Hili ni toleo lililohifadhiwa la Sheria na Masharti yetu. Tazama toleo la sasa au matoleo yote ya awali.

Sheria na Masharti ya Google

Inatumika kuanzia 31 Machi 2020 | Matoleo yaliyowekwa kwenye kumbukumbu | Pakua PDF

Mambo yanayoshughulikiwa katika sheria na masharti haya

Tunafahamu kuwa unaweza kutaka kuruka Sheria na Masharti haya, lakini ni muhimu ujue mambo unayofaa kutarajia kutoka kwetu unapotumia huduma za Google na mambo tunayotarajia kutoka kwako.

Sheria na Masharti haya yanaonyesha jinsi biashara ya Google hufanya kazi, sheria zinazotumika katika kampuni yetu na mambo fulani ambayo tunaamini kila mara kuwa ya kweli. Kutokana na hayo, Sheria na Masharti haya yanasaidia kufafanua uhusiano wako na Google unapotumia huduma zetu. Kwa mfano, sheria na masharti haya yana mada zifuatazo:

Ni muhimu uelewe sheria na masharti haya kwa sababu, kwa kutumia huduma zetu, unakubali sheria na masharti haya.

Mbali na sheria na masharti haya, pia huwa tunachapisha Sera ya Faragha. Ingawa si sehemu ya sheria na masharti haya, tunakuhimiza uisome ili uelewe kwa njia bora jinsi unavyoweza kusasisha, kudhibiti, kutuma na kufuta taarifa zako.

Mtoa huduma

Huduma za Google zinatolewa na, na unaingia katika mkataba na:

Google LLC
imepangwa kwa mujibu wa sheria za Jimbo la Delaware, Marekani na inafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Marekani

1600 Amphitheatre Parkway
Mountain View, California 94043
Marekani

Masharti ya umri

Iwapo hujafikisha umri unaoruhusiwa kusimamia Akaunti yako mwenyewe ya Google, ni lazima uwe na ruhusa ya mzazi au mlezi anayejulikana kisheria, ya kutumia Akaunti ya Google. Tafadhali mwombe mzazi au mlezi wako anayejulikana kisheria asome sheria na masharti haya pamoja nawe.

Iwapo wewe ni mzazi au mlezi unayejulikana kisheria na unamruhusu mtoto wako atumie huduma, basi sheria na masharti haya yanatumika kwako na unawajibikia shughuli za mtoto wako kwenye huduma.

Baadhi ya huduma za Google zina masharti ya ziada ya umri jinsi inavyobainishwa katika sera na sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi.

Uhusiano wako na Google

Sheria na masharti haya yanasaidia kufafanua uhusiano kati yako na Google. Kwa jumla, tunakupa ruhusa ya kutumia huduma zetu iwapo utakubali kufuata sheria na masharti haya, ambayo yanaonyesha jinsi biashara ya Google hufanya kazi na jinsi tunavyochuma pesa. Tunapozungumza kuhusu “Google,” “sisi,” “tu-,” na “yetu,” tunamaanisha Google LLC na washirika wake.

Mambo unayoweza kutarajia kutoka kwetu

Kutoa aina nyingi ya bidhaa zinazofaa

Tunatoa aina nyingi za huduma ambazo zinategemea sheria na masharti haya, ikiwa ni pamoja na:

  • programu na tovuti (kama vile huduma za Tafuta na Ramani)
  • mifumo (kama vile Google Play)
  • huduma zilizojumuishwa (kama vile Ramani zilizopachikwa kwenye programu au tovuti za kampuni zingine)
  • vifaa (kama vile Google Home)

Huduma zingine zinabuniwa ili zifanye kazi pamoja, hali inayokurahisishia kutoka kwenye shughuli moja hadi nyingine. Kwa mfano, Ramani zinaweza kukumbusha uhudhurie miadi ambayo inaonekana kwenye Kalenda ya Google.

