Mifumo ya kisheria ya kuhamisha data

Inatumika kuanzia 25 Mei 2018

Sheria za ulinzi wa data ni tofauti katika kila nchi. Kuna nchi ambazo hutoa ulinzi zaidi kuliko nyingine. Maelezo yako yatashughulikiwa popote kwa kuzingatia sheria za ulinzi wa data kama ilivyofafanuliwa kwenye Sera ya Faragha. Pia tunazingatia mifumo fulani ya kisheria ya kuhamisha data, kama vile mifumo ya Ulaya iliyoelezwa hapa chini.

Tume ya Ulaya imebaini kuwa baadhi ya nchi zilizo nje ya Eneo la Uchumi wa Ulaya (EEA) zinatoa ulinzi wa kutosha wa data binafsi. Unaweza kuona sheria za sasa za kulinda data za Tume ya Ulaya hapa. Ili kuhamisha data kutoka Eneo la Uchumi wa Ulaya yaani EEA kwenda nchi nyingine, kama vile Marekani, tunazingatia mifumo ya kisheria yenye viwango sawa vya ulinzi na sheria za Umoja wa Ulaya.

EU-US na Swiss-US Privacy Shield frameworks

Kama ilivyoelezewa katika uthibitisho wetu wa Privacy Shield , tunazingatia EU-US na Swiss-US Privacy Shield Frameworks kama ilivyobainishwa na Idara ya Biashara ya Marekani kuhusu ukusanyaji, matumizi na uwekaji wa maelezo ya kibinafsi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na Uswizi mtawalia. Google, pamoja na Google LLC na kampuni zake tanzu zilizo Marekani, imethibitisha kuwa inatii Kanuni za Privacy Shield. Bado Google inawajibika kwa maelezo yako yoyote ya binafsi yanayoshirikiwa chini ya Kanuni ya Uhamishaji na wahusika wengine kwa ajili ya uchakataji wa nje kwa niaba yetu, kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya “Kushiriki maelezo yako”. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu mpango wa Privacy Shield na kuangalia uthibitisho wa Google, tafadhali tembelea tovuti ya Privacy Shield.

Ikiwa una swali lolote kuhusu desturi zetu za faragha zinazohusiana na uthibitisho wetu wa Ngao ya Faragha (Privacy Shield), tunakuhimiza uwasiliane nasi. Google inategemea mamlaka ya uchunguzi na utekelezaji ya Tume ya Biashara ya Marekani (FTC). Pia unaweza kutuma malalamiko kwenye mamlaka inayolinda data ya eneo lako na tutashirikiana nayo kutatua tatizo lako. Katika hali fulani, Mfumo wa Ngao ya Faragha (Privacy Shield Framework) unatoa haki ya kutekeleza upatanishi wa kushurutishwa ili kusuluhisha malalamiko ambayo hayajasuluhishwa kwa njia nyingine, kama inavyoelezewa katika Kiambatisho cha I kwenye Kanuni za Ngao ya Faragha (Privacy Shield Principles) .

Vifungu maalum vya mkataba

Tume ya Ulaya imeidhinisha kutekelezwa kwa vifungu maalum vya mkataba ili kuhakikisha kuwa data inalindwa kwa njia ya kutosha inapohamishwa nje ya EEA. Kwa kujumuisha vifungu maalum vya mkataba kwenye mkataba ulioafikiwa na wanaohamisha data, data binafsi inaweza kulindwa inapohamishiwa nje ya EEA kwenda nchi ambazo hazijathibitishwa na Tume ya Ulaya kuwa zinaweza kutoa ulinzi wa kutosha wa data binafsi.

Google inatoa vifungu hivi maalum vya mkataba kwa wateja wa huduma zake za biashara ikiwemo GSuite na Google Cloud Platform. Maelezo kuhusu matumizi ya Google ya vifungu maalum vya mkataba yanapatikana kwenye privacy.google.com/businesses.