Hili ni toleo lililohifadhiwa la Sera yetu ya Faragha. Tazama toleo la sasa au matoleo yote ya awali.

Sera ya Faragha ya Google

Unapotumia huduma zetu, unaamini kuwa tutalinda maelezo yako. Tunaelewa kuwa hili ni jukumu kubwa na tunafanya tuwezalo ili kulinda maelezo yako na kuhakikisha kuwa unaweza kuyadhibiti.

Sera hii ya Faragha imekusudiwa kukusaidia uelewe maelezo tunayokusanya, sababu za kuyakusanya na jinsi unavyoweza kusasisha, kudhibiti, kuhamisha na kufuta maelezo yako.

Ukaguzi wa Faragha

Ungependa kubadilisha mipangilio yako ya faragha?

Fanya Ukaguzi wa Faragha

Inatumika kuanzia 1 Julai 2021 | Matoleo yaliyowekwa kwenye kumbukumbu | Pakua PDF

Tunaunda huduma mbalimbali zinazosaidia mamilioni ya watu kuwasiliana na kufahamu yanayotukia ulimwenguni kote kila siku kwa njia mpya. Huduma zetu zinajumuisha:

  • Programu, tovuti na vifaa vya Google kama vile Tafuta na Google, YouTube na Google Home
  • Mifumo kama vile kivinjari cha Chrome na mfumo wa uendeshaji wa Android
  • Bidhaa ambazo zinatumiwa na programu na tovuti nyingine, kama vile matangazo na Ramani za Google zilizopachikwa

Unaweza kutumia huduma zetu kwa njia mbalimbali kudhibiti faragha yako. Kwa mfano, unaweza kufungua Akaunti ya Google ikiwa ungependa kuunda na kudhibiti maudhui kama vile barua pepe na picha, au kuona matokeo ya utafutaji yanayokufaa. Unaweza pia kutumia huduma nyingi za Google ukiwa umeondoka katika akaunti au hata ukiwa huna akaunti kama vile kutafuta kwenye Google au kutazama video kwenye YouTube. Pia, unaweza kuvinjari wavuti kwa faragha katika Hali fiche ukitumia Chrome. Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya faragha kwenye huduma zetu zote ili udhibiti maelezo yako tunayokusanya na tunavyoyatumia.

Ili tuweze kufafanua mambo wazi kabisa, tumejumuisha mifano, video zenye maelezo na ufafanuzi wa masharti muhimu. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Sera hii ya Faragha, wasiliana nasi.

Maelezo ambayo Google hukusanya

Tungependa ujue maelezo tunayokusanya unapotumia huduma zetu

Sisi hukusanya maelezo ili kutoa huduma bora kwa watumiaji wetu wote — kutoka kubashiri vitu vya msingi kama vile lugha unayozungumza, hadi vitu changamani zaidi kama vile matangazo yanayokufaa, watu muhimu sana kwako mtandaoni, au video ambazo huenda utapenda kwenye YouTube. Maelezo yanayokusanywa na Google na jinsi yanavyotumika inategemea unavyotumia huduma zetu na unavyodhibiti vidhibiti vyako vya faragha.

Ikiwa hujaingia katika Akaunti ya Google, sisi huhifadhi maelezo ambayo tumekusanya kwa kutumia vitambulishaji vya kipekee vilivyojumuishwa ndani ya kivinjari chako, programu au kifaa unachotumia. Hii inatusaidia kutekeleza mambo kama vile kudumisha lugha unayopendelea unapovinjari kokote.

Ukiwa umeingia katika akaunti, sisi hukusanya pia maelezo tunayohifadhi kwenye Akaunti yako ya Google na tunayachukulia kuwa maelezo ya binafsi.

Maudhui unayounda au kutupa

Unapofungua Akaunti ya Google, unatupa maelezo ya binafsi yanayojumuisha jina na nenosiri lako. Unaweza pia kuongeza nambari ya simu au maelezo ya malipo kwenye akaunti yako. Hata ikiwa hujaingia katika Akaunti ya Google, unaweza kutupa maelezo — kama vile anwani ya barua pepe ili upokee taarifa kuhusu huduma zetu.

Sisi pia hukusanya maudhui unayounda, unayopakia, au kupokea kutoka kwa watu wengine unapotumia huduma zetu. Hii inajumuisha vipengee kama vile barua pepe unazotuma na kupokea, picha na video unazohifadhi, hati na malahajedwali unayounda na maoni unayotoa kwenye video za YouTube.

Maelezo tunayokusanya unapotumia huduma zetu

Programu, vivinjari na vifaa vyako

Google hukusanya maelezo kuhusu programu, vivinjari na vifaa unavyotumia kufikia huduma zake. Hii hutusaidia kutoa vipengele kama vile masasisho ya kiotomatiki ya bidhaa na kipengele cha kupunguza ung'avu wa skrini ikiwa betri yako inakaribia kuisha chaji.

Maelezo tunayokusanya ni pamoja na vitambulishaji vya kipekee, aina na mipangilio ya kivinjari, aina na mipangilio ya vifaa, mfumo wa uendeshaji, maelezo ya mtandao wa simu ikiwa ni pamoja na jina la mtoa huduma na nambari ya simu na nambari ya toleo la programu. Sisi hukusanya pia maelezo kuhusu mawasiliano kati ya programu, vivinjari na vifaa vyako na huduma zetu, ikiwemo Anwani ya IP, ripoti za kuacha kufanya kazi, shughuli za mfumo na tarehe, saa na URL ya kuelekeza ya ombi lako.

Tunakusanya maelezo haya wakati huduma ya Google kwenye kifaa chako inawasiliana na seva zetu - kwa mfano, unaposakinisha programu kutoka kwenye Google Play au wakati huduma inatafuta masasisho ya kiotomatiki. Ikiwa unatumia Kifaa cha Android chenye programu za Google, kifaa chako kitawasiliana na seva za Google mara kwa mara kutoa maelezo ya kifaa na muunganisho kwenye huduma zetu. Maelezo haya yanajumuisha mambo kama vile, aina ya kifaa chako, jina la mtoa huduma, ripoti za kuacha kufanya kazi na programu ulizosakinisha.

Shughuli zako

Sisi hukusanya maelezo ya shughuli zako kwenye huduma zetu. Maelezo haya hutumika kutekeleza mambo kama vile kukupendekezea video ambazo huenda ukapenda kwenye YouTube. Maelezo ya shughuli tunayokusanya yanajumuisha:

Ukitumia huduma zetu kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe, tunaweza kukusanya maelezo ya kumbukumbu ya simu na ujumbe kama vile nambari ya simu, nambari ya anayekupigia, nambari ya unayempigia, nambari za kusambaza simu, anwani ya barua pepe ya anayetuma na anayepokea, saa na tarehe za simu na ujumbe, muda wa kuongea kwenye simu, maelezo ya kuelekezwa kwa simu na aina na idadi ya simu na ujumbe.

Unaweza kutembelea Akaunti ya Google ili upate na kudhibiti maelezo ya shughuli ambayo yamehifadhiwa katika akaunti yako.

Nenda kwenye Akaunti ya Google

Maelezo mahali ulipo

Tunakusanya maelezo ya mahali ulipo unapotumia huduma zetu. Maelezo haya hutusaidia kutoa vipengele kama vile ramani ya kukuelekeza unapoendesha gari kwa mapumziko ya wikendi au kukuarifu kuhusu filamu zinazochezwa karibu nawe.

Mahali ulipo panaweza kukadiriwa kwa kutumia:

Aina za data ya mahali tunazokusanya zinategemea kwa kiwango fulani mipangilio ya kifaa na akaunti yako. Kwa mfano, unaweza kuwasha au kuzima kipengele cha mahali kwenye kifaa chako cha Android ukitumia programu ya mipangilio ya kifaa. Unaweza pia kuwasha kipengele cha Kumbukumbu ya Maeneo Yangu ikiwa ungependa kuunda ramani ya faragha ya unakokwenda ukiwa na vifaa vyako ambavyo umetumia kuingia katika akaunti.


Katika hali fulani, Google pia hukusanya taarifa kukuhusu kutoka kwenye nyenzo zinazopatikana hadharani. Kwa mfano, ikiwa jina lako limeandikwa kwenye gazeti la eneo uliko, mtambo wa kutafuta kwenye Google unaweza kuainisha makala hayo na kuyaonyesha kwa watu wengine wakitafuta jina lako. Tunaweza pia kukusanya taarifa kukuhusu kutoka kwa washirika wanaoaminika, kama vile huduma za saraka, ambao hutupa maelezo ya biashara yatakayoonyeshwa kwenye huduma za Google; washirika wa biashara ambao hutupa maelezo kuhusu wateja watarajiwa wa huduma zetu za biashara; na washirika wa usalama ambao hutupa maelezo ili kulinda dhidi ya matumizi mabaya. Tunapokea pia maelezo kutoka kwa watangazaji ili kutoa huduma za utangazaji na utafiti kwa niaba yao.

