea sababu ya kuhifadhi aina tofauti za data kwa muda tofauti.

Unaweza kufuta baadhi ya data wakati wowote, nyingine hufutwa kiotomatiki na nyingine huhifadhiwa kwa muda inapohitajika. Unapofuta data, sera ya ufutaji data inatumika ili kuhakikisha kwamba data yako imeondolewa kabisa kwenye seva zetu kwa njia salama au imehifadhiwa tu kwa njia isiyokutambulisha. Jinsi Google inavyoficha utambulisho wa data

Maelezo yanayohifadhiwa hadi uyaondoe

Tuna huduma mbalimbali zinazokuwezesha kurekebisha au kufuta data iliyohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google. Kwa mfano, unaweza:

Tutahifadhi data hii katika Akaunti yako ya Google hadi utakapoifuta. Ikiwa unatumia huduma zetu bila kuingia katika Akaunti ya Google, unaweza kufuta baadhi ya maelezo yanayohusishwa na kile unachotumia kufikia huduma zetu, kama vile kifaa, kivinjari au programu.

Data ambayo muda wake wa kutumika utakwisha baada ya kipindi mahususi

Wakati mwingine, badala ya kutoa njia ya kufuta data, tunaihifadhi kwa kipindi kilichobainishwa awali. Kwa kila aina ya data, tunabainisha muda wa kuhifadhi kulingana na sababu za kukusanywa kwa data hiyo. Kwa mfano, ili kuhakikisha kuwa huduma zetu zinaonyeshwa vizuri kwenye aina tofauti za vifaa, tunaweza kuhifadhi upana na urefu wa kivinjari kwa muda wa hadi miezi 9. Tunachukua hatua pia ili kuficha utambulisho wa data fulani katika vipindi mahususi vilivyobainishwa. Kwa mfano, kuficha utambulisho wa data ya matangazo katika kumbukumbu za seva kwa kuondoa maelezo ya anwani ya IP baada ya miezi 9 na maelezo ya vidakuzi baada ya miezi 18. Tunaweza pia kuhifadhi data ambayo utambulisho wake umefichwa, kama vile hoja ambazo zimeondolewa kwenye Akaunti za watumiaji wa Google, kwa kipindi fulani kilichobainishwa.

Maelezo yanayohifadhiwa hadi utakapofuta Akaunti yako ya Google

Tunahifadhi baadhi ya data kadri Akaunti yako ya Google inavyodumu, ikiwa inatusaidia kuelewa jinsi watumiaji wanavyotumia vipengele vyetu na jinsi tunavyoweza kuboresha huduma zetu. Kwa mfano, ukifuta anwani ambayo umetafuta katika Ramani za Google, bado akaunti yako inaweza kutambua kuwa umetumia kipengele cha maelekezo. Kwa hivyo, Ramani za Google zinaweza kuepuka kukuonyesha jinsi ya kutumia kipengele cha maelekezo wakati ujao.

Maelezo yanayohifadhiwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa madhumuni maalum

Wakati mwingine, mahitaji ya biashara na sheria yanatulazimu kuhifadhi maelezo fulani, kwa madhumuni maalum. Kwa mfano, Google inapochakata malipo yako, au unapolipa Google, tutahifadhi data hii kwa muda kama inavyotakiwa kwa madhumuni ya ushuru na au uhasibu. Sababu za kuhifadhi data kwa muda ni pamoja na:

Kuwezesha ufutaji kamili wa data na kwa njia salama

Unapofuta data katika akaunti yako ya Google, tunaanza papo hapo mchakato wa kuiondoa kwenye bidhaa na mifumo yetu. Kwanza, tunalenga kuiondoa mara moja isionekane na data haitatumika tena kugeuza hali yako ya utumiaji kwenye Google ikufae. Kwa mfano, ukifuta video uliyotazama kwenye dashibodi ya Shughuli Zangu, YouTube itaacha mara moja kukuonyesha mahali ambapo umefikia kutazama video hiyo.

