Matangazo

Matangazo hukuwezesha kutumia Google na tovuti na huduma nyingi unazotumia bila malipo. Sisi hutia bidii kuhakikisha kuwa matangazo ni salama, yasiyosumbua na yanakufaa zaidi iwezekanavyo. Kwa mfano, hutaona matangazo ibukizi kwenye Google na tunazifunga akaunti za mamia ya maelfu ya wachapishaji na watangazaji wanaokiuka sera zetu kila mwaka – pamoja na matangazo yaliyo na programu hasidi, matangazo ya bidhaa bandia au matangazo yanayojaribu kutumia vibaya maelezo yako ya kibinafsi.

Jinsi Google hutumia vidakuzi katika matangazo

Vidakuzi husaidia kufanya matangazo kuwa bora zaidi. Bila vidakuzi, ni vigumu kwa mtangazaji kufikia hadhira yake au kujua ni matangazo mangapi yaliyoonyeshwa na ni mibofyo mingapi iliyopokewa.

Tovuti nyingi, kama vile tovuti za habari na blogu, hushirikiana na Google kuonyesha matangazo kwa wageni wao. Tukifanya kazi na washirika wetu, tunaweza kutumia vidakuzi kwa madhumuni kadhaa, kama vile kukusitisha kuona tangazo sawa tena na tena, kugundua na kusitisha udanganyifu wa kubofya, na kuonyesha matangazo ambayo yana uwezekano wa kuwa wa maana zaidi (kama vile matangazo yanayolingana na tovuti ulizotembelea).

Tunahifadhi rekodi ya matangazo tunayoyatoa katika kumbukumbu zetu. Kumbukumbu hizi za seva kwa kawaida hujumuisha ombi lako la wavuti, anwani ya IP, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na wakati wa ombi lako na moja au zaidi ya vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari chako kipekee. Tunahifadhi data hii kwa sababu kadhaa, ya muhimu kabisa ni kuboresha huduma zetu na kudumisha usalama wa mifumo yetu. Sisi huondoa utambulisho wa data hii ya kumbukumbu kwa kuondoa sehemu ya anwani ya IP (baada ya miezi 9) na maelezo ya kidakuzi (baada ya miezi 18).

Vidakuzi vyetu vya utangazaji

Ili kusaidia washirika wetu kudhibiti matangazo yao na tovuti, sisi hutoa bidhaa nyingi, ikiwa ni pamoja na AdSense, AdWords, Google Analytics, na huduma mbalimbali zilizochapishwa za DoubleClick. Unapotembelea ukurasa au kuona tangazo linalotumia moja ya bidhaa hizi, iwe kwenye huduma za Google au kwenye tovuti na programu zingine, huenda vidakuzi mbalimbali vikatumwa kwenye kivinjari chako.

Vidakuzi vinaweza kuwekwa kutoka vikoa kadhaa tofauti, ikiwa ni pamoja na google.com, doubleclick.net, googlesyndication.com, googleadservices.com, au vikoa vya tovuti za washirika wetu. Baadhi ya bidhaa zetu za utangazaji huwezesha washirika wetu kutumia huduma nyingine kwa kushirikiana na bidhaa zetu (kama vile kipimo cha tangazo na huduma ya kuripoti) na huduma hizi zinaweza kutuma vidakuzi vyake kwenye kivinjari chako. Vidakuzi hivi vitawekwa kutoka vikoa vyao.

Tazama maelezo zaidi kuhusu aina za vidakuzi vinavyotumiwa na Google na washirika wetu, na jinsi tunavyovitumia.

Jinsi unavyoweza kudhibiti vidakuzi vya utangazaji

Unaweza kutumia Mipangilio ya Matangazo kudhibiti matangazo ya Google unayoona na kujiondoa kwenye Matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia. Hata ukijiondoa kwenye Matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia, bado unaweza kuona matangazo kulingana na mambo kama vile mahali ulipo kwa jumla kutokana na anwani yako ya IP, aina ya kivinjari chako na hoja zako za utafutaji.

Unaweza pia kudhibiti vidakuzi vya kampuni nyingi vinavyotumiwa kwa utangazaji wa mtandaoni kupitia zana za chaguo za wateja chini ya programu za kujidhibiti katika nchi nyingi, kama vile ukurasa wa nchini Marekani unaoitwa aboutads.info choices au programu ya Ulaya inayoitwa Your Online Choices.

Hatimaye, unaweza kudhibiti vidakuzi katika kivinjari chako .

Teknolojia zingine zinazotumika katika utangazaji

Mifumo ya Google ya utangazaji inaweza kutumia teknolojia zingine, ikiwa ni pamoja na Flash na HTML5, kwa utendakazi kama uonyeshaji wa maumbizo ya kuingiliana ya matangazo. Tunaweza kutumia anwani ya IP, kwa mfano, ili kutambua eneo lako kwa jumla. Pia tunaweza kuchagua utangazaji kulingana na maelezo kuhusu kompyuta au kifaa chako, kama vile muundo wa kifaa chako, aina ya kivinjari, au kitambuzi katika kifaa chako kama kipima uchapuzi.

Eneo

Bidhaa za matangazo ya Google zinaweza kupokea au kutambua maelezo kuhusu mahali ulipo kutoka vyanzo tofauti. Kwa mfano, tunaweza kutumia anwani ya IP kutambua mahali pa jumla ulipo; tunaweza kupokea mahali sahihi ulipo kutoka kifaa chako cha mkononi. Tunaweza kukisia mahali ulipo kutokana na hoja ulizotafuta; na tovuti au programu ambazo unatumia zinaweza kututumia maelezo kuhusu mahali ulipo. Google hutumia maelezo ya mahali katika bidhaa zake za matangazo kutambua maelezo ya kidemografia ili kuboresha umuhimu wa matangazo unayoona, kutathmini utendaji wa tangazo na kuripoti kuhusu takwimu za jumla kwa watangazaji.

