Mwongozo wa Faragha kwa Vijana
Faragha yako kwenye Google
Hapa ndipo unaweza kupata majibu ya baadhi ya maswali tunayoulizwa sana kuhusu faragha, kama vile Data ni nini? Soma pia Sera ya Faragha iwapo ungependa kupata maelezo zaidi.
Mahali ulipo
Je, Google hujua mahali nilipo?
Wakati wowote ukitumia intaneti, programu na tovuti zinaweza kukadiria mahali ulipo na Google pia inaweza kufanya hivyo. Google inaweza pia kujua eneo mahususi ulipo, kulingana na mipangilio ya kifaa chako. (Angalia sehemu ya Data ya mahali nilipo ni mahususi kwa kiasi gani?)
Ukitafuta kwenye Google, kama vile ukitumia huduma ya Tafuta, Ramani au Kiratibu cha Google, maelezo ya mahali ulipo kwa wakati huo yanaweza kutumiwa ili kukupa matokeo yanayokufaa zaidi. Kwa mfano, ukitafuta migahawa, matokeo yanayokufaa zaidi yanaweza kuwa migahawa iliyo karibu na mahali ulipo.
Angalia sehemu ya Jinsi unavyoweza kudhibiti data ya mahali ulipo
Ninawezaje kuwasha au kuzima mipangilio ya mahali?
Ukitafuta kwenye Google, Google itakadiria eneo la jumla ambako unatafutia, kila wakati. Sawa na programu au tovuti yoyote unayotumia inayounganishwa na Intaneti, Google inaweza kukadiria mahali ulipo kulingana na anwani ya IP ya kifaa chako. Kwa maelezo zaidi, angalia sehemu ya Google hujuaje mahali nilipo?
Ili uchague iwapo ungependa kutuma maelezo ya eneo mahususi ulipo wakati unatumia Google, unaweza kuwasha au kuzima ruhusa za mahali kwenye programu au tovuti mahususi na kwenye kifaa chako.
Ukiweka anwani yako ya nyumbani au ya kazini na Google ikadirie kwamba upo nyumbani au kazini, basi anwani hiyo mahususi itatumiwa kwenye utafutaji wako.
Data ya mahali nilipo ni mahususi kwa kiasi gani?
Eneo la jumla ulipo
Ukitafuta kwenye Google, Google itakadiria eneo la jumla ambako unatafutia, kila wakati. Kwa njia hii, Google inaweza kukupa matokeo yanayofaa na kuimarisha usalama wa akaunti yako kwa kutambua shughuli zisizo za kawaida, kama vile tukio la kuingia katika akaunti kwenye jiji tofauti.
Eneo la jumla ni kubwa kuliko kilomita tatu mraba na lina angalau watumiaji 1,000 ili eneo la jumla ambako unatafutia lisikutambulishe. Hali hii husaidia kulinda faragha yako.
Eneo mahususi ulipo
Ukiiruhusu, Google inaweza kutumia maelezo ya eneo mahususi ulipo. Kwa mfano, Google inahitaji maelezo ya eneo mahususi ulipo ili ikupe matokeo yanayokufaa zaidi ukitafuta vitu kama vile “aiskrimu karibu nami” au maelekezo ya kutembea hatua kwa hatua kuelekea dukani.
Eneo mahususi linamaanisha mahali ulipo haswa, kama vile anwani maalum.
Google hujuaje mahali nilipo?
Data yako ya mahali hutokana na vyanzo tofauti vinavyotumiwa kwa pamoja kukadiria mahali ulipo.
Anwani ya IP ya kifaa chako
Anwani za IP kimsingi hutegemea maeneo ya kijiografia, kama ilivyo misimbo ya maeneo ya namba za simu. Hii inamaanisha kwamba programu au tovuti yoyote unayotumia, ikiwa ni pamoja na google.com, inaweza kukadiria eneo la jumla ulipo kutokana na anwani yako ya IP. Anwani ya IP ya kifaa chako hukabidhiwa kifaa chako na Mtoa Huduma za Intaneti na inahitajika ili utumie intaneti.