Tunatumia teknolojia mbalimbali kukusanya na kuhifadhi maelezo, vikiwemo vidakuzi, lebo za pikseli, hifadhi za ndani kama vile hifadhi ya kivinjari au akiba za data ya programu, hifadhidata na kumbukumbu za seva.

Sababu ya Google kukusanya data

Tunatumia data tunayokusanya kuboresha huduma

Tunatumia maelezo tunayokusanya kutoka kwenye huduma zetu zote kwa madhumuni yafuatayo:

Kutoa huduma zetu

Tunatumia maelezo yako kutoa huduma zetu, kama vile kuchakata hoja unazotafuta ili kukupa matokeo au kukusaidia kushiriki maudhui kwa kukupendekezea wapokeaji kati ya watu unaowasiliana nao.

Kudumisha na kuboresha huduma zetu

Pia tunatumia maelezo yako kuhakikisha kuwa huduma zetu zinafanya kazi ipasavyo, kama vile kufuatilia hitilafu au kutatua matatizo unayoripoti kwetu. Tunatumia pia maelezo yako kuboresha huduma zetu — kwa mfano, kutambua hoja za utafutaji ambazo huendelezwa visivyo mara nyingi kunatusaidia kuboresha vipengele vya kikagua maendelezo vinavyotumika katika huduma zetu zote.

Kuunda huduma mpya

Tunatumia maelezo tunayokusanya katika huduma zilizopo kutusaidia kuunda huduma mpya. Kwa mfano, baada ya kuelewa jinsi watu wanavyopanga picha zao katika programu ya Picasa ambayo ndiyo programu ya kwanza ya picha ya Google, tuliweza kuunda na kuanzisha programu ya Picha kwenye Google.

Kutoa huduma zinazokufaa, ikiwa ni pamoja na maudhui na matangazo

Tunatumia maelezo tunayokusanya ili kukupa huduma zinazokufaa, ikiwemo kukupa mapendekezo, maudhui na matokeo ya utafutaji yanayokufaa. Kwa mfano, Ukaguzi wa Usalama hukupa vidokezo vya usalama kutokana na jinsi unavyotumia bidhaa za Google. Google Play hutumia maelezo kama vile programu ambazo umesakinisha na video ulizotazama kwenye YouTube kukupendekezea programu ambazo huenda ukapenda.

Kutegemea mipangilio yako, tunaweza pia kukuonyesha matangazo yanayokufaa kulingana na mambo yanayokuvutia. Kwa mfano, ukitafuta "baiskeli za kupanda milima," unaweza kuona tangazo la vifaa vya michezo unapovinjari tovuti inayoonyesha matangazo kutoka Google. Unaweza kudhibiti maelezo tunayotumia kukuonyesha matangazo kwenye mipangilio yako ya matangazo.

  • Hatutumii vigezo nyeti, kama vile rangi, dini, mwelekeo wa ngono au afya kukuonyesha matangazo yanayokufaa.
  • Hatukuonyeshi matangazo yaliyowekewa mapendeleo kulingana na maudhui yako kutoka huduma za Hifadhi, Gmail au Picha.
  • Hatushiriki maelezo yako yanayokutambulisha binafsi kwa watangazaji kama vile jina au anwani yako ya barua pepe isipokuwa utuombe kufanya hivyo. Kwa mfano, ukiona tangazo la duka la maua lililo karibu nawe kisha uchague "gusa ili upige simu", tutaunganisha simu yako na tunaweza kushiriki nambari yako ya simu na duka hilo la maua.

Nenda kwenye Mipangilio ya Matangazo

Pima utendaji

Tunatumia data kwa uchanganuzi na upimaji ili kujua jinsi huduma zetu zinavyotumiwa. Kwa mfano, tunachanganua data kuhusu mara ambazo umetembelea tovuti zetu kufanya mambo kama vile kuboresha muundo wa bidhaa. Pia, tunatumia data kuhusu matangazo unayoangalia ili kuwasaidia watangazaji wajue utendaji wa kampeni za matangazo yao. Katika kutekeleza hili, tunatumia zana mbalimbali ikiwemo Google Analytics. Unapotembelea tovuti zinazotumia Google Analytics, mteja wa Google Analytics anaweza kuchagua kuruhusu Google iunganishe maelezo yanayohusu shughuli zako kutoka kwenye tovuti hiyo na shughuli kutoka kwenye tovuti nyingine zinazotumia huduma zetu za matangazo.

Kuwasiliana nawe

Tunatumia maelezo yako tunayokusanya, kama vile anwani yako ya barua pepe ili kuwasiliana nawe moja kwa moja. Kwa mfano, tunaweza kukuarifu tunapogundua shughuli za kutiliwa shaka kama vile jaribio la kuingia katika Akaunti yako ya Google kutoka mahali ambapo si pa kawaida. Au tunaweza kukujulisha kuhusu mabadiliko au maboresho yajayo kwenye huduma zetu. Na unapowasiliana na Google, tutaweka rekodi ya ombi lako ili tukusaidie kutatua tatizo lolote unalokumbana nalo.

Kulinda Google, watumiaji wetu na umma

Tunatumia maelezo kuboresha usalama na uaminifu wa huduma zetu. Hii ni pamoja na kuchunguza, kuzuia na kukabiliana na ulaghai, matumizi mabaya, hatari na matatizo ya kiufundi ambayo yanaweza kuathiri Google, watumiaji wetu, au umma.


Tunatumia teknolojia tofauti kuchakata maelezo yako kwa madhumuni haya. Tunatumia mifumo ya kiotomatiki ambayo huchanganua maudhui yako ili kukupa huduma kama vile matokeo ya utafutaji yaliyoboreshwa, matangazo yanayokufaa au vipengele vingine kulingana na jinsi unavyotumia huduma zetu. Tunachanganua pia maudhui yako ili tuweze kugundua matumizi mabaya kama vile barua taka, programu hasidi na maudhui yasiyo halali. Pia tunatumia algoriti ili kutambua ruwaza katika data. Kwa mfano, Tafsiri na Google huwasaidia watu wa lugha tofauti kuwasiliana kwa kuchunguza ruwaza za kawaida za lugha katika vifungu vya maneno ambavyo ungependa itafsiri.

Tunaweza kuweka pamoja maelezo tunayokusanya katika huduma zetu na kwenye vifaa vyako vyote kwa madhumuni yaliyoelezwa hapo juu. Kwa mfano, ukitazama video za wachezaji wa gitaa kwenye YouTube, unaweza kuona tangazo la mafunzo ya gitaa kwenye tovuti inayotumia bidhaa zetu za matangazo. Kulingana na mipangilio ya akaunti yako, shughuli zako kwenye programu na tovuti nyingine zinaweza kuhusishwa na maelezo yako ya binafsi ili kuboresha huduma za Google na matangazo kutoka Google.

Ikiwa watumiaji wengine tayari wana anwani yako ya barua pepe au maelezo yako mengine ya binafsi, tunaweza kuwaonyesha maelezo yako ya Akaunti ya Google yanayoonekana kwa umma, kama vile jina na picha yako. Kwa mfano, hatua hii huwasaidia watu kutambua barua pepe inayotoka kwako.

Tutaomba idhini yako kabla ya kutumia maelezo yako kwa madhumuni ambayo hayajatajwa katika Sera hii ya Faragha.

Vidhibiti vyako vya faragha

Unaweza kuchagua maelezo tunayoweza kukusanya na jinsi tunavyoyatumia

Sehemu hii inafafanua vidhibiti muhimu vya kudhibiti faragha yako katika huduma zetu zote. Unaweza pia kutembelea Ukaguzi wa Faragha, ambapo utaweza kukagua na kubadilisha mipangilio muhimu ya faragha. Mbali na zana hizi, tunatoa pia mipangilio maalum ya faragha katika bidhaa zetu - unaweza kupata maelezo zaidi kwenye Mwongozo wetu wa Faragha ya Bidhaa.

Nenda kwenye Ukaguzi wa Faragha

Kudhibiti, kukagua na kusasisha maelezo yako

Ukiwa umeingia katika akaunti, unaweza kukagua na kusasisha maelezo wakati wowote kwa kutembelea huduma unazotumia. Kwa mfano, Picha kwenye Google na Hifadhi ya Google zimeundwa ili kukusaidia kudhibiti aina mahususi za maudhui ambayo umehifadhi kwenye Google.