Kuboresha huduma za Google

Tunaendelea kubuni vipengele na teknolojia mpya ili kuboresha huduma zetu. Kwa mfano, tunawekeza katika utashi wa kompyuta ambao unatumia mbinu ya mashine kujifunza ili kutambua na kuzuia taka na programu hasidi na kukupa vipengele bora, kama vile tafsiri za moja kwa moja. Kama sehemu ya juhudi hizi za kuendelea kuboresha huduma zetu, wakati mwingine tunaongeza au kuondoa vipengele na utendaji, kuongeza au kupunguza wigo wa huduma zetu, na kuanza kutoa huduma mpya au kusimamisha za zamani.

Iwapo tutafanya mabadiliko muhimu ambayo yataathiri vibaya jinsi utakavyotumia huduma zetu au iwapo tutaacha kutoa huduma, tutakupa ilani adilifu ya mapema na fursa ya kuhamisha maudhui yako kutoka kwenye Akaunti yako ya Google ukitumia Google Takeout, isipokuwa katika hali za dharura kama vile kuzuia matumizi mabaya, kutimiza mahitaji ya kisheria au kushughulikia masuala ya utendaji na usalama.

Mambo tunayotarajia kutoka kwako

Fuata sheria na masharti haya na sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi

Ruhusa tunayokupa ya kutumia huduma zetu huendelea kutumika mradi unatimiza wajibu wako katika:

Pia tunafanya sera, vituo vya usaidizi na nyenzo zingine mbalimbali zipatikane kwako ili kujibu maswali ya kawaida na kuweka matarajio kuhusu utumiaji wa huduma zetu. Nyenzo hizi ni pamoja na Sera ya Faragha, Kituo cha Usaidizi wa Hakimiliki, Kituo cha Usalama na kurasa zingine zinazoweza kufikiwa kwenye tovuti yetu ya sera.

Ingawa tunakupa ruhusa ya kutumia huduma zetu, tunahifadhi haki zozote za uvumbuzi tulizonazo kwenye huduma.

Kuheshimu watu wengine

Huduma zetu nyingi zinakuruhusu ushirikiane na watu wengine. Tunataka kudumisha mazingira yenye heshima kwa kila mtu, hali inayomaanisha kuwa ni lazima utii kanuni hizi za msingi za matendo:

  • utii sheria zinazotumika, ikiwa ni pamoja na sheria za udhibiti wa bidhaa zinazohamishwa, vikwazo na sheria za ulanguzi wa binadamu
  • uheshimu haki za watu wengine, ikiwa ni pamoja na faragha na haki za uvumbuzi
  • usiwadhulumu wala kuwadhuru watu wengine au kujidhuru (au utishie au uhimize dhuluma au madhara kama hayo) — kwa mfano, kwa kupotosha, kulaghai, kudhalilisha, kuchokoza, kunyanyasa au kunyatia watu wengine
  • usitumie vibaya, kudhuru, kuathiri au kukatiza huduma

Sheria na masharti na sera zetu za ziada za huduma mahususi zinatoa maelezo ya ziada kuhusu vitendo vinavyoruhusiwa ambavyo watumizi wote wa hizo huduma lazima watii. Iwapo utapata kuwa watu wengine hawafuati sheria hizi, huduma zetu nyingi zinakuruhusu uripoti matumizi mabaya. Iwapo tutachukua hatua kutokana na ripoti ya matumizi mabaya, tutatoa pia mchakato wa haki jinsi inavyobainishwa katika sehemu ya Kuchukua hatua iwapo matatizo yatatokea.

Ruhusa ya kutumia maudhui yako

Baadhi ya huduma zetu zinakuruhusu upakie, uwasilishe, uhifadhi, utume, upokee au ushiriki maudhui yako. Huna wajibu wowote wa kuweka maudhui yoyote kwenye huduma zetu na una uhuru wa kuchagua maudhui ambayo ungependa kuweka. Iwapo utaamua kupakia au kushiriki maudhui, tafadhali hakikisha kuwa una haki zinazohitajika kufanya hivyo na kuwa maudhui ni halali.

Leseni

Maudhui yako husalia kuwa yako, yaani unahifadhi haki zozote za uvumbuzi ulizonazo kwenye maudhui. Kwa mfano, una haki za uvumbuzi katika maudhui bunifu unayotengeneza, kama vile maoni unayotoa. Au, unaweza kuwa na haki ya kushiriki maudhui bunifu ya mtu mwingine iwapo amekupa ruhusa.