Mahali kifaa chako kilipo
Ukiipa programu au tovuti ya Google ruhusa ya kutumia maelezo ya mahali kifaa chako kilipo, maelezo hayo yanaweza kutumika kusaidia kuelewa mahali ulipo. Takriban vifaa vyote vina mipangilio ya mahali iliyojumuishwa kwenye mfumo wa uendeshaji, kwa kawaida huwa katika mipangilio.
Shughuli zako kwenye Google
Google inaweza kukadiria eneo la jumla uliko, kutokana na utafutaji wako wa awali kwenye Google. Kwa mfano, ikiwa una mazoea ya kutafuta maeneo ya piza Mumbai, inawezekana ungependa kuona matokeo yaliyo katika eneo la Mumbai.
Maeneo uliyowekea lebo
Ukiweka anwani yako ya nyumbani au ya kazini, Google inaweza kuitumia kukadiria mahali ulipo. Kwa mfano, iwapo umeweka anwani yako ya nyumbani, anwani ya IP, shughuli zako za awali au vyanzo vingine vya maelezo ya mahali vikidokeza kwamba huenda uko karibu na nyumbani, basi tutatumia eneo la nyumbani kwako kukadiria mahali ulipo.
Ni nani anaweza kuona data ya mahali nilipo?
Uamuzi ni wako. Ukitumia Kipengele cha Google cha Kuruhusu Ufikiaji wa Data ya Mahali, unaweza kuruhusu marafiki na familia yako wafikie data ya mahali ulipo katika wakati halisi kwenye huduma mbalimbali za Google.
Angalia iwapo unaruhusu ufikiaji wa data ya mahali ulipo
Kipengele cha Kuruhusu Ufikiaji wa Data ya Mahali kimezimwa kwa chaguomsingi. Iwapo ungependa kuruhusu ufikiaji wa data ya mahali ulipo katika wakati halisi, unahitaji kuchagua na kuthibitisha unayetaka aifikie na kwa muda gani. Unaweza kuacha kuruhusu ufikiaji wa data ya mahali ulipo wakati wowote.
Angalia sehemu ya Kuruhusu wengine wafikie data ya mahali ulipo katika wakati halisi
Kutuma maudhui kwenye Google
Watu wengine wanaweza kuona maelezo gani nikiruhusu ufikiaji kwenye Google?
Maelezo ambayo watu wengine wanaweza kuona kukuhusu kwenye huduma za Google yanategemea maelezo unayoruhusu yafikiwe na jinsi unavyoruhusu:
Kuruhusu ufikiaji hadharani
Ukichangia kwenye programu kama vile Ramani za Google, watu wengine wanaweza kuona jina na picha yako. Kwa mfano, ukikadiria duka la aiskrimu ulipendalo, watu wengine wanaweza kuona ukadiriaji wako, jina na picha yako wakiangalia maelezo ya duka hilo kwenye Ramani za Google.
Kuruhusu ufikiaji kwa faragha
Ukiwatumia wengine vitu kama vile picha, video na hati, jina na picha yako huonekana kwa mtu unayemtumia pamoja na maudhui unayotuma.
Fikiria kwa makini kabla ya kuwaruhusu wengine wafikie maudhui yako na uelewe kiwango cha idhini ya kufikia unachowapa. Kwa mfano, ukiruhusu ufikiaji wa vitu kama vile folda katika Hifadhi ya Google au albamu katika huduma ya Picha kwenye Google, huenda watu wakaendelea kuwa na idhini ya kufikia kadiri unavyoongeza maudhui mapya.
Ni nani anayeweza kuona vitu ninavyoruhusu vifikiwe, kama vile picha, video na hati?
Unaweza kuchagua kuruhusu watu wengine wafikie maudhui mahususi katika huduma za Google unazotumia.
Usisahau kwamba ukiruhusu maudhui yafikiwe, inawezekana watu wengine wakaruhusu yafikiwe tena, hata katika programu na tovuti zilizo nje ya Google.
Unaweza kufuta maudhui yako mwenyewe kwenye akaunti yako wakati wowote, lakini hatua hii haifuti nakala ambazo tayari umeruhusu zifikiwe.
