Google hulindaje faragha yangu na kuweka maelezo yangu yakiwa salama?

Tunajua usalama na faragha ni muhimu kwako - na ni muhimu kwetu, pia. Tunalipatia suala la kuwa na usalama dhabiti kipaumbele na kukupa imani ya kwamba maelezo yako ni salama na utayapata unapoyahitaji.

Tunaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama dhabiti, kulinda faragha yako na kufanya Google kukufaa na kukupa ufanisi zaidi. Kila mwaka tunatumia mamilioni ya dola kwa suala la usalama, na kuajiri wataalamu mashuhuri duniani katika usalama wa data ili kuweka maelezo yako salama. Pia tuliunda zana rahisi kutumia za faragha na usalama kama Dashibodi ya Google, uthibitishaji wa hatua mbili na Mipangilio ya Matangazo. Kwa hivyo, unadhibiti maelezo unayoshiriki na Google.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu ulinzi na usalama mtandaoni, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kujilinda mwenyewe na familia yako mtandaoni, katika Kituo cha Usalama cha Google .

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyoweka maelezo yako ya kibinafsi yakiwa ya faragha na salama — na kukuweka kwenye usukani.

Ninawezaje kuondoa maelezo kunihusu kutoka matokeo ya utafutaji ya Google?

Matokeo ya utafutaji Google ni mfano wa maudhui yanayopatikana na umma kwenye wavuti. Mitambo ya kutafuta haiwezi kuondoa maudhui moja kwa moja kutoka kwa tovuti, kwa hivyo kuondoa matokeo ya utafutaji kutoka Google hakuwezi kuondoa maudhui kwenye tovuti. Ikiwa unataka kuondoa chochote kwenye wavuti, unafaa kuwasiliana na msimamizi wa wavuti wa tovuti ambayo maelezo yamechapishwa na umuulize abadilishe. Maudhui yanapoondolewa na Google imetambua mabadiliko, maelezo hayatapatikana katika matokeo ya utafutaji ya Google. Kama una ombi la dharura la kuondoa maudhui, unaweza pia kutembelea ukurasa wetu wa usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Je, hoja zangu za utafutaji hutumwa kwenye tovuti ninapobofya matokeo kwenye huduma ya Tafuta na Google?

Ndiyo, katika hali fulani. Unapobofya matokeo ya utafutaji katika huduma ya Tafuta na Google, huenda pia kivinjari chako kikatuma anwani ya Intaneti, au URL, ya ukurasa wa matokeo ya utafutaji kwenye ukurasa lengwa wa wavuti kama URL Iliyoelekeza. Wakati mwingine URL ya ukurasa wa matokeo ya utafutaji inaweza kuwa na hoja uliyoweka ya utafutaji. Ikiwa unatumia Utafutaji wa SSL (kipengele cha Google cha kutafuta kwa usimbaji fiche), mara nyingi, hoja uliyotafuta haitatumwa kama sehemu ya URL katika URL Iliyoelekeza. Kuna baadhi ya hali zisizofuata mkondo huu, kama vile, ikiwa unatumia vivinjari visivyo maarufu sana. Maelezo zaidi kuhusu Utafutaji wa SSL yanaweza kupatikana hapa. Hoja za utafutaji au maelezo yaliyo katika URL Iliyoelekeza yanaweza kupatikana kupitia Google Analytics au kiolesura cha kusanifu programu (API). Aidha, watangazaji wanaweza kupokea maelezo yanayohusiana na maneno muhimu yaliyowafanya watumiaji wabofye tangazo.

Programu za Google
Menyu kuu