Tunahitaji ruhusa yako iwapo haki zako za uvumbuzi zinatuzuia kutumia maudhui yako. Unaipa Google ruhusa hiyo kupitia leseni hii.

Mambo yanayoshughulikiwa

Leseni hii inashughulikia maudhui yako iwapo maudhui hayo yanalindwa kwa haki za uvumbuzi.

Mambo ambayo hayashughulikiwi

  • Leseni hii haiathiri haki zako za faragha — inahusu tu haki zako za uvumbuzi
  • Leseni hii haishughulikii aina hizi za maudhui:
    • maelezo ya kweli yanayopatikana kwa umma ambayo unatoa, kama vile masahihisho kwenye anwani ya biashara za karibu. Maelezo hayo hayahitaji leseni kwa sababu yanazingatiwa kuwa maarifa ya kawaida ambayo kila mtu ana uhuru wa kuyatumia.
    • maoni unayotoa, kama vile mapendekezo ya kuboresha huduma zetu. Maoni yanashughulikiwa katika sehemu ya Mawasiliano yanayohusiana na huduma hapa chini.

Upeo

Leseni hii:

  • inatumika ulimwenguni kote, yaani inakubaliwa mahali popote ulimwenguni
  • si ya kipekee, yaani unaweza kutoa leseni ya maudhui yako kwa watu wengine
  • haina mrabaha, yaani hamna ada kwa leseni hii

Haki

Leseni hii inairuhusu Google:

  • kupangisha, kutengeneza upya, kusambaza, kuwasiliana na kutumia maudhui yako — kwa mfano, kuhifadhi maudhui yako kwenye mifumo yetu na kufanya yapatikane popote uendapo
  • kuchapisha, kutumia au kuonyesha maudhui yako hadharani, iwapo umeyafanya yaonekane kwa watu wengine
  • kubadilisha na kubuni miigo ya kazi zinazotokana na maudhui yako, kama vile kubadilisha muundo au kuyatafsiri
  • kutoa haki hizi za kijileseni kwa:
    • watumiaji wengine waruhusu huduma ifanye kazi jinsi inavyopaswa, kama vile kukuruhusu ushiriki picha na watu unaowachagua
    • makontrakta wetu ambao wameweka sahihi makubaliano nasi ambayo yanafuata sheria na masharti haya, kwa madhumuni machache yanayobainishwa tu katika sehemu ya Madhumuni hapa chini

Madhumuni

Leseni hii inatumika kwa madhumuni machache ya:

  • kuendesha na kuboresha huduma, yaani kuruhusu huduma kufanya kazi jinsi inavyopaswa na kutengeneza vipengele na utendaji mpya. Hii ni pamoja na kutumia algoriti na mifumo otomati ili kuchanganua maudhui yako:
    • kwa taka, programu hasidi na maudhui haramu
    • kutambua mitindo katika data, kama vile kubaini wakati wa kupendekeza albamu mpya katika programu ya Picha kwenye Google ili kuweka picha zinazohusiana pamoja
    • ili kufanya huduma zetu zikufae zaidi, kama vile kukupa mapendekezo, matangazo, maudhui na matokeo ya utafutaji yanayokufaa zaidi, (ambayo unaweza kubadilisha au kuzima katika Mipangilio ya Matangazo)
    Uchambuzi huu hutokea wakati maudhui yanatumwa, kupokewa, na wakati yanahifadhiwa.
  • kutumia maudhui ambayo umeshiriki hadharani ili kutangaza huduma. Kwa mfano, ili kutangaza programu ya Google, tunaweza kunukuu maoni uliyotoa. Au, ili kutangaza Google Play, tunaweza kuonyesha picha ya skrini ya programu uliyoweka katika Duka la Google Play.
  • kubuni teknolojia na huduma mpya za Google kwa kuzingatia sheria na masharti haya

Muda

Leseni hii inatumika kwa kipindi chote ambapo maudhui yako yanalindwa kwa haki za uvumbuzi.