Kuwa makini kuhusu maudhui unayoruhusu yafikiwe na uruhusu yafikiwe tu na watu unaowaamini.
Je, Google huruhusu wengine wafikie taarifa zangu binafsi?
Haturuhusu taarifa zako binafsi zifikiwe na kampuni, mashirika au watu binafsi nje ya Google isipokuwa katika hali chache kama vile tukihitajika na sheria kufanya hivyo.
Ikiwa una Akaunti ya Google kupitia shule yako (akaunti ya Google Workspace for Education), msimamizi wa shule anayedhibiti akaunti yako atakuwa na uwezo wa kufikia taarifa zako.
Uwezo wa kufikia wa wasimamizi wa shule
Huenda msimamizi wa shule yako akaweza kufikia taarifa zifuatazo katika akaunti yako ya Google Workspace for Education:
- Kufikia na kudumisha maelezo yaliyohifadhiwa katika akaunti yako, kama vile barua pepe zako
- Kuona takwimu kuhusu akaunti yako, kama vile idadi ya programu unazosakinisha
- Kubadilisha nenosiri la akaunti yako
- Kusimamisha au kukomesha ufikiaji wa akaunti yako
- Kupokea maelezo ya akaunti yako ili kutimiza sheria, kanuni, mchakato wa kisheria, au ombi husika la kutekelezeka la kiserikali
- Kuzuia uwezo wako wa kufuta au kubadilisha maelezo au mipangilio yako ya faragha
Sababu za Google kuruhusu taarifa zako zifikiwe
Ukitupatia ruhusa
Kwa mfano, ukitumia Kiratibu cha Google kuagiza piza, tutaomba ruhusa yako kabla ya kuruhusu mgahawa husika ufikie jina au namba yako ya simu. Angalia sehemu ya Jinsi Google inavyokusaidia kuruhusu huduma na programu za wengine zifikie data kwa usalama
Na wasimamizi wa vikoa, kama ilivyoelezwa hapo juu.
Kwa madhumuni ya uchakataji wa nje, Huwa tunazipatia kampuni tunazofanya nazo kazi taarifa binafsi ili ziweze kuchakata data kulingana na maagizo tunayozipa. Kwa mfano, tunatumia kampuni za nje ili zitusaidie kutoa usaidizi kwa wateja na tunalazimika kuruhusu kampuni hizo zifikie taarifa binafsi ili ziweze kujibu maswali ya watumiaji.
Kwa sababu za kisheria
Tutaruhusu taarifa binafsi zifikiwe nje ya Google ikiwa tunaamini kuwa kufanya hivyo ni muhimu ili:
- Kutimiza sheria, kanuni, mchakato wa kisheria au ombi lolote la utekelezaji la kiserikali ambalo linakubalika.
- Kutekeleza Sheria na Masharti yanayotumika, ikiwemo uchunguzi wa ukiukaji unaoweza kutokea.
- Kugundua, kuzuia, au kushughulikia ulaghai, masuala ya usalama au kiufundi.
- Kulinda dhidi ya ukiukaji wa haki, madhara kwa mali au usalama wa Google, watumiaji wetu au umma inavyohitajika au kuruhusiwa na sheria.
Data na uwekaji mapendeleo
Google hukusanya data gani kunihusu?
Ukitumia huduma za Google, huwa tunakusanya taarifa tunazohitaji ili kukupa huduma hizo, kuzifanya zikufae zaidi na kwa sababu nyingine kama ilivyofafanuliwa katika sehemu ya Kwa nini Google hukusanya data?.
Ukitumia mipangilio yako, unaweza kudhibiti data tunayokusanya na jinsi data hiyo inavyotumiwa. Kwa mfano, iwapo hutaki tuhifadhi Historia yako ya YouTube kwenye Akaunti yako ya Google, unaweza kuzima kipengele cha Historia ya YouTube. Angalia sehemu ya Ninawezaje kuamua data inayohifadhiwa na Google?
Data ni nini?
