Kudhibiti vidakuzi katika kivinjari chako

Baadhi ya watu wanapendelea kutoruhusu vidakuzi, ndiyo sababu vivinjari vingi vinakupa uwezo wa kudhibiti vidakuzi ili kukufaa.

Baadhi ya vivinjari huzuia au kufuta vidakuzi, kwa hivyo unahitaji kukagua mipangilio yako ya vidakuzi na mipangilio ya matangazo. Katika baadhi ya vivinjari unaweza kusanidi kanuni ili kudhibiti vidakuzi katika msingi wa tovuti kwa tovuti, na kukupa udhibiti laini zaidi wa faragha yako. Hii inamaanisha kwamba unaweza kutoruhusu vidakuzi kutoka kwa tovuti zote isipokuwa zile ambazo unaamini.

Katika kivinjari cha Google Chrome, menyu ya Zana ina chaguo la Ondoa Data ya Kuvinjari. Unaweza kutumia chaguo hili kufuta vidakuzi na data nyingine ya tovuti na programu-jalizi, pamoja na data iliyohifadhiwa kwenye kifaa chako na Adobe Flash Player (ijulikanayo kama vidakuzi vya Flash). Ona maagizo yetu ya kudhibiti vidakuzi katika Chrome.

Kipengele kingine cha Chrome ni hali yake fiche. Unaweza kuvinjari katika hali fiche wakati hutaki ziara zako za tovuti au vipakuzi zirekodiwa katika historia yako ya kuvinjari na kupakua. Vidakuzi vyovyote vilivyoundwa wakati wa hali fiche hufutwa baada ya kufunga madirisha yote fiche.