Iwapo utaondoa maudhui yoyote yanayoshughulikiwa na leseni hii kwenye huduma zetu, basi mifumo yetu itaondoa maudhui hayo hadharani kwa muda adilifu. Kuna hali mbili zisizofuata kanuni:

  • Iwapo tayari ulishiriki maudhui yako na watu wengine kabla ya kuyaondoa. Kwa mfano, iwapo ulishiriki picha na rafiki ambaye baadaye alitoa nakala yake au kuishiriki tena, basi picha hiyo inaweza kuendelea kuonekana kwenye Akaunti ya Google ya rafiki yako hata baada ya kuiondoa kwenye Akaunti yako ya Google.
  • Ukifanya maudhui yako yapatikane kupitia huduma za kampuni zingine, kuna uwezekano kuwa mitambo ya kutafuta, ikiwa ni pamoja na huduma ya Tafuta na Google, itaendelea kupata na kuonyesha maudhui yako kama sehemu ya matokeo yake ya utafutaji.

Kutumia huduma za Google

Akaunti yako ya Google

Iwapo unatimiza masharti haya ya umri unaweza kufungua Akaunti ya Google unapohitaji. Baadhi ya huduma zinahitaji uwe na Akaunti ya Google ili ziweze kufanya kazi — kwa mfano, ili utumie Gmail, unahitaji Akaunti ya Google ili uwe na mahali pa kutuma na kupokea barua pepe yako.

Unawajibikia shughuli unazofanya kwenye Akaunti yako ya Google, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zinazofaa za kulinda usalama wa Akaunti yako ya Google. Tunakuhimiza utumie tovuti ya Ukaguzi wa Usalama mara kwa mara.

Kutumia huduma za Google kwa niaba ya shirika

Mashirika mengi, kama vile biashara, mashirika yasiyo ya faida na shule, hupata manufaa ya huduma zetu. Ili utumie huduma zetu kwa niaba ya shirika:

  • ni lazima mwakilishi aliyeidhinishwa wa shirika hilo akubali sheria na masharti haya
  • msimamizi wa shirika lako anaweza kukukabidhi Akaunti ya Google. Msimamizi huyo anaweza kutaka ufuate kanuni za ziada na anaweza kufikia au kufunga Akaunti yako ya Google.

Ili kukupa huduma zetu, wakati mwingine huwa tunakutumia matangazo ya huduma na maelezo mengine. Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyowasiliana nawe, angalia Sera ya Faragha ya Google.

Iwapo utachagua kutupa maoni, kama vile mapendekezo ya kuboresha huduma zetu, tunaweza kuchukua hatua kutokana na maoni yako bila kuwa na wajibu wowote kwako.

Maudhui katika huduma za Google

Maudhui yako

Baadhi ya huduma zetu hukupa fursa ya kufanya maudhui yako yapatikane kwa umma — kwa mfano, unaweza kuchapisha bidhaa au maoni ya mkahawa uliyoandika au unaweza kupakia chapisho kwenye blogu ambalo umetunga.

  • Angalia sehemu ya Ruhusa ya kutumia maudhui yako ili upate maelezo zaidi kuhusu haki zako katika maudhui yako na jinsi maudhui yako yanavyotumika kwenye huduma zetu
  • Angalia sehemu ya Kuondoa maudhui yako ili upate maelezo ya sababu na jinsi tunavyoweza kuondoa maudhui yaliyotengenezwa na watumiaji kwenye huduma zetu

Iwapo unafikiri kuwa mtu fulani anakiuka haki zako za uvumbuzi, unaweza kutuma ilani ya ukiukaji na tutachukua hatua zinazofaa. Kwa mfano, huwa tunasimamisha au kufunga Akaunti ya Google ya watu wanaokiuka hakimiliki mara kwa mara jinsi inavyobainishwa katika Kituo chetu cha Usaidizi wa Hakimiliki.

Maudhui ya Google

Baadhi ya huduma zetu ni pamoja na maudhui yanayomilikiwa na Google — kwa mfano, michoro mingi unayoona kwenye Ramani za Google. Unaweza kutumia maudhui ya Google jinsi inavyoruhusiwa na sheria na masharti haya na sheria na masharti yoyote ya ziada ya huduma mahususi, lakini tunahifadhi haki zozote za uvumbuzi tulizonazo katika maudhui yetu. Usiondoe, kuficha au kubadilisha chapa, nembo au ilani zetu zozote za kisheria. Iwapo ungependa kutumia nembo au chapa zetu, tafadhali angalia ukurasa wa Ruhusa za Chapa za Google.