Taarifa zako binafsi ni pamoja na data unayotupatia inayokutambulisha, kama vile jina lako au anwani yako ya barua pepe. Pia ni pamoja na data nyingine ambayo Google inaweza kuhusisha nawe, kama vile taarifa tunazohusisha nawe katika Akaunti yako ya Google.
Taarifa zako binafsi zinajumuisha vitu vya aina mbili:
Data unayotoa au kutayarisha
Ukifungua Akaunti ya Google, unatupatia taarifa binafsi kama vile jina lako na nenosiri.
Unaweza pia kuhifadhi maudhui unayotayarisha, unayopakia au kupokea kutoka kwa watu wengine, kama vile ujumbe wa barua pepe pamoja na picha.
Mambo unayofanya kwenye Google
Huwa tunakusanya taarifa kuhusu shughuli zako katika huduma zetu. Taarifa hizo zinaweza kujumuisha vitu kama vile hoja unazozitafuta na video unazotazama, watu unaowasiliana nao au unaowatumia maudhui na historia yako ya kuvinjari kwenye Chrome ili tuweze kuboresha hali yako ya utumiaji.
Huwa tunakusanya taarifa kuhusu programu, vivinjari na vifaa unavyotumia kufikia huduma za Google. Kufanya hivyo hutusaidia kutoa vipengele kama vile kupunguza mwangaza wa skrini yako ikiwa chaji ya betri yako inakaribia kuisha.
Sisi huchakata data ya mahali ulipo, kwa mfano wakati unatumia vipengele kama vile maelekezo ya hatua kwa hatua. Kwa maelezo zaidi, angalia sehemu ya Mahali.
Kwa nini Google hukusanya data?
Huwa tunakusanya taarifa tunazohitaji ili kutoa huduma zetu, kuzifanya zikufae zaidi na kwa sababu nyingine kama ilivyofafanuliwa katika sehemu ya "Jinsi tunavyotumia data".
Kwa mfano, huduma ya Ramani za Google inaweza kukusaidia kufika unakokwenda kwa kuepuka msongamano wa magari kwa sababu inakusanya maelezo kuhusu mahali ulipo (data yako) na data ya umma (ramani na maelezo kuhusu maeneo ya umma).
Jinsi tunavyotumia data
Kutoa huduma zetu
Sisi hutumia data kutoa huduma zetu, kama vile kuchakata hoja unazotafuta ili tukupe matokeo.
Kudumisha na kuboresha huduma zetu
Data hutusaidia kudumisha na kuboresha huduma zetu. Kwa mfano, tunaweza kufuatilia hitilafu. Kutambua hoja za utafutaji zinazondelezwa visivyo mara kwa mara hutusaidia kuboresha vipengele vya kikagua tahajia vinavyotumika katika huduma zetu mbalimbali.
Kuunda huduma mpya
Data hutusaidia kubuni huduma mpya. Kwa mfano, tuliweza kuelewa jinsi watu walivyopanga picha zao katika programu yetu ya kwanza ya picha, Picasa na tukatumia data hiyo kusaidia kubuni na kuzindua huduma ya Picha kwenye Google. Na tunaweza kutumia data ya matumizi yako ya huduma zetu, ikiwa ni pamoja na bidhaa zetu za akiliunde zalishi, kubuni na kuboresha huduma hizi.
Kutoa huduma zinazokufaa, ikiwa ni pamoja na maudhui na matangazo
Huwa tunatumia data kutoa maudhui yaliyowekwa mapendeleo, kwa mfano, mapendekezo ya video ambazo huenda ukazipenda. Kulingana na mipangilio uliyoweka na umri wako, huenda tukakuonyesha matangazo yaliyowekwa mapendeleo kwa kutegemea mambo yanayokuvutia.
Pima utendaji
Pia, huwa tunatumia data kupima utendaji na kuelewa jinsi huduma zetu zinavyotumiwa
Kuwasiliana nawe
Huenda tukatumia anwani yako ya barua pepe kukutumia arifa tukitambua shughuli ya kutiliwa shaka
Kulinda Google, watumiaji wetu na umma
Huwa tunatumia data kuimarisha usalama wa watu mtandaoni, kama vile kutambua na kuzuia ulaghai
Google hutumia vipi data kuweka mapendeleo ya vitu?