Kisha tunaanza mchakato wa kufuta data kabisa kwa njia salama kwenye mifumo yetu ya kuhifadhi. Ufutaji data kwa njia salama ni muhimu kwa ajili ya kuwalinda watumiaji na wateja wetu kutokana na kufuta data kimakosa. Ufutaji kamili wa data kwenye seva zetu ni muhimu ili kuwahakikishia watumiaji kuwa data yao imefutwa kabisa. Mchakato huu kwa kawaida huchukua takribani miezi 2 kutoka wakati data ilifutwa. Mchakato huu unajumuisha kipindi cha hadi mwezi mmoja wa kurejesha data endapo ilifutwa kimakosa.

Kila mfumo wa hifadhi ya Google ambao data yake hufutwa ina mchakato wake wa kina wa kufuta data kabisa kwa njia salama. Hii inaweza kuhusisha ukaguzi wa mfumo wa mara kwa mara ili kuthibitisha kuwa data yote imefutwa, au ucheleweshaji wa muda mfupi ili kuwezesha data iliyofutwa kimakosa irejeshwe. Kutokana na hili, huenda wakati mwingine ufutaji ukachukua muda wakati muda wa ziada unapohitajika ili kufuta data kabisa na kwa njia salama.

Huduma zetu pia hutumia hifadhi mbadala iliyosimbwa kwa njia fiche kama safu nyingine ya ulinzi dhidi ya vitisho vya usalama vinavyoweza kutokea. Data inaweza kusalia kwenye mifumo hii hadi miezi 6.

Kama ilivyo katika mchakato wowote wa kufuta, mambo kama vile kudumisha shughuli za kawaida, nguvu za umeme kupotea bila kutarajia, hitilafu au kasoro katika itifaki zetu yanaweza kusababisha kuchelewesha michakato na muda uliobainishwa katika makala haya. Tunadumisha mifumo inayoweza kugundua na kutatua matatizo haya.

Usalama, kuzuia ulaghai na matumizi mabaya

Maelezo

Ili kukulinda wewe, watu wengine na Google dhidi ya ulaghai, matumizi mabaya na ufikiaji usioidhinishwa.

Matukio

Kwa mfano, Google ikishuku kuwa mtu anafanya ulaghai wa matangazo.

Kudhibiti kumbukumbu za kifedha

Maelezo

Wakati Google inahusika katika miamala ya kifedha, ikijumuisha wakati Google inachakata malipo yako au unapoilipa Google. Kuhifadhi maelezo haya kwa muda mrefu mara nyingi huhitajika kwa madhumuni kama vile uhasibu, utatuzi wa migogoro na kutii masharti ya kodi, kurejesha mali iliyoachwa, kuzuia pesa haramu na sheria nyingine za kifedha.

Matukio

Kwa mfano, ukinununua programu kutoka kwenye Play Store au bidhaa kutoka Google Store.

Kutii mahitaji au kanuni za kisheria

Maelezo

Ili kutimiza sheria, kanuni, utaratibu wa kisheria unaotumika au ombi la serikali linalopaswa kutekelezwa au linalohitajika ili kutekeleza Sheria na Masharti yanayotumika, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa ukiukaji unaoweza kutokea.

Matukio

Kwa mfano, ikiwa Google itapokea amri halali ya kutoa ushahidi.

Kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma zetu

Maelezo

Ili kuhakikisha kwamba wewe na watumiaji wengine mnaendelea kupokea huduma.

Matukio

Kwa mfano, unaposhiriki maelezo na watumiaji wengine (kama vile unapomtumia mtu mwingine barua pepe), kuyafuta kwenye Akaunti yako ya Google hakutaziondoa nakala zilizohifadhiwa na wapokeaji.

Kuwasiliana na Google moja kwa moja

Maelezo

Ikiwa umewasiliana na Google moja kwa moja kupitia kituo cha usaidizi kwa wateja, fomu ya maoni, au ripoti ya hitilafu, Google inaweza kuhifadhi kiasi fulani cha rekodi za mawasiliano hayo.

Matukio

Kwa mfano, unapotuma maoni ndani ya programu ya Google kama vile Gmail au Hifadhi.

Programu za Google
Menyu kuu