Maudhui mengine

Mwisho, baadhi ya huduma zetu zinakupa uwezo wa kufikia maudhui ya watu au mashirika mengine — kwa mfano, maelezo ya mmiliki wa duka kuhusu biashara yake mwenyewe au makala ya gazeti yanayoonyeshwa kwenye Google News. Hupaswi kutumia maudhui haya bila ruhusa ya mtu au shirika hilo au bila ruhusa ya kisheria. Maoni yanayotolewa kwenye maudhui ya watu au mashirika mengine ni yao na huenda hayawakilishi maoni ya Google.

Programu katika huduma za Google

Baadhi ya huduma zetu ni pamoja na programu zinazoweza kupakuliwa. Tunakupa ruhusa ya kutumia programu hiyo kama sehemu ya huduma.

Leseni tunayokupa:

  • inatumika ulimwenguni kote, yaani inakubaliwa mahali popote ulimwenguni
  • si ya kipekee, kumaanisha tunaweza kuruhusu utumizi wa programu hii kwa wengine
  • haina mrabaha, yaani hamna ada kwa leseni hii
  • ni ya kibinafsi, yaani haiwezi kutumiwa na mtu mwingine
  • haiwezi kukabidhiwa kwa mtu mwingine, yaani huruhusiwi kumkabidhi mtu mwingine leseni hii

Baadhi ya huduma zetu ni pamoja na programu ambayo inatolewa chini ya sheria na masharti ya leseni ya programu huria ambayo tunakupa. Wakati mwingine kuna sheria katika leseni ya programu huria ambayo inabatilisha kwa njia ya wazi sehemu za sheria na masharti haya, kwa hivyo tafadhali hakikisha kuwa unasoma leseni hizo.

Hupaswi kunakili, kubadilisha, kusambaza, kuuza au kupangisha sehemu yoyote ya huduma au programu zetu. Vile vile, hupaswi kufanya utafiti wa kihandisi au kujaribu kuchopoa msimbo wetu wowote wa tovuti isipokuwa uwe na ruhusa yetu kupitia maandishi au uruhusiwe kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria inayotumika.

Wakati huduma inahitaji au ina programu inayoweza kupakuliwa, programu hiyo hujisasisha kiotomatiki wakati mwingine kwenye kifaa chako pindi kipengele au toleo jipya linapopatikana. Baadhi ya huduma hukuruhusu urekebishe mipangilio yako ya masasisho ya kiotomatiki.

Iwapo kutatokea tatizo au kutokubaliana

Kulingana na sheria, una haki ya (1) kupokea huduma ya kiwango fulani cha ubora, na (2) namna za kusuluhisha shida zinapotokea. Masharti haya hayazuii haki hizo wala kuziondoa. Kwa mfano, ikiwa wewe ni mtumiaji, basi utaendelea kufurahia haki zote za kisheria zinazotolewa kwa wateja kisheria.

Dhima

Tunatoa huduma zetu kwa umakinifu na ujuzi adilifu. Iwapo hatutimizi viwango vya ubora vinavyoelezewa katika dhamana, unakubali kutueleza na tutashirikiana nawe ili kujaribu kusuluhisha tatizo.

Makanusho

Ahadi ya pekee tunayotoa kuhusu huduma zetu (ikiwa ni pamoja na maudhui kwenye huduma, utendakazi mahususi wa huduma zetu au hali ya kutegemeka, upatikanaji au uwezo wa kutimiza mahitaji yako) (1) imefafanuliwa katika sehemu ya Dhamana, (2) imebainishwa katika sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi au (3) imetolewa kwa mujibu wa sheria zinazotumika. Hatutoi ahadi nyingine yoyote kuhusu huduma zetu.

Na isipokuwa iwe inatakikana kisheria, hatutoi dhamana zisizotajwa, kama vile dhamana zisizotajwa za ubora kwa mauzo, ufaafu kwa madhumuni mahususi na kutokiuka haki.