Huwa tunatumia taarifa tunazokusanya ili kufanya programu na tovuti zetu zikufae, kwa mfano:
- Mapendekezo ya video ambazo huenda ukazipenda
- Vidokezo vya usalama vinavyotokana na jinsi unavyotumia huduma za Google (angalia sehemu ya Ukaguzi wa Usalama)
Pia, huwa tunatumia data kuweka mapendeleo ya matangazo isipokuwa katika hali ambapo mipangilio hiyo imezimwa au kwa watu wenye umri fulani.
Je, Google huwekea mapendeleo matangazo ninayoyaona?
Sisi hujaribu kufanya matangazo tunayokuonyesha yawe muhimu iwezekanavyo. Lakini hatuweki mapendeleo ya matangazo kwa watu wenye umri fulani au kwa watu waliozima mipangilio ya Kuweka mapendeleo ya matangazo.
Bado tunaweza kufanya matangazo yakufae hata bila kuyawekea mapendeleo. Kwa mfano, ikiwa unatazama ukurasa wenye matokeo ya “viatu vipya,” huenda ukaona tangazo kutoka kwa kampuni ya viatu vya raba. Tangazo linaweza kutegemea vigezo vya jumla kama vile wakati, eneo la jumla uliko na maudhui ya ukurasa unaoangalia.
Udhibiti ni wako
Ninawezaje kuamua data inayohifadhiwa na Google kwenye akaunti yangu?
Wakati unatumia huduma ya Google, kama vile Picha kwenye Google, kuna mipangilio inayokuwezesha kuamua mambo kama vile iwapo ungependa kuhifadhi nakala za picha zako na kuzisawazisha.
Pia kuna mipangilio inayokuruhusu uamue iwapo maelezo kuhusu shughuli zako kwenye huduma za Google yatahifadhiwa kama historia katika Akaunti yako ya Google na iwapo huduma za Google zinaweza kutumia maelezo kwenye Akaunti yako ya Google ili kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji.
Mapendekezo Yaliyowekewa Mapendeleo katika huduma za Utafutaji
Hukuruhusu kuchagua iwapo huduma za Utafutaji, kama vile Tafuta, Ramani, Ununuzi, Hoteli, Safari za Ndege, Tafsiri na Google News, zinaweza kukupa mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo kulingana na maelezo yaliyo katika Akaunti yako ya Google, kama vile maelezo ya wasifu wako na historia iliyohifadhiwa. Kwa mfano, huduma za Utafutaji zinaweza kutumia maelezo hayo kutoa majibu ya AI yanayolingana na mambo yanayokuvutia.
Search Services History
Huhifadhi shughuli zako kwenye huduma za Utafutaji, kama vile utafutaji wako na maelezo yanayohusiana kama vile eneo la jumla uliko. Shughuli zako hutumiwa kuwekea mapendeleo hali zako za utumiaji kwenye huduma za Utafutaji. Kwa mfano, ukianza kuandika, unaweza kuona utafutaji wa awali kama mapendekezo. Google pia hutumia data yako ya Historia ya Huduma za Utafutaji kusaidia kuboresha huduma na teknolojia za Google, ikiwa ni pamoja na mifumo ya AI na kulinda Google, watumiaji wake na umma.
Kuweka Mapendeleo kwenye Google Play
Hukuruhusu uchague iwapo Google Play inaweza kutumia maelezo yaliyo katika Akaunti yako ya Google, kama vile vipengee unavyonunua na kupakua kutoka kwenye Duka la Google Play, ili kuwekea mapendeleo zaidi hali yako ya utumiaji. Kwa mfano, Google Play inaweza kujifunza kupitia programu unazotumia ili kukupendekezea programu zinazokufaa.