Pia unaweza kukagua na kudhibiti maelezo yaliyohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google. Akaunti yako ya Google inajumuisha:

Vidhibiti vya faragha

Vidhibiti vya Shughuli

Teua aina za shughuli ambazo ungependa kuhifadhi katika akaunti yako. Kwa mfano, unaweza kuwasha kipengele cha Kumbukumbu ya Maeneo Yangu ikiwa ungependa kupata ubashiri wa hali ya trafiki kila siku, au unaweza kuhifadhi Historia ya Video Ulizotazama kwenye YouTube ili upate mapendekezo ya video zinazokufaa.

Nenda kwenye Vidhibiti vya Shughuli

Mipangilio ya matangazo

Dhibiti mapendeleo yako ya matangazo unayoona kwenye Google na kwenye tovuti na programu zinazoshirikiana na Google kuonyesha matangazo. Unaweza kubadilisha mambo yanayokuvutia, kuchagua ikiwa maelezo yako ya binafsi yanaweza kutumiwa kukuonyesha matangazo yanayokufaa na kuwasha au kuzima huduma fulani za matangazo.

Nenda kwenye Mipangilio ya Matangazo

Kukuhusu

Dhibiti mambo ambayo watu wengine wanaona kukuhusu kwenye huduma zote za Google.

Nenda kwenye sehemu ya Kukuhusu

Mapendekezo kutoka miduara yako

Chagua ikiwa ungependa jina na picha yako zionekana kando ya shughuli zako, kama vile maoni na mapendekezo yanayoonekana katika matangazo.

Nenda kwenye ukurasa wa Mapendekezo kutoka miduara yako

Jinsi ya kukagua na kusasisha maelezo yako

Shughuli Zangu

Kipengele cha Shughuli Zangu hukuwezesha kukagua na kudhibiti data inayoundwa unapotumia huduma za Google, kama vile utafutaji wako au kutembelea Google Play. Unaweza kuvinjari kulingana na tarehe na mada na kufuta baadhi ya shughuli zako au shughuli zote.

Tembelea ukurasa wa Shughuli Zangu

Dashibodi ya Google

Dashibodi ya Google inakuwezesha kudhibiti maelezo yanayohusiana na bidhaa mahususi.

Nenda kwenye Dashibodi

Maelezo yako ya binafsi

Dhibiti maelezo yako ya mawasiliano, kama vile jina, anwani ya barua pepe na nambari yako ya simu.

Nenda kwenye ukurasa wa Maelezo ya Binafsi

Ukiwa umeondoka katika akaunti, unaweza kudhibiti maelezo yanayohusiana na kivinjari au kifaa chako, ikiwa ni pamoja na:

Kuhamisha, kuondoa na kufuta maelezo yako

Unaweza kuhamishia nakala ya maudhui kwenye Akaunti yako ya Google ikiwa ungependa kuhifadhi nakala yake au kuitumia katika huduma isiyo ya Google.

Hamisha data yako

Unaweza pia kuomba kuondoa maudhui kwenye huduma mahususi za Google kulingana na sheria inayotumika.

Ili ufute maelezo yako, unaweza:

Kufuta maelezo yako

Mwisho kabisa, Kidhibiti cha Akaunti Isiyotumika hukuruhusu kumpa mtu mwingine idhini ya kufikia baadhi ya maelezo katika Akaunti yako ya Google endapo hutaweza kuitumia akaunti yako kutokana na matukio yasiyotarajiwa.


Kuna njia nyingine za kudhibiti maelezo ambayo Google hukusanya iwe umeingia au hujaingia katika Akaunti ya Google, ikiwa ni pamoja na:

  • Mipangilio ya kivinjari: Kwa mfano, unaweza kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili kikuarifu Google inapoweka kidakuzi katika kivinjari chako. Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili uzuie vidakuzi vyote vya kikoa mahususi au vikoa vyote. Lakini kumbuka kuwa huduma zetu zinategemea vidakuzi ili zifanye kazi ipasavyo, kwa mambo kama vile kukumbuka mapendeleo yako ya lugha.
  • Mipangilio ya kifaa: Huenda kifaa chako kina vidhibiti vinavyobaini maelezo tunayoweza kukusanya. Kwa mfano, unaweza kubadilisha mipangilio ya mahali kwenye kifaa chako cha Android.

Kushiriki maelezo yako

Unaposhiriki maelezo yako

Huduma zetu nyingi hukuruhusu kushiriki maelezo na watu wengine na unaweza kudhibiti jinsi unavyoshiriki. Kwa mfano, unaweza kushiriki video kwenye YouTube kwa umma au uziweke kwa faragha. Kumbuka, unaposhiriki maelezo kwa umma, maudhui yako yanaweza kufikiwa kupitia mitambo ya kutafuta, ikiwemo Huduma ya Tafuta na Google.

Unapotumia huduma fulani za Google ukiwa umeingia katika akaunti, kama vile kutoa maoni kuhusu video kwenye YouTube au kuhusu programu kwenye Google Play, jina na picha yako zitaonekana kando ya shughuli zako. Tunaweza pia kuonyesha maelezo haya katika matangazo kulingana na mipangilio yako ya Mapendekezo kutoka miduara yako.

Google inaposhiriki maelezo yako

Hatushiriki maelezo yako ya binafsi na kampuni, mashirika au watu binafsi nje ya Google isipokuwa mojawapo ya hali zifuatazo itokee:

Kwa idhini yako

Taarifa binafsi zako zitashirikiwa nje ya Google unapoidhinisha. Kwa mfano, ukitumia Google Home kuhifadhi nafasi kupitia huduma ya kuweka nafasi, hatutashiriki na mkahawa jina lako au nambari yako ya simu bila idhini yako. Tutaomba utupe idhini yako dhahiri kabla ya kushiriki taarifa binafsi yoyote nyeti.

Na wasimamizi wa kikoa

Ikiwa wewe ni mwanafunzi au unafanya kazi katika shirika linalotumia huduma za Google, msimamizi wa kikoa chako na wauzaji wanaodhibiti akaunti yako wataweza kufikia Akaunti yako ya Google. Wanaweza:

  • Kufikia na kudumisha maelezo yaliyohifadhiwa katika akaunti yako, kama vile barua pepe zako
  • Kuona takwimu kuhusu akaunti yako, kama vile idadi ya programu unazosakinisha
  • Kubadilisha nenosiri la akaunti yako
  • Kusimamisha au kukomesha ufikiaji wa akaunti yako
  • Kupokea maelezo ya akaunti yako ili kutimiza sheria, kanuni, mchakato wa kisheria, au ombi husika la kutekelezeka la kiserikali
  • Kuzuia uwezo wako wa kufuta au kubadilisha maelezo au mipangilio yako ya faragha

Kwa mchakato wa nje

Tunatoa maelezo ya binafsi kwa washirika wetu wadogo na biashara nyingine tunazoamini au watu ili kuyachakata kwa niaba yetu, kulingana na maagizo yetu na kwa kufuata Sera yetu ya Faragha na hatua nyingine zozote zinazofaa za faragha na usalama. Kwa mfano, tunatumia watoa huduma katika kutoa usaidizi kwa wateja.

Kwa sababu za kisheria

Tutashirikisha maelezo ya binafsi nje ya Google ikiwa tunaaamini kuwa ufikiaji, mamtumizi, uhifadhi au ufumbuzi wa maelezo hayo ni muhimu kwa:

  • Kutimiza sheria, kanuni, mchakato wa kisheria au ombi lolote la kutekelezeka la kiserikali ambalo linatumika. Tunashiriki maelezo kuhusu idadi na aina ya maombi tunayopokea kutoka kwa serikali katika Ripoti yetu ya Uwazi.
  • Kutekeleza Sheria na Masharti yanayotumika, ikiwemo uchunguzi wa ukiukaji unaoweza kutokea.
  • Kugundua, kuzuia, au kushughulikia ulaghai, masuala ya usalama au kiufundi.
  • Kulinda dhidi ya ukiukaji wa haki, madhara kwa mali au usalama wa Google, watumiaji wetu au umma inavyohitajika au kuruhusiwa na sheria.

Tunaweza kushiriki maelezo ya jumla yasiyoweza kukutambulisha kibinafsi kwa umma na pia na washirika wetu — kama vile wachapishaji, watangazaji, wasanidi programu au wenye hakimiliki. Kwa mfano, tunashiriki maelezo kwa umma ili kuonyesha mitindo kuhusu utumiaji wa jumla wa huduma zetu. Pia tunaruhusu washirika mahususi kukusanya maelezo kutoka kwenye kivinjari au kifaa chako kwa madhumuni ya matangazo na kupima kwa kutumia vidakuzi vyao au teknolojia sawa.

Ikiwa Google itahusishwa katika muungano na kampuni nyingine, ununuzi au uuzaji wa mali, tutadumisha usiri wa maelezo yako ya binafsi na kuwajulisha watumiaji walioathirika kabla ya kuhamisha maelezo yao ya binafsi au kuyaweka chini ya sera tofauti ya faragha.