Dhima

Kwa watumiaji wote

Sheria na masharti haya yanadhibiti tu wajibu wetu kwa mujibu wa sheria inayotumika. Hasa, sheria na masharti haya hayadhibiti dhima ya Google kuhusu kifo au majeraha ya binafsi, ulaghai, uwakilishi wa uongo, ulegevu uliokithiri au tabia zisizoruhusiwa zinazofanywa kimakusudi.

Mbali na wajibu na haki zilizobainishwa katika sehemu hii (Iwapo kutatokea matatizo au kutokubaliana), Google haitawajibikia hasara zozote zingine, isipokuwa ziwe zimetokana na hali ambapo tumekiuka sheria na masharti haya au sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi.

Kwa watumiaji wa kibiashara na mashirika pekee

Iwapo wewe ni mtumiaji wa kibiashara au shirika, basi kwa mujibu wa sheria inayotumika:

  • Utaifidia Google na wakurugenzi, maofisa, wafanyakazi na makontrakta wake kutokana na utaratibu wowote wa kisheria unaofanywa na mtu au kampuni nyingine (ikiwa ni pamoja na vitendo vinavyotokana na mamlaka za serikali) unaotokana au kuhusiana na utumiaji wako wa huduma kinyume na sheria au ukiukaji wa sheria na masharti haya au sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi. Fidia hii inashughulikia dhima au matumizi yoyote yanayotokana na madai, hasara, uharibifu, maamuzi, faini, gharama za manza na ada za kisheria.
  • Google haitawajibikia dhima zifuatazo:
    • kupoteza faida, mapato, fursa za kibiashara, sifa au akiba inayotarajiwa
    • hasara inayoambatana au isiyo ya moja kwa moja
    • fidia ya adhabu
  • Dhima kamili ya Google inayotokana au inayohusiana na sheria na masharti haya inatumika kwa kiwango kinachozidi (1) US$500 au (2) 125% ya ada uliyolipa ili utumie huduma zinazohusiana ndani ya miezi 12 kabla ya ukiukaji

Iwapo umeruhusiwa kisheria usitende majukumu fulani, ikiwa ni pamoja na ahadi ya kulipa, basi majukumu hayo hayatumiki kwako chini ya sheria na masharti haya. Kwa mfano, Umoja wa Mataifa hupata kinga fulani za wajibu wa kisheria na sheria na masharti haya hayabatilishi kinga hizo.

Kuchukua hatua iwapo matatizo yatatokea

Kabla ya kuchukua hatua jinsi inavyofafanuliwa hapa chini, tutakupa ilani ya mapema panapowezekana kwa njia adilifu, tutaelezea sababu za kuchukua hatua na tukupe fursa ya kurekebisha tatizo, isipokuwa tuamini kwa njia adilifu kuwa kufanya hivyo kunaweza:

  • kusababisha madhara au dhima kwa mtumiaji, mtu au kampuni nyingine au Google
  • kukiuka sheria au amri ya mamlaka ya utekelezaji wa sheria
  • kuathiri uchunguzi
  • kuathiri uendeshaji, maadili au usalama wa huduma zetu

Kuondoa maudhui yako

Iwapo tunaamini kwa njia adilifu kuwa maudhui yako yoyote (1) yanakiuka sheria na masharti haya, sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi au sera, (2) yanakiuka sheria inayotumika au (3) yanaweza kuwadhuru watumiaji wetu, watu au kampuni zingine au Google, basi tunahifadhi haki ya kuondoa baadhi ya maudhui au maudhui hayo yote kwa mujibu wa sheria inayotumika. Mifano ni pamoja na ponografia inayohusisha watoto, maudhui yanayofanikisha unyanyasaji au ulanguzi wa watu na maudhui yanayokiuka haki za uvumbuzi za mtu mwingine.

