Aina ya vidakuzi vinavyotumiwa na Google

Tunatumia aina tofauti za kidakuzi kuendesha tovuti za Google na bidhaa zinazohusika na matangazo. Baadhi au vidakuzi vyote vilivyotambulishwa hapa chini vinaweza kuhifadhiwa katika kivinjari chako. Unaweza kutazama na kudhibiti vidakuzi katika kivinjari chako(ingawa vivinjari vya simu za mkononi vinaweza kosa kutoa mwonekano huu).

Aina ya matumiziMfano

Mapendeleo

Vidakuzi hivi huruhusu tovuti zetu kukumbuka maelezo ambayo yanabadilisha jinsi tovuti inavyotenda au kuonekana, kama vile lugha unayopendelea au eneo uliopo. Kwa mfano, kwa kukumbuka eneo lako, tovuti inaweza kukupa ripoti za hali ya hewa ya eneo lako au habari za trafiki. Vidakuzi hivi pia vinaweza kukusaidia kubadilisha ukubwa wa maandishi, fonti na sehemu nyingine za kurasa za wavuti ambazo unaweza kuweka mapendeleo.

Kupotea kwa maelezo yaliyohifadhiwa katika kidakuzi cha mapendeleo kunaweza kufanya zoezi la tovuti kuwa na utendaji wa chini lakini haifai kuizuia kufanya kazi.

Watumiaji wengi wa Google watakuwa na kidakuzi cha mapendeleo kiitwacho 'NID' katika vivinjari vyao. Kivinjari hutuma kidakuzi hiki na maombi kwa tovuti za Google. Kidakuzi cha NID kina kitambulisho cha kipekee ambacho Google hutumia kukumbuka mapendeleo na maelezo yako mengine, kama vile lugha unayopendelea (k.m. Kiingereza), matokeo mangapi ya utafutaji ungependa kuonyeshwa kwa kila ukurasa (k.m. 10 au 20), na kama ungependa au hungependa kuwasha kichujio cha Google SafeSearch.

Usalama

Tunatumia vidakuzi vya usalama ili kuthibitisha watumiaji, kuzuia utumizi wa ulaghai wa vitambulisho vya kuingia, na kulinda data ya mtumiaji kutoka kwa wengine ambao hawajaidhinishwa.

Kwa mfano, sisi hutumia vidakuzi vinavyoitwa 'SID' na 'HSID' ambavyo vina rekodi zilizotiwa saini kitarakimu na zilizosimbwa kwa njia fiche za kitambulisho cha akaunti ya Google ya mtumiaji na wakati wa hivi karibuni wa kuingia. Muunganisho wa vidakuzi hivi viwili huturuhusu kuzuia aina nyingi za shambulio, kama vile majaribio ya kuiba maudhui ya fomu ambazo unakamilisha kwenye kurasa za wavuti.

Michakato

Vidakuzi vya mchakato husaidia tovuti ifanye kazi na kuwasilisha huduma ambazo mgeni wa tovuti anatarajia, kama kuabiri kurasa za wavuti au kufikia maeneo salama ya wavuti. Bila vidakuzi hivi, tovuti haiwezi kufanya kazi vizuri.

Kwa mfano, sisi hutumia kidakuzi kiitwacho 'Ibcs' ambacho kinaifanya Google Docs kuweza kufungua Nyaraka nyingi katika kivinjari kimoja. Kuzuia kidakuzi hiki kunaweza kuzuia Google Docs kutenda kazi vizuri.

Matangazo

Tunatumia vidakuzi ili kufanya utangazaji uwahusishe zaidi watumiaji na uwe wa thamani zaidi kwa wachapishaji na watangazaji. Baadhi ya programu za kawaida za vidakuzi huchagua utangazaji kulingana na ni nini muhimu kwa mtumiaji, ili kuboresha kuripoti utendaji wa kampeni na kuzuia kuonyesha matangazo ambayo mtumiaji tayari ameona.

Google hutumia vidakuzi kama NID na SID kusaidia kubadilisha matangazo kukufaa kwenye huduma za Google, kama vile huduma ya Tafuta na Google. Kwa mfano, sisi hutumia vidakuzi kama hivi ili kukumbuka utafutaji wako wa hivi karibuni, mawasiliano yako ya awali na matangazo ya mtangazaji au matokeo ya utafutaji, na ziara zako kwa tovuti ya mtangazaji. Hii hutusaidia kukuonyesha matangazo yaliyobadilishwa kukufaa kwenye Google.

Sisi pia hutumia vidakuzi kwenye matangazo tunayotoa kote kwenye wavuti. Mojawapo ya kidakuzi chetu kikuu cha utangazaji kwenye tovuti zisizo za Google kinaitwa ‘IDE‘ na kinahifadhiwa kwenye vivinjari chini ya kikoa cha doubleclick.net. Kingine kinahifadhiwa katika google.com na kinaitwa ANID. Tunatumia vidakuzi vingine na majina kama vile DSID, FLC, AID, TAID, na exchange_uid. Huduma nyingine za Google kama vile YouTube, huenda pia zikatumia vidakuzi ili kukuonyesha matangazo yanayokufaa zaidi.