Kulinda maelezo yako

Tunadumisha usalama katika huduma zetu ili kulinda maelezo yako

Bidhaa zote za Google zina vipengele thabiti vya usalama ambavyo hulinda maelezo yako kila wakati. Ufahamu tunaopata kutokana na kudumisha huduma zetu hutusaidia kukulinda kwa kutambua na kuzuia kiotomatiki vitisho vya usalama. Ikiwa tutagundua vitisho vya usalama ambavyo tunaamini unapaswa kujua, tutakuarifu na kukupa hatua za kuchukua ili kujilinda vyema.

Tunajitahidi kukulinda wewe pamoja na Google dhidi ya ufikiaji, mabadiliko, ufumbuzi au uharibifu usioidhinishwa wa maelezo tuliyoweka, ikiwa ni pamoja na:

  • Tunatumia usimbaji fiche ili kuweka data yako faraghani tunapoihamisha
  • Tuna vipengele mbalimbali vya usalama vinavyokuwezesha kulinda akaunti yako. Vipengele hivi ni kama vile Kuvinjari Salama, Ukaguzi wa Usalama na Uthibitishaji wa Hatua Mbili
  • Tunakagua desturi zetu za maelezo tunayokusanya, hifadhi na uchakataji wake, ikiwa ni pamoja na hatua halisi za usalama, ili kulinda mifumo yetu dhidi ya ufikiaji ambao haujaidhinishwa.
  • Maelezo ya binafsi yanaweza kufikiwa tu na waajiriwa wa Google, wanakandarasi na mawakala ambao tumewaruhusu kuchakata maelezo hayo. Mtu yeyote aliye na idhini ya kufikia maelezo haya anapaswa kuzingatia kikamilifu wajibu wa usiri wa mkataba na anaweza kuadhibiwa au kusimamishwa ikiwa atakiuka wajibu huu.

Kuhamisha na kufuta maelezo yako

Unaweza kuhamishia au kufuta nakala ya maelezo kwenye Akaunti yako ya Google wakati wowote.

Unaweza kuhamishia nakala ya maudhui kwenye Akaunti yako ya Google ikiwa ungependa kuhifadhi nakala yake au kuitumia katika huduma isiyo ya Google.

Hamisha data yako

Ili ufute maelezo yako, unaweza:

Kufuta maelezo yako

Kuhifadhi taarifa zako

Tunahifadhi data ambayo tunakusanya kwa vipindi tofauti kwa kutegemea aina ya data, jinsi tunavyoitumia na jinsi unavyoweka mipangilio yako:

  • Unaweza kufuta baadhi ya data wakati wowote, kama vile maudhui unayounda au kupakia. Unaweza pia kufuta maelezo kuhusu shughuli yaliyohifadhiwa katika akaunti yako au uchague yafutwe kiotomatiki baada ya kipindi kilichobainishwa.
  • Data nyingine hufutwa au utambulisho wake hufichwa kiotomatiki baada ya kipindi kilichobainishwa, kama vile data ya utangazaji katika kumbukumbu za seva.
  • Tunahifadhi baadhi ya data hadi utakapofuta Akaunti yako ya Google, kama vile maelezo kuhusu mara ambazo unatumia huduma zetu.
  • Na tunahifadhi baadhi ya data kwa vipindi virefu panapohitajika kwa madhumuni halali ya kibiashara au kisheria, kama vile kulinda usalama, kuzuia ulaghai na matumizi mabaya au kuweka rekodi za kifedha.

Unapofuta data, tunazingatia mchakato wa kufuta ili kuhakikisha kwamba data yako imeondolewa kabisa kwenye seva zetu kwa njia salama au imehifadhiwa tu kwa namna inayoficha utambulisho wake. Tunajitahidi kuhakikisha kuwa huduma zetu zinalinda taarifa ili yasifutwe kimakosa au kwa nia ya kudhuru. Kwa sababu hii, huenda ikachukua muda kuondoa kitu unachofuta kwenye mifumo yetu inayofanya kazi na kwenye mifumo ya kuhifadhi nakala.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu vipindi vya kuhifadhi data kwenye Google, ikiwa ni pamoja na muda tunaohifadhi taarifa zako kabla ya kuzifuta.

Uzingatiaji na ushirikiano na wasimamizi

Sisi hukagua Sera hii ya Faragha mara kwa mara na kuhakikisha kwamba tunachakata maelezo yako kwa kuzingatia sera hii.

Uhamishaji data

Tuna seva duniani kote na maelezo yako yanaweza kuchakatwa kwenye seva zilizo nje ya nchi unakoishi. Sheria za ulinzi wa data hutofautiana katika kila nchi. Kuna nchi ambazo hutoa ulinzi zaidi kuliko nyingine. Popote maelezo yako yanapochakatwa tunazingatia sheria za ulinzi wa data kama ilivyofafanuliwa kwenye sera hii. Pia, tunatii mifumo fulani ya kisheria inayohusiana na uhamishaji wa data.

Tunapopokea malalamiko yaliyoandikwa kirasmi, tunayachakata kwa kuwasiliana na mtu aliyetoa malalamiko hayo. Tunafanya kazi na mamlaka ya sheria inayohusika, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kulinda data ya eneo, ili kutatua malalamiko yoyote kuhusiana na uhamishaji wa data yako ambayo hatuwezi kutatua na wewe moja kwa moja.

Masharti ya California

Sheria ya California ya Ulinzi wa Faragha ya Watumiaji (CCPA) inahitaji ufumbuzi mahususi kwa wakaazi wa California.

Sera hii ya Faragha imetungwa kukusaidia uelewe jinsi Google hushughulikia taarifa yako:

Sheria ya CCPA pia inakupa haki ya kuomba maelezo kuhusu jinsi Google hukusanya, kutumia na kufumbua taarifa yako binafsi. Na hukupa haki ya kufikia taarifa zako na kuomba Google ifute taarifa hizo. Mwisho, sheria ya CCPA inakupa haki ya kutokubaguliwa kwa kutumia haki zako za faragha.

Tunafafanua chaguo ulizo nazo za kudhibiti faragha na data yako kote kwenye huduma za Google katika Vidhibiti vyako vya faragha. Unaweza kutekeleza haki zako kwa kutumia vidhibiti hivi, ambavyo hukupa idhini ya kufikia, kukagua, kusasisha na kufuta taarifa zako, pamoja na kutuma na kupakua nakala zake. Unapozitumia, tutaidhinisha ombi lako kwa kuthibitisha kuwa umeingia katika Akaunti yako ya Google. Iwapo una maswali au maombi yanayohusiana na haki zako chini ya sheria ya CCPA, wewe (au dalali wako aliyeidhinishwa) unaweza pia kuwasiliana na Google. Unaweza pia kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google hushughulikia maombi ya CCPA.

Sheria ya CCPA inahitaji maelezo ya desturi za data kwa kutumia aina mahususi. Jedwali hili linatumia aina hizi kupanga taarifa katika Sera hii ya Faragha.

Aina za taarifa binafsi ambazo tunakusanya

Vitambulishi kama vile jina lako, nambari yako ya simu na anwani yako, pamoja na vitambulishi vya kipekee vilivyo kwenye kivinjari, programu au kifaa unachotumia.

Maelezo ya demografia, kama vile umri, jinsia na lugha yako.

Maelezo ya biashara kama vile maelezo ya malipo na historia ya ununuzi unaofanya kwenye huduma za Google.

Maelezo ya kibayometriki iwapo utachagua kuyatoa, kama vile alama za vidole kwenye tafiti za kubuni bidhaa za Google.

Intaneti, mtandao na taarifa nyingine za shughuli kama vile hoja zako za utafutaji, mara ambazo umetazama na kutumia maudhui na matangazo; historia ya kuvinjari kwenye Chrome ambayo umesawazisha kwenye Akaunti yako ya Google; taarifa kuhusu utumiaji wa programu, vivinjari, na vifaa vyako kwenye huduma zetu (kama vile Anwani ya IP, ripoti ya kuacha kufanya kazi na shughuli za mfumo); na shughuli kwenye tovuti na programu za wengine zinazotumia huduma zetu. Unaweza kukagua na kudhibiti data ya shughuli inayohifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google katika sehemu ya Shughuli Zangu.

Data ya kutambulisha mahali, jinsi inavyoweza kubainishwa na GPS, Anwani ya IP na data kutoka vitambuzi vilivyo kwenye kifaa chako au karibu nacho, kulingana na mipangilio ya akaunti na kifaa chako kwa kiasi fulani. Pata maelezo zaidi kuhusu Jinsi Google hutumia taarifa za mahali.

