Washirika wa Google ni nani?

Google hushirikiana na mashirika na biashara kwa njia mbalimbali. Sisi hurejelea biashara na mashirika haya kama "washirika". Kwa mfano, tovuti na programu zaidi ya milioni 2 zisizo za Google hushirikiana na Google kuonyesha matangazo. Mamilioni ya washirika wasanidi programu huchapisha programu zao kwenye Google Play. Washirika wengine husaidia Google kwa kuimarisha usalama wa huduma zetu; maelezo kuhusu vitisho vya usalama yanaweza kutusaidia kukujulisha ikiwa tunahofia kuwa akaunti yako imeathiriwa (ambapo tunaweza kukusaidia kuchukua hatua za kulinda akaunti yako).

Kumbuka kuwa sisi pia hushirikiana na biashara zinazoaminika ili zifanye kazi kama "wachakataji wa data" badala ya washirika, kumaanisha kuwa wanachakata maelezo kwa niaba yetu, kusaidia utoaji huduma zetu, kulingana na maagizo yetu na kwa kutii Sera yetu ya Faragha na hatua nyinginezo za siri na usalama. Sera ya Faragha ya Google ina maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia wachakataji wa data.

Maelezo yanayokusanywa au kupokewa na washirika wa matangazo wa Google

Washirika maalum, walioorodheshwa hapa chini, wanaweza kukusanya au kupokea maelezo yasiyokutambulisha binafsi kuhusu kivinjari au kifaa chako wakati unatumia tovuti na programu za Google. Washirika hawa hukusanya maelezo haya kwa madhumuni ya utangazaji na vipimo vya matangazo, kwa kutumia vidakuzi vyao au teknolojia zinazofanana.

Kwa mfano, tunaruhusu wabunifu na watangazaji wa YouTube kufanya kazi na kampuni za vipimo ili kupata maelezo zaidi kuhusu watazamaji wa video au matangazo yao ya YouTube, kwa kutumia vidakuzi au teknolojia zinazofanana.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi washirika hawa mahususi wanavyokusanya na kutumia maelezo yako:

YouTube pia huwawezesha watangazaji na watayarishi kuonyesha matangazo moja kwa moja, kwa kutumia teknolojia zao za kuonyesha matangazo, nje ya nchi za EEA.

Mfano mwingine ni wauzaji kwenye kurasa zetu za ununuzi, ambao hutumia vidakuzi kuelewa jinsi watu tofauti huona bidhaa zao kwenye ukurasa unaoorodhesha bidhaa.

Hatuwapi washirika wetu wa matangazo maelezo ambayo yanakutambua binafsi, kama vile jina lako au anwani ya barua pepe, isipokuwa ukituomba tufanye hivyo. Kwa mfano, ukiona tangazo la duka la maua lililo karibu nawe kisha uchague kitufe cha "gusa ili upige simu", tutaunganisha simu yako na tunaweza kushiriki nambari yako ya simu na duka hilo la maua.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu maelezo ambayo Google hukusanya, ikijumuisha kutoka kwa washirika, katika Sera ya Faragha.