Sera ya Matumizi Yasiyokubalika ya AI Inayoweza Kuandaa
Mara ya Mwisho Kubadilishwa: 17 Desemba 2024
Mifumo ya AI zalishi inaweza kukusaidia kugundua, kujifunza na kubuni. Tunatarajia uitumie kwa kuwajibika na kuzingatia sheria na usalama. Masharti yafuatayo yanazingatiwa kwenye matumizi yako ya AI zalishi katika bidhaa na huduma za Google zinazorejelea sera hii.
- Usijihusishe na shughuli hatari, zisizo halali au vinginevyo kukiuka sheria na kanuni zinazotumika. Hii ni pamoja na kutayarisha au kusambaza maudhui ambayo:
- Yanahusiana na dhuluma au unyanyasaji wa watoto kingono.
- Yanawezesha itikadi kali yenye vurugu au ugaidi.
- Yanawezesha kutuma picha za kimapenzi bila idhini ya mhusika.
- Yanawezesha matendo ya kujijeruhi.
- Yanawezesha shughuli haramu au ukiukaji wa sheria, kwa mfano, kutoa maagizo ya kutengeneza au kupata bidhaa au huduma haramu au zinazodhibitiwa.
- Yanakiuka haki za wengine, ikiwa ni pamoja na haki za faragha na za uvumbuzi, kwa mfano, kutumia data binafsi au taarifa za kibayometri bila kibali kinachohitajika kisheria.
- Yanamfuatilia au kumchunguza mtu bila idhini yake.
- Yanafanya maamuzi ya kiotomatiki bila usimamizi wa binadamu na kuathiri vibaya haki ya mtu binafsi katika sekta muhimu sana, kwa mfano, katika ajira, huduma za afya, fedha, kisheria, makazi, bima au ustawi wa jamii.
- Usihatarishe usalama wa wengine au wa huduma za Google. Hii ni pamoja na kutayarisha au kusambaza maudhui ambayo yanawezesha:
- Taka, wizi wa data binafsi au programu hasidi.
- Kutumia vibaya, kudhuru, kukatiza au kuvuruga miundombinu au huduma za Google au za wengine.
- Kukwepa ulinzi dhidi ya matumizi mabaya au vichujio vya usalama, kwa mfano, kuchezea mfumo huo ili kukiuka sera zetu.
- Usijihusishe katika shughuli dhahiri za kingono, vurugu, chuki au zinazosababisha madhara. Hii ni pamoja na kutayarisha au kusambaza maudhui ambayo yanawezesha:
- Chuki au matamshi ya chuki.
- Unyanyasaji, uchokozi, vitisho, kuwadhulumu au kuwatusi wengine.
- Vurugu au uchochezi wa vurugu.
- Maudhui dhahiri ya ngono, kwa mfano, maudhui yaliyoandaliwa kwa madhumuni ya ponografia au kujiridhisha kingono.
- Usijihusishe na taarifa zisizo kweli, uwakilishi wa uongo au shughuli za kupotosha. Hii ni pamoja na
- Ulaghai au vitendo vingine vya udanganyifu.
- Kuiga mtu (aliye hai au aliyefariki) bila kubainisha hilo wazi, ili kuhadaa.
- Kuwezesha madai ya kupotosha kuhusu utaalamu au ujuzi katika masuala nyeti, kwa mfano katika afya, fedha, huduma za serikali au sheria ili kudanganya.
- Kuwezesha madai yanayopotosha kuhusu michakato ya kiserikali au ya kidemokrasia au shughuli hatari za kiafya, ili kuhadaa.
- Kuwapotosha wengine kuhusu maudhui yaliyotayarishwa kwa kutumia AI kwa kudai yaliandaliwa na binadamu pekee, ili kuhadaa.
Tunaweza kuweka hali zisizofuata kanuni kwa sera hizi kwa kuzingatia malengo ya kielimu, kihalisia, kisayansi, au kisanii, au ambapo madhara ni machache zaidi kuliko manufaa kwa umma.