Taarifa za sauti, elektroniki, video na taarifa sawa na hizo, kama vile taarifa za sauti na matamshi unapotumia vipengele vya sauti.

Taarifa za kitaalamu, kikazi na kielimu, kama vile taarifa unazotoa au zinazohifadhiwa kupitia shirika linalotumia huduma za Google unakofanyia kazi au kusomea.

Taarifa nyingine unazotunga au kutoa, kama vile maudhui unayobuni, kupakia au kupokea (kama vile picha na video au barua pepe, hati na malahajedwali). Dashibodi ya Google hukuruhusu udhibiti taarifa zinazohusiana na bidhaa mahususi.

Maelezo yanayotokana na taarifa hapo juu, kama vile aina za matangazo yanayokuvutia.

Madhumuni ya biashara ambayo maelezo yanaweza kutumika au kufumbuliwa

Kutoa ulinzi dhidi ya tishio za usalama, matumizi mabaya na shughuli haramu: Google hutumia na inaweza kufumbua taarifa ili kutambua, kuzuia na kushughulikia matukio ya kiusalama na kutoa ulinzi dhidi ya shughuli zingine hasidi, za kupotosha, za ulaghai au haramu. Kwa mfano, ili kulinda huduma zetu, huenda Google ikapokea au ikafichua taarifa kuhusu anwani za IP ambazo zimeathiriwa na watumiaji hasidi.

Hesabu na vipimo: Google hutumia taarifa za takwimu na vipimo ili kuelewa jinsi huduma zetu zinavyotumika, pamoja na kutimiza wajibu kwa washirika wetu kama vile wachapishaji, watangazaji, wasanidi programu au wenye hakimiliki. Tunaweza kufumbua taarifa zisizomtambulisha mtu mahususi hadharani na kwa washirika hawa, ikiwa ni pamoja na kwa madhumuni ya kufanya hesabu.

Kudumisha huduma zetu: Google hutumia taarifa kuhakikisha kuwa huduma zetu zinafanya kazi ipasavyo, kama vile kufuatilia matatizo na kutatua hitilafu na matatizo mengine unayoripoti kwetu.

Utafiti na ubunifu: Google hutumia taarifa kuboresha huduma zetu na kubuni bidhaa, vipengele na teknolojia mpya ambazo huwafaa watumiaji wetu na umma. Kwa mfano, tunatumia taarifa zinazopatikana kwa umma ili kusaidia kufunza miundo ya lugha ya Google na kubuni vipengele kama vile Google Tafsiri.

Utumiaji wa watoa huduma: Google hushiriki taarifa na watoa huduma ili kutoa huduma kwa niaba yetu, kwa kutii Sera yetu ya Faragha na hatua nyingine zinazofaa za usiri na usalama. Kwa mfano, tunaweza kutegemea watoa huduma ili kutusaidia kutoa usaidizi kwa wateja.

Utangazaji Google huchakata taarifa, ikiwa ni pamoja na vitambulishi vya mtandaoni na taarifa kuhusu jinsi unavyojihusisha na matangazo, ili kutoa huduma ya utangazaji. Hali hii hufanya huduma za Google na tovuti na huduma nyingi unazotumia zitolewe bila malipo. Unaweza kudhibiti aina ya taarifa tunazotumia kukuonyesha matangazo kwa kutembelea mipangilio yako ya matangazo.

Sababu za kisheria: Google pia hutumia taarifa kutii kanuni au sheria zinazotumika na hufichua taarifa zikihitajika katika mchakato wa kisheria au maombi ya serikali yanayoweza kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa sheria. Tunatoa taarifa kuhusu idadi na aina ya maombi tunayopokea kutoka kwa serikali katika Ripoti yetu ya Uwazi.

Washirika ambao tunaweza kushiriki taarifa nao

Watu wengine ambao unachagua kushiriki taarifa zako nao, kama vile hati au picha na video au maoni kwenye YouTube.

Washirika wengine ambao umeruhusu kushiriki taarifa zako nao, kama vile huduma ambazo hujumuishwa na huduma za Google. Unaweza kukagua na kudhibiti programu na tovuti za wengine zilizo na idhini ya kufikia data kwenye Akaunti yako ya Google.

Watoa huduma, biashara au watu wanaoaminika na ambao huchakata taarifa kwa niaba ya Google, kulingana na maagizo yetu na kwa kutii Sera yetu ya Faragha na nyingine zozote zinazofaa za usiri na usalama.

Wasimamizi wa vikoa, iwapo unafanya kazi au kusoma katika shirika linalotumia huduma za Google.

Watekelezaji wa sheria au washirika wengine, kwa sababu za kisheria zilizoelezewa katika sehemu ya Kushiriki taarifa zako.

Kuhusu sera hii

Sera hii inapotumika

Sera hii ya Faragha inatumika kwa huduma zote za Google LLC na washirika wake wadogo, ikiwa ni pamoja na YouTube, Android na huduma kwenye tovuti nyingine kama vile huduma za matangazo. Sera hii ya Faragha haitumiki kwa huduma ambazo zina sera tofauti za faragha ambazo hazijumuishi Sera hii ya Faragha.

Sera hii ya Faragha haitumiki kwa:

  • Desturi za mawasiliano za kampuni na mashirika mengine yanayotangaza huduma zetu
  • Huduma zinazotolewa na kampuni nyingine au watu binafsi, zikiwemo bidhaa au tovuti zinazoweza kujumuisha huduma za Google, unazoweza kuona katika matokeo ya utafutaji, au ambazo huenda zimeunganishwa kutoka kwenye huduma zetu

Mabadiliko kwenye sera hii

Sera hii ya Faragha hubadilishwa mara kwa mara. Hatutapunguza haki zako kwa mujibu wa Sera hii ya Faragha bila kibali chako dhahiri. Tunahakikisha kuwa tumeonyesha tarehe ambayo sera ilibadilishwa mara ya mwisho na tunakupa idhini ya kufikia matoleo yaliyohifadhiwa kwenye kumbukumbu ili uweze kuyakagua. Ikiwa mabadiliko ni muhimu, tutakuarifu kwa kina zaidi (pamoja na, kwa huduma fulani, utaarifiwa kupitia barua pepe kuhusu mabadiliko ya Sera ya Faragha).

Desturi za faragha zinazohusiana

Huduma mahususi za Google

Ilani zifuatazo za faragha hutoa maelezo ya ziada kuhusu huduma fulani za Google:

Ikiwa wewe ni mwanachama wa shirika linalotumia Google Workspace au Mfumo wa Wingu la Google, pata maelezo kuhusu jinsi huduma hizi hukusanya na kutumia taarifa zako binafsi katika Ilani ya Faragha ya Wingu la Google.

Nyenzo nyingine muhimu

Viungo vifuatavyo vinaonyesha nyenzo muhimu za kupata maelezo zaidi kuhusu desturi na mipangilio yetu ya faragha.

Masharti muhimu

Akaunti ya Google

Unaweza kufikia baadhi ya huduma zetu kwa kufungua Akaunti ya Google na kutoa baadhi ya maelezo yako ya binafsi (kwa kawaida jina lako, anwani ya barua pepe na nenosiri). Maelezo haya ya akaunti hutumiwa kukuthibitisha unapofikia huduma za Google na kulinda akaunti yako isifikiwe na watu ambao hujawaidhinisha. Unaweza kubadilisha maelezo kwenye akaunti au kuifunga wakati wowote kupitia mipangilio ya Akaunti yako ya Google.

Algoriti

Mchakato au taratibu zinazofuatwa na kompyuta kutatua matatizo.

Anwani ya IP

Kila kifaa kilichounganishwa kwenye Intaneti kimetawazwa nambari inayojulikana kama anwani ya itifaki ya Intaneti (IP). Kwa kawaida nambari hizi hutawazwa katika vikundi vya kijiografia. Mara nyingi anwani ya IP inaweza kutumiwa kutambua kifaa kinaunganishwa kutoka eneo gani kwenye Intaneti.

Hifadhi ya kivinjari cha wavuti

Hifadhi ya kivinjari huwezesha tovuti kuhifadhi data katika kivinjari kwenye kifaa. Unapoitumia katika hali ya "hifadhi ya ndani", inakuwezesha kuhifadhi data katika vipindi vyote. Hii inakuwezesha kupata data hata baada ya kufunga na kufungua upya kivinjari. Teknolojia moja ambayo inawezesha kuhifadhi kwenye wavuti ni HTML 5.

Hifadhi ya ndani ya data ya programu

Hifadhi ya ndani ya data ya programu ni hifadhi ya data kwenye kifaa. Inaweza, kwa mfano, kuwezesha programu ya wavuti kuendeshwa bila muunganisho wa intaneti na kuboresha utendaji wa programu kwa kuwezesha upakiaji wa haraka wa maudhui.