Kufunga au kusimamisha uwezo wako wa kufikia huduma za Google

Google inahifadhi haki ya kusimamisha au kumaliza uwezo wako wa kufikia huduma au kufuta Akaunti yako ya Google iwapo kutatokea jambo lolote kati ya haya:

  • unapokiuka mara kwa mara au kwa kiasi kikubwa sheria na masharti, sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi
  • tunatakiwa kufanya hivyo ili kutii mahitaji ya kisheria au amri ya mahakama
  • tunaamini kwa njia adilifu kuwa vitendo vyako vinasababisha madhara au dhima kwa mtumiaji, mtu au kampuni nyingine au Google — kwa mfano, kwa kudukua, kuiba data binafsi, kunyanyasa, kutuma taka, kupotosha wengine au kuchapisha maudhui ambayo si yako

Iwapo unaamini kuwa Akaunti yako ya Google imesimamishwa au kufungwa kimakosa, unaweza kukata rufaa.

Bila shaka, una uhuru wa kuacha kutumia huduma zetu wakati wowote. Iwapo utaacha kutumia huduma fulani, tutashukuru iwapo utatujulisha sababu ili tuweze kuendelea kuboresha huduma zetu.

Kusuluhisha mizozo, sheria ya serikali na mahakama

Kwa maelezo kuhusu jinsi ya kuwasiliana na Google, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa mawasiliano.

Sheria ya California itasimamia mizozo yote inayotokana au inayohusiana na sheria na masharti haya, sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi au huduma zozote zinazohusiana, bila kujali ukinzani wa kanuni za sheria. Mizozo hii itasuluhishwa kwa njia ya kipekee katika mahakama za nchi au jimbo la Santa Clara, California, Marekani na wewe na Google mnakubali uamuzi wa eneo la mamlaka katika mahakama hizo.

Ikiwa sheria za nchi zinazuia migogoro na kesi kusuluhishwa mbele ya korti ya California, huenda ukaweza kuleta kesi hizo mbele ya korti ya nchi yako. Vivyo hivyo, ikiwa sheria za nchi zinazuia korti ya nchi kusuluhisha kesi ikizingatia sheria ya California basi kesi hizo zitasuluhishwa zikizingatia sheria za nchi, mkoa au sehemu ya makazi yako.

Kuhusu sheria na masharti haya

Kwa mujibu wa sheria, una haki fulani ambazo haziwezi kudhibitiwa na mkataba kama vile sheria na masharti haya. Sheria na masharti haya hayanuii kwa njia yoyote kudhibiti haki hizo.

Sheria na masharti haya yanafafanua uhusiano kati yako na Google. Hayabuni haki zozote za kisheria kwa watu au mashirika mengine, hata kama wengine wananufaika kutokana na uhusiano huo chini ya sheria na masharti haya.

Tunataka kufanya sheria na masharti haya yawe rahisi kueleweka, kwa hivyo tumetumia mifano kutoka kwenye huduma zetu. Lakini huenda si bidhaa zote zilizotajwa zinapatikana katika nchi uliko.

Iwapo sheria na masharti haya yanakinzani na sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi, sheria na masharti ya ziada yatatumika kwa huduma hiyo.

Ikitokea kwamba sheria na masharti fulani hayatumiki au hayawezi kutekelezwa, hali hii haitaathiri sheria na masharti mengine yoyote.

Iwapo hufuati sheria na masharti haya au sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi na hatuchukui hatua moja kwa moja, hiyo haimaanishi kuwa tunaachilia haki ambazo huenda tunazo, kama vile kuchukua hatua baadaye.

Tunaweza kusasisha sheria na masharti haya na sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi (1) ili kulingana na mabadiliko kwenye huduma zetu au jinsi tunavyofanya biashara — kwa mfano, tunapoweka huduma, vipengele, teknolojia, bei au manufaa mapya (au kuondoa za zamani), (2) kwa sababu za usalama, udhibiti au sheria (3) ili kuzuia madhara au matumizi mabaya.

Iwapo tutabadilisha masharti haya au sheria na masharti ya ziada ya huduma mahususi, tutakupa taarifa maalum kwa wakati unaofaa na nafasi ya kupitia mabadaliko hayo, isipokuwa (1) tunapozindua huduma au vipengele vipya, au (2) katika hali za dharura zinazohitaji kusuluhishwa kwa haraka, kama kuzuia unyanyasaji unaoendelea, au kujibu mawasiliano ya kisheria. Ikiwa haukubaliani na masharti haya mapya, unapaswa kutoa maudhui yako na uache kutumia huduma hizi. Pia, unaweza kukata uhusiano wako nasi wakati wowote kwa kufunga akaunti yako ya Google.

