Jinsi Google Voice hufanya kazi
Google Voice huhifadhi, kuchakata na kuhifadhi historia yako ya simu (ikiwa ni pamoja na nambari za wanaokupigia, nambari za waliopigiwa, tarehe, saa, na muda wa simu) salamu za ujumbe wa sauti, ujumbe wa sauti, Huduma ya Ujumbe Mfupi (SMS), mazungumzo yaliyorekodiwa, na data nyingine inayohusiana na akaunti yako ili kutoa huduma kwako.
Unaweza kufuta historia yako ya simu, salamu za sauti, ujumbe wa sauti (wa kusikilizwa na/au wa kunukuliwa), ujumbe wa Huduma ya Ujumbe Mfupi (SMS), na mazungumzo yaliyorekodiwa kupitia akaunti yako ya Google Voice. Hata hivyo, historia ya simu ulizopiga, ambazo zinalipishwa, huenda ikabaki kwenye akaunti yako. Baadhi ya maelezo yanaweza kubaki kwa muda mfupi kwenye seva zetu zinazotumika, kwa sababu za bili au majukumu mengine ya biashara, na nakala za akiba zinaweza kubaki katika mifumo yetu ya kuhifadhi rudufu. Nakala zisizotambulisha za maelezo ya rekodi za simu, zisizokuwa na maelezo ya kibinafsi yanayoweza kumtambua mtu, zitabaki katika mifumo yetu ili kutimiza mahitaji yetu ya kuripoti na ukaguzi.