Kifaa

Kifaa ni kompyuta ambayo inaweza kutumika ili kufikia huduma za Google. Kwa mfano, kompyuta za mezani, kompyuta kibao, spika mahiri na simu mahiri, zote zinachukuliwa kuwa vifaa.

Kumbukumbu za seva

Kama tovuti mingi, seva zetu hurekodi maombi ya ukurasa yanayofanywa unapotembelea tovuti zetu kiotomatiki. “Kumbukumbu za seva” kwa kawaida hujumuisha ombi lako la wavuti, anwani ya IP, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na wakati wa ombi lako na moja au zaidi ya vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari chako kipekee.

Huu ni mfano wa kumbukumbu ambapo utafutaji ni wa “magari”:

123.45.67.89 - 25/Mar/2003 10:15:32 -
http://www.google.com/search?q=cars -
Firefox 1.0.7; Windows NT 5.1 -
740674ce2123e969
  • 123.45.67.89 ni anwani ya IP inayotolewa kwa mtumiaji na mtoa huduma za intaneti. Kulingana na huduma ya mtumiaji, anwani tofauti inaweza kutolewa kwa mtumiaji na mtoa huduma wake kila wakati anapounganisha kwenye Intaneti.
  • 25/Mar/2003 10:15:32 ndiyo tarehe na saa ya hoja.
  • http://www.google.com/search?q=cars ndiyo URL iliyoombwa, ikiwemo hoja ya utafutaji.
  • Firefox 1.0.7; Windows NT 5.1 ndicho kivinjari na mfumo wa uendeshaji unaotumika.
  • 740674ce2123a969 ndicho kitambulisho cha kipekee cha kidakuzi kilichotolewa kwa kompyuta hii mara ya kwanza ilipotumika kutembelea Google. (Vidakuzi vinaweza kufutwa na watumiaji. Ikiwa mtumiaji amefuta kidakuzi kwenye kompyuta kutoka wakati wa mwisho alipotembelea Google, kitambulisho cha kipekee cha kidakuzi kitatolewa kwa mtumiaji atakapotembelea Google tena akitumia kompyuta hiyo).

Lebo ya Pixeli

Lebo ya pikseli ni aina ya teknolojia inayowekwa kwenye tovuti au katika kiini cha barua pepe kwa lengo la kufuatilia shughuli fulani kwenye tovuti, kama vile tovuti inapotembelewa au barua pepe zinapofunguliwa. Lebo za pikseli kwa kawaida hutumiwa pamoja na vidakuzi.

Maelezo nyeti ya kibinafsi

Hii ni aina mahususi ya maelezo ya binafsi yanayohusiana na maelezo ya siri ya afya, asili ya mbari au kabila, imani za kisiasa au dini au mwelekeo wa jinsia.

Maelezo ya kibinafsi

Haya ni maelezo ambayo unatupa yanayokutambulisha binafsi, kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, au maelezo ya malipo, au data nyingine ambayo inaweza kuhusishwa kwa kawaida na maelezo kama hayo na Google, kama vile maelezo tunayohusisha na Akaunti yako ya Google.

Maelezo yasiyotambulisha kibinafsi

Haya ni maelezo yanayorekodiwa kuhusu watumiaji ili yasionyeshe wala kurejelea tena mtumiaji binafsi anayetambulika.

URL Iliyoelekeza

URL Iliyoelekeza (Uniform Resource Locator) ni maelezo yanayowasilishwa na kivinjari kwenye ukurasa lengwa wa wavuti, kwa kawaida unapobofya kiungo cha ukurasa huo. URL Iliyoelekeza ina URL ya ukurasa wa mwisho wa wavuti uliovinjari.

Vidakuzi

Kidakuzi ni faili ndogo iliyo na msururu wa herufi inayotumwa kwenye kompyuta yako unapotembelea tovuti fulani. Unapotembelea tovuti tena, kidakuzi kinaruhusu tovuti hiyo kutambua kivinjari chako. Vidakuzi vinaweza kuhifadhi mapendeleo ya mtumiaji na maelezo mengine. Unaweza kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili kisitumie vidakuzi au kikuarifu kidakuzi kinapotumwa. Hata hivyo, vipengee vingine vya tovuti au huduma huenda visifanye kazi vizuri bila vidakuzi. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia vidakuzi na data, vikiwemo vidakuzi, unapotumia tovuti au programu za washirika wetu.

Vitambulishaji vya kipekee

Kitambulishaji cha kipekee ni mfuatano wa herufi ambao unaweza kutumika kutambua kivinjari, programu au kifaa maalum. Vitambulishaji tofauti hutofautiana kulingana na muda vinaodumu, ikiwa vinaweza kubadilishwa na mtumiaji na jinsi vinavyoweza kufikiwa.

Vitambulishaji vya kipekee vinaweza kutumika kwa madhumuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na usalama na ugunduaji ulaghai, kusawazisha huduma kama vile barua pepe zako, kukumbuka mapendeleo yako na kukuonyesha matangazo yanayokufaa. Kwa mfano, vitambulishaji vya kipekee vilivyohifadhiwa kwenye vidakuzi vinasaidia tovuti unayovinjari kuonyesha maudhui katika lugha unayopendelea. Unaweza kuweka mipangilio kwenye kivinjari chako ili kisitumie vidakuzi au kikuarifu kidakuzi kinapotumwa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia vidakuzi.

Kwenye mifumo mingine kando na vivinjari, vitambulishaji vya kipekee hutumika kutambua kifaa au programu maalum kwenye kifaa hicho. Kwa mfano, kitambulishaji cha kipekee kama vile Kitambulisho cha kifaa kwa ajili ya Matangazo hutumika kutoa matangazo yanayofaa kwenye vifaa vya Android na kinaweza kudhibitiwa kwenye mipangilio ya kifaa chako. Vitambulishaji vya kipekee vinaweza pia kujumuishwa kwenye kifaa na mtengenezaji (wakati mwingine huitwa kitambulisho cha kipekee ulimwenguni au UUID), kama vile nambari ya IMEI ya simu ya mkononi. Kwa mfano, kitambulisho cha kipekee cha kifaa kinaweza kutumika kukupa huduma zinazokufaa au kukagua matatizo ya kifaa yanayohusiana na huduma zetu.

Washirika

Mshirika ni kampuni ambayo ipo kwenye kundi la kampuni za Google, zikiwemo kampuni zifuatazo zinazotoa huduma za watumiaji katika Umoja wa Ulaya: Google Ireland Limited, Google Commerce Ltd, Google Payment Corp na Google Dialer Inc. Pata maelezo zaidi kuhusu kampuni zinazotoa huduma za biashara katika Umoja wa Ulaya.

Muktadha wa Ziada

aina nyeti

Tunapokuonyesha matangazo yanayokufaa, tunatumia mada ambazo tunadhania zinaweza kukuvutia kulingana na shughuli zako. Kwa mfano, unaweza kuona matangazo ya vitu kama vile "Kupika na Mapishi" au "Usafiri wa Ndege.” Huwa hatutumii mada au kuonyesha matangazo yanayokufaa kulingana na aina nyeti kama vile rangi, dini, mwelekeo wa kingono au afya. Na huwa tunahitaji kuona hivyo kutoka kwa watangazaji wanaotumia huduma zetu.

Data ya sensa kutoka kwenye kifaa chako

Huenda kifaa chako kikawa na sensa ambazo zinaweza kutumiwa kusaidia kuelewa vyema eneo lako na kokote unakoenda. Kwa mfano, kipima mchapuko kinaweza kutumiwa kubainisha kasi na gurudumu tuzi kujua mwelekeo wako wa safari.

huduma mahususi za Google

Kwa mfano, unaweza kufuta blogu yako kwenye Blogger au tovuti ya Google unayomiliki kwenye Tovuti za Google. Pia unaweza kufuta maoni ulioacha kwenye programu, michezo na maudhui mengine katika Duka la Google Play.

huduma za kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe

Mifano ya huduma hizi inajumuisha:

  • Google Voice, kwa ajili ya kupiga na kupokea simu, kutuma SMS na kudhibiti ujumbe wa sauti
  • Google Meet, kwa ajili ya kupiga na kupokea simu za video
  • Gmail, kwa ajili ya kutuma na kupokea barua pepe
  • Google Chat, kwa ajili ya kutuma na kupokea ujumbe
  • Google Duo, kwa ajili ya kupiga na kupokea simu za video na kutuma na kupokea ujumbe
  • Google Fi, kwa mpango wa simu

huduma za kutangaza na utafiti kwa niaba yao

Kwa mfano, watangazaji wanaweza kupakia data kutoka programu zao za kadi ya uaminifu ili waweze kuelewa vyema utendaji wa kampeni zao za matangazo. Tunatoa tu ripoti za ujumlisho ambazo hazifichui maelezo kuhusu watu maalum kwa watangazaji.

