Sera ya Matumizi Yasiyokubalika ya AI Inayoweza Kuandaa

Mara ya Mwisho Kubadilishwa: 14 Machi 2023

Mifumo ya AI Inayoweza Kuandaa inaweza kukusaidia kugundua mada mpya, kuchochea ubunifu wako na kujifunza mambo mapya. Hata hivyo, tunatarajia utumie mifumo hiyo kwa kuwajibika, na kwa kuzingatia sheria. Hivyo basi, huruhusiwi kutumia Huduma za Google zinazodhibitiwa chini ya sera hii kufanya yafuatayo:

  1. Kutekeleza au kuwezesha shughuli hatari, hasidi, au zisizo halali, ikiwemo
    1. Kuwezesha au kuendeleza ukiukaji wa sheria au shughuli zisizo halali, kama vile
      1. Kuandaa au kushiriki maudhui yanayohusiana na dhuluma au unyanyasaji wa watoto kingono
      2. Kutangaza au kuwezesha mauzo ya, au kutoa maagizo ya kutengeneza au kupata, bidhaa au huduma haramu
      3. Kuwezesha au kuhimiza watumiaji kutenda uhalifu wowote
      4. Kuandaa au kushiriki maudhui ya vurugu iliyokithiri au ya kigaidi
    2. Matumizi mabaya, kudhuru, kutatiza, au kukatiza huduma (au kuwawezesha wengine kufanya hivyo), kama vile
      1. Kuhimiza au kuwezesha uundaji au usambazaji wa taka
      2. Kuandaa maudhui kwa madhumuni ya shughuli za udanganyifu, ulaghai, wizi wa data binafsi, au programu hasidi.
    3. Kujaribu kubatilisha au kukwepa vichujio vya usalama au kuelekeza mfumo kutekeleza kitendo kinachokiuka sera zetu.
    4. Kuandaa maudhui yanayoweza kudhuru au kusababisha madhara kwa watu binafsi au kikundi, kama vile
      1. Kuandaa maudhui yanayochochea au yanayohimiza chuki
      2. Kuwezesha unyanyasaji au uchokozi ili kuwatisha, kuwanyanyasa au kuwadhalilisha wengine
      3. Kutayarisha maudhui yanayowezesha, yanayoendeleza, au yanayochochea vurugu
      4. Kutayarisha maudhui yanayowezesha, yanayoendeleza, au yanayochochea mtu kujijeruhi
      5. Kuandaa taarifa inayomtambulisha mtu kwa lengo la kusambaza au kusababisha madhara mengine
      6. Kumfuatilia au kumchunguza mtu bila idhini yake
      7. Kuandaa maudhui yanayoweza kumwathiri mtu vibaya, hasa kuhusiana na sifa nyeti au zinazolindwa
  2. Kutayarisha na kushiriki maudhui ya uongo, ya kupotosha, au yasiyo ya kweli, ikiwemo
    1. Kuwapotosha wengine kuhusu chanzo cha maudhui kwa kudai maudhui yaliandaliwa na binadamu, au kudai umiliki wa maudhui, ili kuhadaa
    2. Kuandaa maudhui ya kuiga mtu (aliye hai au aliyefariki) bila kubainisha hilo wazi, ili kuhadaa
    3. Kutoa madai ya kupotosha kuhusu utaalamu au ujuzi hasa kuhusiana na masuala nyeti (k.m. afya, fedha, huduma za serikali, au masuala ya sheria)
    4. Kutumia mfumo kufanya maamuzi kiotomatiki kwa masuala yanayoathiri maslahi au haki za mtu binafsi (k.m., fedha, sheria, ajira, afya, makazi, bima na ustawi wa kijamii)
  3. Kuandaa maudhui dhahiri ya ngono, ikijumuisha maudhui yaliyotayarishwa kwa madhumuni ya ponografia au ngono (k.m. programu inayopiga gumzo kuhusu ngono). Kumbuka, hii haijumuishi maudhui yaliyotayarishwa kwa madhumuni ya kisayansi, kielimu, kisanii, au matukio halisia.
Programu za Google
Menyu kuu