Ufafanuzi

chapa ya biashara

Ishara, majina na picha zinazotumika katika biashara ambazo zinaweza kutofautisha bidhaa au huduma za shirika au mtu binafsi au shirika na zile za mtu au shirika lingine.

dhamana

Hakikisho kuwa bidhaa au huduma itakuwa na utendaji wa kiwango fulani.

dhima

Hasara zinazotokana na aina yoyote ya madai ya kisheria, iwe madai yanatokana na mkataba, sheria za ulegevu (ikiwa ni pamoja na ulegevu) au sababu zingine na iwapo hasara hizo zingeweza au hazingeweza kutarajiwa au kutabiriwa kwa njia adilifu.

fidia

Wajibu wa kimkataba wa shirika au mtu binafsi wa kufidia hasara zinazopatikana kwa shirika au mtu binafsi kutokana na utaratibu wa mahakama kama vile kesi.

haki za uvumbuzi (hataza)

Haki za kazi za akili ya mtu, kama vile ubunifu (haki za hataza); kazi za fasihi na sanaa (hakimiliki); usanifu (haki za usanifu); na ishara, majina na picha zinazotumika katika biashara (chapa za biashara). Haki za uvumbuzi zinaweza kumilikiwa na wewe, mtu mwingine au shirika.

Haki ya kisheria ambayo inamruhusu mtayarishi wa kazi halisi (kama vile chapisho kwenye blogu, picha au video) kuamua iwapo na jinsi kazi hiyo halisi inaweza kutumiwa na watu wengine.

huduma

Huduma za Google zinazotegemea sheria na masharti haya ni huduma na bidhaa zilizoorodheshwa katika https://policies.google.com/terms/service-specific, ikiwa ni pamoja na:

  • Tovuti na programu za Google (kama vile Tafuta na Ramani)
  • mifumo (kama vile Google Play)
  • huduma zilizojumuishwa (kama vile Ramani zilizopachikwa kwenye programu au tovuti za kampuni zingine)
  • vifaa (kama vile Google Home)

kanusho

Taarifa inayodhibiti majukumu ya kisheria ya mtu.

maudhui yako

Mambo unayoandika, kupakia, kuwasilisha, kuhifadhi, kutuma, kupokea au kushiriki na Google kwa kutumia huduma zetu, kama vile:

  • Hati, Majedwali ya Google na Slaidi za Google unazotengeneza
  • machapisho kwenye blogu unayopakia kupitia Blogger
  • maoni unayotoa kupitia Ramani
  • video unazohifadhi kwenye Hifadhi
  • barua pepe unazotuma na kupokea kupitia Gmail
  • picha unazoshiriki na marafiki kupitia programu ya Picha
  • ratiba za usafiri unazoshiriki na Google

Mfumo wa Umoja wa Ulaya wa Kudhibiti Biashara

Kanuni za (Umoja wa Ulaya) 2019/1150 kuhusu kuhimiza usawa na uwazi kwa watumiaji wa kibiashara wa huduma za uwakala wa mitandaoni.

mshirika

Shirika ambalo liko kwenye kikundi cha kampuni za Google, yaani Google LLC na kampuni inazomiliki, ikiwa ni pamoja na kampuni zifuatazo ambazo zinatoa huduma kwa watumiaji katika Umoja wa Ulaya: Google Ireland Limited, Google Commerce Ltd na Google Dialer Inc.

mtumiaji

Mtu binafsi anayetumia huduma za Google kwa madhumuni ya kibinafsi na yasiyo ya kibiashara nje ya soko, biashara, fani au taaluma yake. (Angalia mtumiaji wa kibiashara)

mtumiaji wa kibiashara

Shirika au mtu binafsi ambaye si mtumiaji (angalia watumiaji).

shirika

Shirika la kisheria (kama vile kampuni, shirika lisilo la faida au shule) wala si mtu binafsi.

Programu za Google
Menyu kuu