Google Analytics hutegemea vidakuzi vya mtu wa kwanza, kumaanisha kuwa vidakuzi vimewekwa na mteja wa Google Analytics. Kwa kutumia mifumo yetu, data inayozalishwa kupitia Uchanganuzi wa Google inaweza kuunganishwa na mteja wa Google Analytics na Google kwenye vidakuzi vya wahusika wengine ambavyo vinahusiana na matembeleo ya tovuti nyingine. Kwa mfano, mtangazaji anaweza kutaka kutumia data yake ya Google Analytics ili kuunda matangazo muhimu zaidi, au kuchanganua trafiki yake zaidi. Pata maelezo zaidi

hutegemea vidakuzi ili kufanya kazi vizuri

Kwa mfano, tunatumia kidakuzi kinachoitwa 'Ibcs' ambacho kinakuwezesha kufungua Hati nyingi za Google katika kivinjari kimoja. Kuzuia kidakuzi hiki kunaweza kuzuia Hati za Google kufanya kazi inavyotakikana. Pata maelezo zaidi

iliyosawazisha na Akaunti yako ya Google

Historia yako ya kuvinjari kwenye Chrome inahifadhiwa tu kwenye akaunti yako ikiwa umeruhusu usawazishaji wa Chrome na Akaunti yako ya Google. Pata maelezo zaidi

Kifaa cha Android kilicho na programu za Google

Vifaa vya Android vilivyo na programu za Google ni pamoja na vifaa vinavyouzwa na Google au na mmojawapo wa washirika wetu na inajumuisha simu, kamera, magari, vifaa vya kuvaliwa na runinga. Vifaa hivi hutumia Huduma za Google Play na programu ambazo zilisanikishwa awali ambazo ni pamoja na huduma kama vile Gmail, Ramani, kamera ya simu yako na kipiga simu, ubadilishaji wa maandishi kwenda usemi, kibodi na vipengele vya ulinzi.

kuboresha

Kwa mfano, tunatumia vidakuzi ili kuchanganua jinsi watu wanavyotumia huduma zetu. Na uchanganuzi huo unaweza kutusaidia kutengeneza bidhaa bora. Kwa mfano, unaweza kutusaidia kugundua kwamba inachukua watu muda mrefu kukamilisha kazi fulani au wanatatizika kabisa kumaliza hatua. Hivyo tunaweza kuunda tena kipengele hicho na kuboresha bidhaa kwa kila mtu.

kuhakikisha kuwa huduma zetu zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa

Kwa mfano, sisi huendelea kufuatilia mifumo yetu ili tutatue matatizo. Na tukipata hitilafu kwenye kipengele mahususi, kukagua maelezo ya shughuli yaliyokusanywa kabla ya tatizo kuanza, hutusaidia kutatua matatizo kwa haraka zaidi.

kuhakikisha na kuboresha

Kwa mfano, tunachanganua jinsi watu wanavyotumia utangazaji kuboresha utendaji wa matangazo yetu.

kulinda dhidi ya matumizi mabaya

Kwa mfano, maelezo kuhusu vitisho vya usalama yanaweza kutusaidia kukuarifu ikiwa tunadhani akaunti yako imeathiriwa (ambapo kutoka hapo tunaweza kukusaidia kuchukua hatua za kulinda akaunti yako).

Watu wengi wakianza kutafuta kitu, shughuli hizo zinaweza kutoa maelezo muhimu kuhusu mitindo maalum wakati huo. Google Trends hukusanya utafutaji kwenye wavuti katika Google ili kukadiria umaarufu wa utafutaji uliofanywa katika kipindi fulani na hushiriki matokeo hayo hadharani kwa kijumla. Pata maelezo zaidi

kushirikiana na Google

Kuna tovuti na programu zaidi ya milioni 2 zisizo za Google zinazoshirikiana na Google kuonyesha matangazo. Pata maelezo zaidi

kutambua matumizi mabaya

Tunapotambua barua taka, programu hasidi, maudhui yasiyo halali na matumizi mengine mabaya kwenye mifumo yetu dhidi ya ukiukaji wa sera zetu, tunaweza kufunga akaunti yako au kuchukua hatua nyingine inayofaa. Katika hali fulani, pia tunaweza kuripoti ukiukaji huu kwa mamlaka yanayofaa.

kuwasilisha huduma zetu

Mifano ya jinsi tunavyotumia maelezo yako ili kuwasilisha huduma zetu ni pamoja na:

  • Tunatumia anwani ya IP ya kifaa chako ili tukutumie data uliyoomba kama vile kupakia video ya YouTube
  • Tunatumia vitambulishaji vya kipekee vilivyohifadhiwa katika vidakuzi kwenye kifaa chako ili kutusaidia kukuthibitisha kuwa mtu anayeweza kufikia Akaunti yako ya Google
  • Picha na video unazopakia katika Picha kwenye Google hutumiwa ili zikusaidie kuunda albamu, uhuishaji na ubunifu mwingine ambao unaweza kuushiriki. Pata maelezo zaidi
  • Barua pepe unayopokea ya kuthibitisha usafiri wa ndege inaweza kutumiwa kuunda kitufe cha kuripoti kuwa umefika ambacho huonekana katika Gmail yako.
  • Unapolipia huduma au bidhaa halisi kutoka kwetu, huenda ukatoa maelezo kama vile anwani yako ya mahali bidhaa zitakapopelekwa au maagizo ya usafirishaji bidhaa. Tunatumia maelezo haya kwa madhumuni kama vile kuchakata, kutekeleza na kusafirisha bidhaa unazoagiza na kutoa usaidizi kuhusu huduma au bidhaa unazonunua.

kuweka pamoja maelezo tunayokusanya

Baadhi ya mifano ya jinsi tunavyoweka pamoja maelezo tunayokusanya ni pamoja na:

  • Wakati umeingia katika Akaunti yako ya Google na kutafuta kwenye Google, unaweza kuona matokeo ya utafutaji kutoka kwenye wavuti wa umma, pamoja na maelezo yanayohusiana kutoka kwenye maudhui uliyo nayo katika bidhaa nyingine za Google, kama vile Gmail au Kalenda ya Google. Hii inaweza kujumuisha vitu kama vile hali ya safari zako zijazo za ndege, mkahawa na kuweka nafasi za hoteli au picha zako. Pata maelezo zaidi
  • Ikiwa umewasiliana na mtu kupitia Gmail na unataka kumwongeza kwenye Hati za Google au tukio katika Kalenda ya Google. Google inarahisisha kufanya hivyo kwa kukamilisha anwani yake ya barua pepe kiotomatiki unapoanza kuandika jina lake. Kipengee hiki hurahisisha kushiriki vitu na watu unaowajua. Pata maelezo zaidi
  • Programu ya Google inaweza kutumia data uliyohifadhi katika bidhaa nyingine za Google ili kukuonyesha maudhui yanayokufaa, kulingana na mipangilio yako. Kwa mfano, ikiwa una utafutaji uliohifadhiwa katika Shughuli zako za Programu na Wavuti, programu ya Google inaweza kukuonyesha makala ya habari na taarifa zingine kuhusu mambo yanayokuvutia, kama alama za michezo, kulingana na shughuli yako. Pata maelezo zaidi
  • Ukiunganisha Akaunti yako ya Google kwenye Google Home, unaweza kudhibiti maelezo yako na kukamilisha shughuli kupitia Mratibu wa Google. Kwa mfano, unaweza kuongeza matukio katika Kalenda yako ya Google au upate ratiba yako ya siku, kuomba masasisho ya hali ya safari yako ijayo ya ndege au kutuma maelezo kama vile maelekezo ya uendeshaji gari kwenye simu yako. Pata maelezo zaidi

maelezo kuhusu vitu vilivyo karibu na kifaa chako

Ikiwa unatumia Huduma za Mahali za Google kwenye Android, tunaweza kuboresha utendaji wa programu zinazotegemea mahali ulipo, kama vile Ramani za Google. Ikiwa unatumia Huduma za Mahali za Google, kifaa chako hutuma maelezo kwa Google kuhusu mahali kilipo, sensa (kama vile kipima mchapuko) na minara ya mitandao iliyo karibu na maeneo ya kufikia Wi-Fi (kama vile anwani ya MAC na uthabiti wa mawimbi). Vitu hivi vyote husaidia kubainisha mahali ulipo. Unaweza kutumia mipangilio ya kifaa chako ili kuwasha huduma za Mahali za Google. Pata maelezo zaidi

maelezo ya malipo

Kwa mfano, ikiwa utaongeza kadi yako ya mikopo au njia nyingine ya kulipa kwenye akaunti yako ya Google, unaweza kuitumia kununua bidhaa katika huduma zetu zote, kama vile programu katika Duka la Google Play. Pia, tunaweza kukuomba utupe maelezo mengine, kama vile nambari ya ushuru ya biashara ili itusaidie kuchakata malipo yako. Katika hali nyingine, pia tunaweza kuhitaji kuthibitisha utambulisho wako na tunaweza kukuomba utupe maelezo ili tufanye hivyo.