Historia kwenye Google Play
Huhifadhi shughuli zako kwenye Google Play, kama vile programu unazofungua kwenye kifaa chako, katika Akaunti yako ya Google. Shughuli hizi zinaweza kutumiwa kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji kwenye huduma za Google, kama vile kukusaidia kupata programu unazotafuta kwa haraka zaidi.
Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu
Huhifadhi shughuli zako kutoka kwenye baadhi ya tovuti na programu za Google, kama vile Google TV na hujumuisha maelezo yanayohusiana kama vile data ya mahali. Pia inahifadhi historia kwenye Chrome na shughuli zilizosawazishwa kutoka kwenye tovuti, programu na vifaa ambavyo vinatumia huduma za Google. Shughuli zako hutumiwa kukupa mapendekezo bora na hali za utumiaji zinazokufaa zaidi kwenye huduma za Google.
Historia ya YouTube
Huhifadhi video unazotazama na mambo unayoyatafuta wakati unatumia YouTube. Historia yako ya YouTube hutumiwa kufanya mambo kama vile kukupa mapendekezo bora na kukusaidia uendelee ulikoachia.
Shughuli kwenye Programu za Gemini
Hukuruhusu kuchagua iwapo Google inaweza kutumia shughuli zako kwenye Gemini, kama vile magumzo yako na maudhui unayoruhusu Gemini ifikie (kama vile faili na picha), ili kusaidia kuboresha huduma za Google, ikiwa ni pamoja na mifumo ya AI. Shughuli zako kwenye Programu za Gemini pia hutumiwa kufanya mambo kama vile kukuwezesha kuendeleza magumzo ulikoachia wakati wowote.
Ninawezaje kufuta data yangu?
Unaweza kufuta data iliyohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google. Data unayoamua kufuta kabisa huondolewa kwenye mifumo yetu. Tunafuata mchakato makinifu wa kuhakikisha kwamba data hii imeondolewa kabisa kwenye seva zetu au imehifadhiwa kwa njia ambayo haiwezi kuhusishwa nawe.
Tembelea sehemu ya Shughuli Zangu ili ukague shughuli zilizohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google, kama vile vidokezo ulivyoweka na vitu ulivyotafuta, ulivyosoma na kutazama. Unaweza kufuta baadhi ya shughuli zako au shughuli zako zote katika kipindi mahususi.
Unaweza pia kuchagua shughuli zako zifutwe kiotomatiki.
Ninawezaje kupakua maudhui yangu?
Maudhui yako ni pamoja na vitu kama vile barua pepe, picha, video, hati, majedwali, maoni, anwani na matukio ya kalenda.
Tembelea sehemu ya Pakua data yako ili uweke kumbukumbu ya maudhui yako — ili uyahifadhie nakala au uyapeleke kwenye kampuni nyingine iwapo ungependa kujaribu huduma tofauti.
Ninapata vidhibiti gani nikiwa nimeondoka kwenye akaunti?
Una vidhibiti vinavyokuwezesha kuchagua jinsi ya kutumia Google, hata ukiwa umeondoka kwenye akaunti. Ukiwa umeondoka kwenye akaunti, tembelea g.co/privacytools ili ubadilishe mipangilio hii:
Kuweka mapendeleo ya utafutaji
Hutumia utafutaji wako kwenye Google kutoka kwenye kivinjari hiki ili kukupa matokeo na mapendekezo yanayokufaa zaidi.
Historia ya Video Ulizotazama na Mambo Uliyotafuta kwenye YouTube
Hutumia shughuli zako kwenye YouTube, kama vile video unazotazama na mambo unayotafuta, kufanya YouTube ikufae.
Unaweza pia kuzuia baadhi au vidakuzi vyote katika kivinjari chako, lakini hatua hii inaweza kusababisha vipengele fulani kwenye wavuti viache kufanya kazi. Kwa mfano, tovuti nyingi huhitaji vidakuzi viwashwe wakati unataka kuingia katika akaunti.
Watumiaji walioondoka kwenye akaunti wanaweza pia kuchagua iwapo wangependa kuona matangazo yaliyowekwa mapendeleo, ijapokuwa hatuweki mapendeleo ya matangazo kwa watu wenye umri fulani.