Vitambulishaji vya utangazaji vya programu za vifaa vya mkononi

Kutoa matangazo katika huduma ambazo teknolojia ya vidakuzi huenda haipatikani (kwa mfano, katika programu za vifaa vya mkononi), tunaweza kutumia teknolojia zinazotekeleza kazi sawa na vidakuzi. Wakati mwingine, Google huunganisha kitambulishi kinachotumika kutangaza kwenye programu za vifaa vya mkononi kwenye kidakuzi cha matangazo kwenye kifaa sawa ili kuratibu matangazo kwenye programu zote za kifaa chako cha mkononi na kivinjari cha kifaa chako. Kwa mfano, hili linaweza kutokea unapoona tangazo kwenye programu inayofungua ukurasa wa wavuti katika kivinjari cha kifaa chako cha mkononi. Hii pia hutusaidia kuimarisha ripoti tunazotoa kwa watangazaji wetu kuhusu ufanisi wa kampeni zao.

Ili kuchagua kutopokea matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia katika programu kwenye kifaa chako cha mkononi, fuata maagizo yaliyo hapa chini.

Android

  1. Tafuta Mipangilio ya Google katika mojawapo ya sehemu hizi (kulingana na kifaa chako):
    1. Programu tofauti inayoitwa Mipangilio ya Google
    2. Katika programu yako kuu ya Mipangilio, sogeza chini na ugonge Google
  2. Gonga Matangazo
  3. Washa Chagua kutopokea matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia

iOS

Vifaa vyenye iOS hutumia Kitambulishi cha Utangazaji cha Apple. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu uamuzi wako wa kutumia kitambulishi hiki, tembelea programu ya Mipangilio kwenye kifaa chako.

Je, ni nini kinachoamua matangazo ambayo ninaona ya Google?

Maamuzi mengi hufanywa ili kuamua ni tangazo lipi unaloona.

Wakati mwingine tangazo unaloliona linalingana na mahali ulipo sasa au ulipokuwa awali. Kwa kawaida, anwani yako ya IP ni ishara nzuri ya ukadiriaji wa eneo ulipo. Kwa hivyo huenda ukaona tangazo kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube.com linalotangaza filamu inayopangiwa kutolewa hivi karibuni nchini mwako, au utafutaji wa "piza" unaweza kukupa matokeo ya mikahawa ya piza mjini mwako.

Wakati mwingine tangazo unaloona linalingana na muktadha wa ukurasa. Ikiwa unatazama ukurasa wa vidokezo vya kilimo cha bustani, unaweza kuona matangazo ya vifaa vya kilimo cha bustani.

Wakati mwingine unaweza kuona tangazo kwenye wavuti kulingana na shughuli zako za programu, au shughuli kwenye huduma za Google; tangazo kwenye programu kulingana na shughuli zako kwenye wavuti; au tangazo kulingana na shughuli zako kwenye kifaa kingine.

Wakati mwingine tangazo unaloona kwenye ukurasa linatolewa na Google lakini limechaguliwa na kampuni nyingine. Kwa mfano, unaweza kuwa umejisajili na tovuti ya gazeti. Kutoka kwa maelezo ambayo umetoa kwa gazeti, inaweza kutoa uamuzi kuhusu ni matangazo yapi ya kukuonyesha, na inaweza kutumia bidhaa za Google za kutoa matangazo ili kuwasilisha matangazo hayo.

Pia unaweza kuona matangazo kwenye bidhaa na huduma za Google, ikiwa ni pamoja na Huduma ya Tafuta na Google, Gmail, na YouTube, kulingana na maelezo kama vile anwani yako ya barua pepe uliyowapa watangazaji na baadaye watangazaji wakaishiriki na Google.

Je, kwa nini ninaona matangazo ya Google kwa bidhaa ambazo nimetazama?

Unaweza kuona matangazo ya bidhaa ulizotazama awali. Kwa mfano tuchukulie umetembelea tovuti ambayo inauza vifaa vya gofu, lakini hununui vifaa hivyo katika ziara yako ya kwanza. Mmiliki wa tovuti anaweza kuamua kukuhimiza urejee na ukamilishe ununuzi wako. Google hutoa huduma ambazo huwaruhusu waendeshaji wavuti kuelekeza matangazo yao kwa watu ambao wametembelea kurasa zao.

Ili hatua hii ifanye kazi, Google husoma kidakuzi ambacho tayari kiko katika kivinjari chako au huhifadhi kidakuzi katika kivinjari chako unapotembelea tovuti hiyo ya gofu, (ikichukuliwa kwamba kivinjari chako huruhusu kuhifadhi vidakuzi).

Unapotembelea wavuti nyingine ambayo inafanya kazi na Google, ambayo haina chochote cha kufanya na gofu, unaweza kuona tangazo la vifaa hivyo vya gofu. Hiyo ni kwa sababu kivinjari chako hutumia Google kidakuzi hicho hicho. Kwa upande mwingine, tunaweza kutumia kidakuzi hicho kukupa tangazo ambalo linaweza kukuhimiza ununue vifaa hivyo vya gofu.

Tembeleo lako kwenye tovuti ya gofu pia linaweza kutumiwa na Google kukuonyesha matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia utakapotafuta vifaa vya gofu kwenye Google.

Tumeweka vikwazo kuhusu aina hii ya tangazo. Kwa mfano, tunawakataza watangazaji kuchagua hadhira kulingana na maelezo nyeti, kama vile maelezo kuhusu afya au imani za kidini.

Pata maelezo zaidi kuhusu matangazo ya Google.

Programu za Google
Menyu kuu