Pia, tunaweza kutumia maelezo ya malipo ili kuthibitisha kwamba unatimiza masharti ya umri, ikiwa kwa mfano, utaandika tarehe ya kuzaliwa isiyo sahihi ambayo inaonyesha kwamba huna umri wa kutosha kuwa na Akaunti ya Google. Pata maelezo zaidi

matangazo ambayo utapata ni muhimu zaidi

Kwa mfano, ikiwa unatazama video kwenye YouTube kuhusu kuoka keki, unaweza kuona matangazo zaidi yanayohusiana na kuoka, unapovinjari wavuti. Pia, tunaweza kutumia anwani yako ya IP ili kukadiria mahali, ili tuweze kukuonyesha matangazo ya huduma ya karibu ya usafirishaji piza ukitafuta "piza." Pata maelezo zaidi kuhusu matangazo ya Google na sababu ya kuweza kuona matangazo maalum.

matangazo yanayokufaa

Pia unaweza kuona matangazo yanayokufaa kulingana na maelezo kutoka kwa mtangazaji. Kwa mfano, ikiwa umenunua kwenye tovuti ya mtangazaji, anaweza kutumia maelezo ya kuingia kwenye tovuti yake kukuonyeshe matangazo. Pata maelezo zaidi

Kwa mfano, wakati umeingia kwenye Akaunti yako ya Google na umewasha kidhibiti cha Shughuli za Wavuti na Programu, unaweza kupata matokeo yanayokufaa zaidi ya utafutaji kulingana na utafutaji na shughuli za awali kutoka kwenye huduma nyingine za Google. Unaweza kupata maelezo zaidi hapa. Pia, unaweza kupata matokeo ya utafutaji yaliyoboreshwa hata ukiwa umeondoka kwenye akaunti. Ikiwa hutaki kiwango hiki cha utafutaji ulioboreshwa, unaweza kutafuta na kuvinjari faraghani au uzime utafutaji unaokufaa ambao umeondolewa kwenye akaunti.

Kama kampuni nyingine za teknolojia na mawasiliano, Google hupokea maombi kutoka kwa serikali na mahakama duniani kote mara kwa mara ili kufumbua data ya mtumiaji. Kuheshimu faragha na usalama wa data inayohifadhi kwenye Google ndiyo kanuni tanayofuata tunapopokea maombi haya ya kisheria. Timu yetu ya sheria hukagua kila ombi, bila kubagua aina na mara nyingi sisi hukataa ombi linaloonekana kuwa pana sana au lisilofuatilia mchakato sahihi. Pata maelezo zaidi katika Ripoti yetu ya Uwazi.

nambari ya simu

Ikiwa utaongeza nambari yako ya simu kwenye akaunti yako, inaweza kutumika kwa madhumuni tofauti ya huduma zote za Google, kulingana na mipangilio yako. Kwa mfano, nambari yako ya simu inaweza kutumiwa ili ikusaidie kufikia akaunti yako iwapo utasahau nenosiri yako, kusaidia watu kukupata na kuunganika nawe na kufanya matangazo unayoyaona yakufae zaidi. Pata maelezo zaidi

seva duniani kote

Kwa mfano, tunasimamia vituo vya data vilivyo duniani kote ili kusaidia kufanya bidhaa zetu ziendelee kupatikana kwa ajili ya watumiaji bila kukoma.

shughuli zako kwenye tovuti na programu nyingine

Shughuli hizi huenda zitokane na matumizi yako ya huduma za Google kama vile usawazishaji wa akaunti yako na Chrome au tovuti na programu zako unazotembelea ambazo zinashirikiana na Google. Tovuti na programu nyingi hushirikiana na Google kuboresha maudhui na huduma zao. Kwa mfano, tovuti inaweza kutumia huduma zetu za matangazo (kama vile AdSense) au zana za uchanganuzi (kama vile Google Analytics), au inaweza kupachika maudhui mengine (kama vile video kutoka YouTube). Huduma hizi huenda zikashiriki taarifa kuhusu shughuli zako na Google, na kulingana na mipangilio ya akaunti yako na bidhaa unazotumia (kwa mfano, mshirika anapotumia Google Analytics pamoja na huduma zetu za matangazo), data hii huenda ikahusishwa na maelezo yako ya binafsi.

Pata maelezo zaidi kuhusu namna Google hutumia data unapotumia tovuti au programu za washirika wetu.

Unavyotazama na kutumia maudhui na matangazo

Kwa mfano tunakusanya maelezo kuhusu mara ulizotazama, pamoja na mawasiliano na matangazo ili tuweze kutoa ripoti za ujumlisho kwa watangazaji, kama vile kuwaambia iwapo tuliweka tangazo lao kwenye ukurasa na iwapo mtazamaji aliweza kuliona tangazo. Pia tunaweza kupima utumiaji mwingine, kama vile unavyosogeza kipanya chako juu ya tangazo au ikiwa unatumia ukurasa ambapo tangazo linaonekana.

usalama na kuaminika

Baadhi ya mifano ya jinsi tunavyotumia maelezo yako ili yatusaidie kuweka huduma zetu salama na za kuaminika ni pamoja na:

  • Kukusanya na kuchanganua anwani za IP na data ya vidakuzi ili kulinda dhidi ya matumizi mabaya ya kiotomatiki. Matumizi haya mabaya huchukua njia nyingi, kama vile kutuma taka kwa watumiaji wa Gmail, kuiba pesa kwa ulaghai kutoka kwa watangazaji kwa kubofya visivyo kwenye matangazo, au kukomesha maudhui kwa kuzindua uvamizi wa Distributed Denial of Service (DDoS).
  • Kipengele cha “shughuli za hivi punde za akaunti” katika Gmail kinaweza kukusaidia kujua ikiwa mtu aliingia katika akaunti yako ya barua pepe na wakati alifanya hivyo bila ufahamu wako. Kipengele hiki hukuonyesha maelezo kuhusu shughuli za hivi majuzi katika Gmail, kama vile anwani za IP ambazo zilifikia barua pepe yako, eneo linalohusiana, pamoja na wakati na tarehe. Pata maelezo zaidi

vifaa

Kwa mfano, tunaweza kutumia maelezo kutoka kwenye vifaa vyako ili yakusaidie kujua ni kifaa kipi ungependa kutumia kusakinisha programu au kutazama filamu unayonunua kutoka Google play. Pia tunatumia maelezo haya ili tusaidie kulinda akaunti yako.

vyanzo vinavyofikiwa na umma

Kwa mfano, tunaweza kukusanya maelezo yanayopatikana mtandaoni kwa umma au kutoka vyanzo vingine vya umma ili kusaidia kufunza mifano ya lugha ya Google na kujenga vipengele kama vile Google Tafsiri. Au, iwapo maelezo ya biashara yako yanaonekana kwenye tovuti, tunaweza kuyaainisha na kuyaonyesha kwenye huduma za Google.

washirika mahususi

Kwa mfano, tunaruhusu wabunifu na watangazaji wa YouTube kufanya kazi na kampuni za vipimo ili kupata maelezo zaidi kuhusu watazamaji wa video au matangazo yao ya YouTube, kwa kutumia vidakuzi au teknolojia zinazofanana. Mfano mwingine ni wauzaji kwenye kurasa zetu za ununuzi, ambao hutumia vidakuzi kuelewa jinsi watu tofauti huona bidhaa zao kwenye ukurasa unaoorodhesha bidhaa. Pata maelezo zaidi kuhusu washirika hawa na jinsi wanavyotumia maelezo yako.

watu ambao ni muhimu kwako zaidi mtandaoni

Kwa mfano, unapocharaza anwani katika sehemu ya Kwa, Nakala kwa, au Nakala fiche kwa ya barua pepe unayoandika, Gmail itapendekeza anwani kutoka kwa watu unaowasiliana nao mara nyingi.

watu wengine

Kwa mfano, tunachakata maelezo yako ili turipoti takwimu za matumizi kwa wamiliki wa haki kuhusu vile maudhui yao yalivyotumika katika huduma zetu. Pia tunaweza kuchakata maelezo yako ikiwa watu watatafuta jina lako na tutaonyesha matokeo ya utafutaji kwa tovuti zilizo na maelezo yanayokuhusu ambayo yanapatikana kwa umma.

Programu za Google
Menyu kuu