Wakati mwingine, vidakuzi vya utangazaji vinaweza kuwekwa kwenye kikoa cha tovuti unayotembelea. Kwa matangazo tunayoonyesha kote katika wavuti, vidakuzi (k.m, vidakuzi vinavyoitwa ‘__gads’ au ‘__gac’) vinaweza kuwekwa kwenye kikoa cha tovuti unayotembelea. Tofauti na vidakuzi ambavyo huwekwa kwenye vikoa mahususi vya Google, vidakuzi hivi haviwezi kusomwa na Google ukiwa kwenye tovuti nyingine tofauti na ile ambayo vidakuzi hivi vimewekwa. Vidakuzi hivi vinafanya kazi kama vile kupima utumiaji wa matangazo kwenye kikoa hicho na kuzuia usionyeshwe matangazo yale yale mara nyingi mno.

Google pia hutumia vidakuzi vya kushawishika (k.m, vidakuzi vinavyoitwa ‘__gcl’), ambavyo lengo lake kuu ni kuwasaidia watangazaji kubaini mara ambazo watu wanaobofya matangazo yao hushawishika kuchukua hatua katika tovuti zao (k.m, kufanya ununuzi). Vidakuzi hivi huruhusu Google na mtangazaji kutambua kwamba ulibofya tangazo na baadaye ukatembelea tovuti ya mtangazaji. Vidakuzi vya kushawishika havitumiwi na Google katika ulengaji wa matangazo maalum na hudumu kwa muda mfupi tu. Baadhi ya vidakuzi vyetu vingine vinaweza pia kutumiwa kupima matukio ya kushawishika. Kwa mfano, Vidakuzi vya Google Marketing Platform na Google Analytics vinaweza pia kutumika kwa madhumuni haya.

Pia tunatumia vidakuzi viitwavyo ‘AID,‘ ‘DSID,’ na ‘TAID‘, ambavyo hutumiwa kuunganisha shughuli zako kwenye vifaa vyote, ikiwa uliingia awali katika akaunti yako ya Google kwa kutumia kifaa kingine. Sisi hufanya hivi ili kuratibu matangazo unayoyaona kwenye vifaa vyote na kutathmini matukio ya kushawishika. Vidakuzi hivi vinaweza kuwekwa kwenye vikoa vya google.com/ads, google.com/ads/measurement, au googleadservices.com. Ikiwa hutaki matangazo unayoyaona yaratibiwe kwenye vifaa vyako vyote, unaweza kuchagua kutopokea Matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia kwa kutumia Mipangilio ya Matangazo.

Hali ya Kipindi

Mara nyingi tovuti hukusanya maelezo kuhusu jinsi watumiaji hutumia tovuti. Hii inaweza kujumuisha kurasa ambazo watumiaji hutembelea mara nyingi, na ikiwa watumiaji hupata ujumbe wa hitilafu kutoka kwenye kurasa fulani. Tunatumia vidakuzi vijulikanavyo kama 'vidakuzi vya hali ya kipindi' ili kutusaidia kuboresha huduma zetu, ili kuboresha zoezi la kuvinjari la watumiaji wetu. Kuzuia au kufuta vidakuzi hivi hakutafanya tovuti isiweze kutumika.

Vidakuzi hivi vinaweza pia kutumiwa kupima bila kutambulisha, ufanisi wa PPC (lipa kwa mbofyo) na utangazaji wa kushirikishwa.

Kwa mfano, tunatumia kidakuzi kinachoitwa 'recently_watched_video_id_list' ili YouTube iweze kurekodi video zilizotazamwa hivi karibuni na kivinjari fulani.

Uchanganuzi

Google Analytics ni zana ya uchanganuzi kutoka Google ambayo husaidia wamiliki wa tovuti na programu waelewe jinsi wageni wao wanavyotumia tovuti na programu zao. Inaweza kutumia kundi la vidakuzi kukusanya maelezo na kuripoti takwimu za matumizi ya tovuti bila kutambulisha wageni mahususi kwenye Google. Kidakuzi kikuu kinachotumiwa na Google Analytics ni ‘_ga’.

Mbali na kuripoti takwimu za matumizi ya tovuti, data inayokusanywa na Google Analytics kwenye huduma za Google inaweza pia kutumiwa, pamoja na baadhi ya vidakuzi vya utangazaji vilivyoelezewa hapa juu, ili kusaidia kuonyesha matangazo yanayokufaa zaidi kwenye huduma za Google (kama vile Tafuta na Google) na kote kwenye wavuti na kupima utumiaji wa matangazo tunayoonyesha.

Pata maelezo zaidi kuhusu Vidakuzi vya uchanganuzi na maelezo ya faragha.

Tunatumia vikoa mbalimbali kuweka vidakuzi vinavyotumiwa katika bidhaa zetu za matangazo, ikiwa ni pamoja na vikoa vifuatavyo na matoleo machache maalum kwa nchi mahususi ya vikoa hivi (kama vile google.fr):

 • admob.com
 • adsensecustomsearchads.com
 • adwords.com
 • doubleclick.net
 • google.com
 • googleadservices.com
 • googleapis.com
 • googlesyndication.com
 • googletagmanager.com
 • googletagservices.com
 • googletraveladservices.com
 • googleusercontent.com
 • google-analytics.com
 • gstatic.com
 • urchin.com
 • youtube.com
 • ytimg.com